JST, Mwanzo 9:4–6. Linganisha na Mwanzo 8:20–22
Baada ya gharika, Nuhu anamwomba Bwana kutoilaani dunia tena.
4 Na Nuhu alijenga madhabahu kwa Bwana, na akachukuwa kila mnyama aliye safi, na kila ndege aliye safi, na akamtolea dhabihu ya kuteketeza juu ya madhabahu; na akamshukuru Bwana, na akafurahi ndani ya moyo wake.
5 Na Bwana akasema na Nuhu, na alimbariki. Na Nuhu alisikia harufu ya kupendeza, na alisema moyoni mwake;
6 Nitaomba kwa jina la Bwana, ili Yeye asije tena akalaani nchi tena kwa ajili ya binadamu, kwani mawazo ya binadamu moyoni mwake ni maovu kutoka ujana wake; na kwamba yeye hatarudia tena kuangamiza kwa vyovyote vile kila kitu kinachoishi, kama alivyofanya, wakati dunia ikiendelea kuwepo;
JST, Mwanzo 9:10–15. Linganisha na Mwanzo 9:4–9
Mwanadamu anawajibika kwa kumwaga damu ya wanyama naya wanadamu. Mungu anaweka na Nuhu na wanawe agano lile lile alilofanya na Henoko.
10 Lakini damu ya wenye nyama wote ambao nimewapa ninyi kwa chakula, itamwagwa juu ya nchi, ili kutoa uhai wake, na damu yake msiile.
11 Na hakika, damu haitamwagika, isipokuwa tu kwa chakula, ili kuokoa maisha yenu; na damu ya kila mnyama nitaitaka mikononi mwenu.
12 Na yeyote atakayemwanga damu ya mwanadamu, damu yake huyo itamwangwa na mwanadamu; kwani mwanadamu hatamwaga damu ya mwanadamu.
13 Kwani amri ninawapa, kwamba kila ndugu wa binadamu ataulinda uhai wa binadamu, kwa maana kwa mfano wangu mwenyewe nilimuumba mwanadamu.
14 Na amri ninaitoa kwenu ninyi, Nanyi zaeni na muongezeke; zaeni kwa wingi sana juu ya dunia, na mkaongezeke ndani yake.
15 Na Mungu akamwambia Nuhu, na wanawe pamoja naye, akisema, Na mimi, tazama, nalithibitisha agano langu nanyi, ambalo nililifanya kwa baba yenu Henoko, juu ya uzao wenu baada yenu.
TJS, Mwanzo 9:21–25. Linganisha na Mwanzo 9:16–17
Mungu anaweka upinde wa mvua mbinguni kama ukumbusho wa agano Lake kwa Henoko na kwa Nuhu. Katika siku za mwisho mkutano mkuu wa Kanisa la Mzaliwa wa Kwanza utaungana na wenye haki duniani.
21 Na upinde utakuwepo katika mawingu; nami nitautizama, ili nipate kukumbuka agano lisilo na mwisho nililolifanya kwa baba yenu Henoko; ili, wanadamu watakapozishika amri zangu zote, Sayuni ipate kuja tena juu ya dunia, mji wa Henoko ambao nimeunyakuwa kwangu.
22 Na hili ndilo agano langu lisilo na mwisho, kwamba uzao wako utakapoukumbatia ukweli, na kutazama juu, kisha Sayuni itazame chini, na mbingu zote zitatikisika kwa furaha, na dunia itatetemeka kwa shangwe;
23 Na mkutano mkuu wa kanisa la mzaliwa wa kwanza utashuka chini kutoka mbinguni, na kuimiliki dunia, nao watakuwa na nafasi hadi mwisho utakapo kuja. Na hili ni agano langu lisilo na mwisho, ambalo nililifanya na baba yenu Henoko.
24 Na upinde utakuwa katika mawingu, nami nitalithibitisha agano langu kwenu, ambalo nililifanya kati yangu na ninyi, kwa ajili ya kila kiumbe kilicho hai cha wenye mwili wote ambao watakuwa juu ya dunia.
25 Na Mungu akamwambia Nuhu, Hii ni ishara ya agano ambayo nimeiweka kati yangu mimi na wewe; kwa ajili ya wenye mwili wote watakaokuwepo juu ya dunia.