Misaada ya Kujifunza
Hosana


Hosana

Neno la Kiebrania ambalo maana yake ni “tafadhali utuokoe” na hutumika katika kusifu na maombi ya unyenyekevu.

Katika Sikukuu ya Tabernakulo ambayo walikuwa wakisherehekea kukombolewa kwa Israeli na Bwana na kuingizwa katika nchi ya ahadi, watu walikuwa wakiimba maneno ya Zaburi 118 na kupepea matawi ya mitende. Bwana alipoingia kwa shangwe katika Yerusalemu, makutano waliimba “Hosana” na kutandika matawi ya mitende ili Yesu akanyage juu yake, hivyo ndivyo walivyoonyesha kufahamu kwao kwamba Yesu alikuwa ndiye yule yule Bwana aliyekuwa amewaokoa Israeli hapo kale (Zab. 118:25–26; Mt. 21:9, 15; Mk. 11:9–10; Yn. 12:13). Watu hawa walimtambua Kristo kama Masiya aliyesubiriwa kwa muda mrefu. Neno Hosana limekuwa likitumika katika kumsherehekea Masiya katika zama zote. (1 Ne. 11:6; 3 Ne. 11:14–17). Kelele za hosana zilijumuishwa katika ibada ya kuweka wakfu kwa Hekalu la Kirtland (M&M 109:79) na sasa ni sehemu ya ibada za uwekaji wakfu wa mahekalu ya kisasa.