Kama linavyotumika katika maandiko, kusamehe kwa ujumla linaamanisha moja ya mambo mawili: (1) Mungu anapowasamehe wanadamu, yeye hufuta au huiweka pembeni adhabu inayotakiwa kwa dhambi ile. Kupitia upatanisho wa Kristo, msamaha wa dhambi unapatikana kwa wote wenye kutubu, isipokuwa wale walio na hatia ya mauaji au ile dhambi isiyo sameheka dhidi ya Roho Mtakatifu. (2) Watu wanaposameheana wao kwa wao, wanafanyiana kwa upendo kama Kristo nao wanakuwa hawana hisia mbaya kwa wale walio wakosea (Mt. 5:43–45; 6:12–15; Lk. 17:3–4; 1 Ne. 7:19–21).