Kupenda anasa, Matamanio ya anasa Ona pia Tamaa mbaya; Uasherati; Usafi wa Kimwili; Utovu wa maadili ya kujamiiana; Uzinzi Hali ya kupenda au kutamani kusiko kwa haki kwa starehe ya kimwili, hususani kwa utovu wa maadili ya kujamiiana. Mke wa Bwana wake akamtamani Yusufu, Mwa. 39:7. Mtu yeyote amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha tenda uzinzi, Mt. 5:28 (3Â Ne. 12:28). Ziepukeni tamaa za mwili, zipiganazo dhidi ya roho, 1Â Pet. 2:11. Tamaa za mwili na tamaa za macho siyo za Baba, 1Â Yoh. 2:16. Usizifuate tena tamaa za macho yako, Alma 39:9. Kwa uvunjaji wa sheria hizi takatifu, mwanadamu akawa mwenye tamaa, M&M 20:20. Iwapo yeyote atafanya uzinzi mioyoni mwao, hawatakuwa na Roho Mtakatifu, M&M 63:16. Acheni tamaa zenu zote zilizo mbaya, M&M 88:121. Watu wakaanza kuwa na tamaa za kimwili, kupenda anasa, na uovu, Musa 5:13 (Mos. 16:3; Musa 6:49).