Helamani, Mwana wa Helamani
Nabii na mtunza kumbu kumbu katika Kitabu cha Mormoni ambaye aliwafundisha watu wa Nefi. Yeye alikuwa mjukuu wa kiume wa Alma Mdogo na baba wa Nefi aliyepewa uwezo juu ya vitu vyote vya asili. Pamoja na mwanawe Nefi, Helamani aliandika Kitabu cha Helamani.
Kitabu cha Helamani
Mlango wa 1–2 inaelezea wakati wa matatizo makubwa ya kisiasa. Mlango wa 3–4 inaandika kwamba, Helamani na Moroniha, jemadari mkuu wa majeshi ya Wanefi, waliweza hatimaye kupata amani kwa muda. Hata hivyo licha ya uongozi wa watu hawa wema, watu walizidi kuongezeka kuwa waovu. Katika Helamani 5:1–6:14 Nefi aliachia kiti cha hukumu, kama babu yake Alma alivyofanya, ili awafundishe watu. Kwa muda watu wakatubu. Katika Helamani 6:15–12:26, hata hivyo, taifa la Wanefi wakawa waovu. Milango ya mwisho, yaani 13–16, ina historia isiyo ya kawaida ya nabii aliyeitwa Samweli Mlamani ambaye alitabiri kuzaliwa na Kusulubiwa kwa Mwokozi na ishara ambazo zingekuwa dalili ya matukio hayo.