Mwaminifu, Uaminifu Ona pia Haki, Uadilifu, enye Uadilifu Kuwa mwaminifu na mkweli, na pasipo udanganyifu. Watu watendao ukweli ndiyo furaha ya Bwana, Mit. 12:22. Lipa kile ambacho umeweka nadhiri, Mh. 5:4–5. Tumeyakataa mambo yasiyo ya uaminifu yaliyositirika, 2 Kor. 4:1–2. Kuweni na mazungumzo ya uaminifu, 1 Pet. 2:12. Ole wake mtu mwongo, kwani atatupwa chini katika jehanamu, 2 Ne. 9:34. Roho husema ukweli na hasemi uongo, Yak. (KM) 4:13. Yeyote aazimaye kitu kwa jirani yake yampasa kurudisha kitu kile alichokiazima, Mos. 4:28 (M&M 136:25). Angalieni ya kuwa mnatenda haki mnaamua kwa haki, na mnatenda yaliyo mema, Alma 41:14. Kila mtu na atende kwa uaminifu, M&M 51:9. Wote wajuao kuwa katika mioyo yao ni waaminifu wanakubaliwa kwangu, M&M 97:8. Walio waaminifu wenye hekima, na watu walio wema yapaswa watafutwe kwa ajili ya ofisi za kisiasa, M&M 98:4–10. Kwa bidii tafuta kurudisha kile ambacho jirani yako amekipoteza, M&M 136:26. Tunaamini katika kuwa waaminifu, M ya I 1:13.