Misaada ya Kujifunza
TJS, 2 Wathesalonike 2


TJS, 2 Wathesalonike 2:2–3, 7–9. Linganisha na 2 Wathesalonike 2:2–9

Shetani atasababisha kupotoka au ukengeufu kabla ya Bwana hajarudi.

2 Kwamba msifadhaishwe upesi akilini, au kusumbuliwa kwa andiko, isipokuwa mmelipokea kutoka kwetu; siyo kwa roho, wala kwa neno, kana kwamba siku ya Kristo i karibu.

3 Na mtu yeyote asiwadanganye kwa njia yoyote; maana utakuja ukengeufu kwanza, na akafunuliwa yule mtu wa dhambi; yule mwana wa upotevu;

7 Maana ile siri ya uovu hivi sasa inatenda kazi, na yeye ndiye atendaye kazi sasa, naye Kristo anamruhusu yeye kutenda kazi, hadi wakati utakapotimia ataondolewa nje ya njia.

8 Na hapo ndipo atakapofunuliwa yule mwovu, ambaye Bwana atammaliza kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa mngʼaro wa ujio wake.

9 Ndiyo, Bwana, hata Yesu, ambaye ujio wake hauji hadi baada ya kuja kwa ukengeufu, kwa kutenda kwake Shetani kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo,