Kiambatisho cha Tafsiri ya Joseph Smith UtanguliziZifuatazo ni sehemu zilizo chaguliwa za Tafsiri ya Joseph Smith ya Biblia ya Toleo la King James (TJS). Bwana alimwongoza Nabii Joseph Smith kuurejesha ukweli kwenye maandiko ya Biblia ya King James ambayo yalipotea au kubadilishwa tangu pale maneno ya kwanza yalipoandikwa. Ukweli huu uliorejeshwa ulifafanua mafundisho na kuboresha uelewa wa maandiko. TJS, Mwanzo Yaliyomo JST, Mwanzo 1–8Maandishi haya ya Biblia yalirejeshwa na Joseph Smith na yamechapishwa katika Lulu ya Thamani Kuu kama Uteuzi kutika Kitabu cha Musa. TJS, Mwanzo 9Baada ya gharika, Nuhu anamwomba Bwana kutoilaani dunia tena. TJS, Mwanzo 14Melkizedeki anambariki Abram. Huduma kuu ya Melkizedeki na nguvu na baraka za Ukuhani wa Melkizedeki zaelezwa. TJS, Mwanzo 15Ibrahimu anajifunza juu ya Ufufuko na anaona ono la huduma ya Yesu akiwa duniani. TJS, Mwanzo 17Watu washindwa kutii ibada za injili, ikijumuisha ubatizo. Mungu amwelezea Ibrahimu juu ya agano la tohara na umri wa uwajibikaji wa watoto. TJS, Mwanzo 19Lutu anajizuia na uovu wa Sodoma, na malaika wanamlinda. TJS, Mwanzo 21Ibrahimu humwabudu Mungu wa milele. TJS, Mwanzo 48Efraimu na Manase wanakuwa makabila ya Israeli. Kama vile Yusufu wa kale alivyoiokoa familia yake kimwili, uzao wake utaiokoa Israeli kiroho katika siku za mwisho. TJS, Mwanzo 50Yusufu akiwa Misri anatoa unabii wa Musa akikomboa Waisraeli toka katika utumwa wa Wamisri; juu ya tawi la uzao wa Yusufu likiongozwa hata nchi ya mbali, mahali ambako watakumbukwa katika maagano ya Bwana; juu ya Mungu kumwita nabii wa siku za mwisho aitwaye Joseph ili kuunganisha kumbukumbu ya Yuda naya Yusufu; na juu ya Haruni kutumikia kama msemaji wa Musa. TJS, Kutoka Yaliyomo TJS, Kutoka 4Bwana hahusiki na ugumu wa moyo wa Farao. Ona pia TJS, Kutoka 7:3, 13; 9:12; 10:1, 20, 27; 11:10; 14:4, 8, 17; kila rejeo, likitafsiriwa kwa usahihi, linaonyesha kwamba Farao alishupaza moyo wake yeye mwenyewe. TJS, Kutoka 18Yethro ni kuhani mkuu. TJS, Kutoka 22Wauaji hawataishi. TJS, Kutoka 32Bwana atawasemehe Waisraeli watakao tubu. TJS, Kutka 33Hakuna mtu mwenye dhambi anayeweza kuuona uso wa Mungu na akaishi. TJS, Kutoka 34Mungu anaandika tena juu ya mbao za mawe zilizotayarishwa na Musa lakini anaondoa Ukuhani wa Melkizedeki na ibada zake kutoka kwa wana wa Israeli. Anawapa sheria za amri za kimwili badala yake. TJS, Kumbukumbu la ToratiJuu ya seti ya kwanza ya mbao za mawe Mungu alifunua agano lisilo na mwisho la ukuhani mtakatifu. TJS, 1 SamweliPepo mchafu ambaye huja juu ya Sauli haji kutoka kwa Bwana. TJS, 2 SamweliDhambi ya kuhuzunisha ya Daudi haijaondolewa na Mungu. TJS, 1 Mambo ya NyakatiMungu anamzuia malaika asiangamize Yerusalemu. TJS, 2 Mambo ya NyakatiBwana hatii roho ya uongo vinywani mwa manabii. TJS, Zaburi Yaliyomo TJS, Zaburi 11Katika siku za mwisho wenye haki watakimbilia kwenye mlima wa Mungu. Wakati Bwana atakapokuja, atawaangamiza waovu na atawaokoa wenye haki. TJS, Zaburi 14Mtunga Zaburi anaona upotevu wa ukweli katika siku za mwisho na anatazamia kuanzishwa kwa Sayuni. TJS, Zaburi 24Mfalme wa Utukufu atawakomboa watu Wake wakati wa ujio Wake. TJS, Zaburi 109Tuwaombee maadui zetu. TJS, Isaya Yaliyomo TJS, Isaya 29Ujumbe ambao mwanzo ulihubiriwa Yerusalemu na manabii wa kale utahubiriwa siku za mwisho kutoka Kitabu cha Mormoni, kilichopatikana “kutoka ardhini.” TJS, Isaya 42Bwana anamtuma mtumishi Wake ili awafundishe wale ambao wamechagua kutoona au kusikia ukweli; wale wasikiao na kutii watafanywa kuwa wakamilifu. TJS, YeremiaBwana hatubu; watu hutubu. TJS, AmosiBwana hatubu; wanadamu hutubu. TJS, Mathayo Yaliyomo TJS, MathayoManabii walitabiri kwamba Bethlehemu patakuwa sehemu atakapozaliwa Masiha. TJS, Mathayo 4Yesu anangozwa na Roho Mtakatifu, siyo na Shetani. TJS, Mathayo 5Yeyote yule anayetii amri na kuwafundisha wengine kufanya vivyo hivyo ataokolewa. TJS, Mathayo 6Bwana hatuongozi sisi katika majaribu. TJS, Mathayo 7Msihukumu bila haki. TJS, Mathayo 9Yesu anakataa ubatizo wa Mafarisayo; kwani hauna thamani kwa sababu wao hawamkubali Yeye. Yeye ana tangaza kwamba Yeye ndiye ambaye aliyewapa sheria ya Musa. TJS, Mathayo 11Yohana Mbatizaji ni Eliasi ambaye atakuja kutayarisha njia kwa ajili ya Mwokozi. TJS, Mathayo 12Yeyote yule anayempinga Roho Mtakatifu hatasamehewa. TJS, Mathayo 13Kabla ya mwisho wa ulimwengu (maangamizo ya waovu), wajumbe waliotumwa toka mbinguni watawakusanya wenye haki kutoka miongoni mwa waovu. TJS, Mathayo 16Yesu anaelezea ina maana gani kusema mtu “kujichukulia msalaba wake”: ni kukataa maovu yote na kila tamaa ya dunia na kushika amri Zake. TJS, Mathayo 17Yesu anafundisha juu ya akina Elia wawili—mmoja kuandaa na mwingine kurejesha. TJS, Mathayo 18Watoto wadogo hawana haja ya toba. TJS, Mathayo 19Watoto wadogo wataokolewa. TJS, Mathayo 21Mwanadamu lazima atubu kabla ya kuamini katika Kristo. TJS, Mathayo 23Yeye aliye mbinguni ni muumba wetu. TJS, Mathayo 26Yesu kwanza anamega mkate wa sakramenti kisha anaubariki. Sakramenti ni ukumbusho wa mwili na damu ya Yesu. TJS, Mathayo 27Kifo cha Yuda chaelezwa. TJS, Marko Yaliyomo TJS, Marko 2Mwana wa Mtu ni Bwana wa Sabato kwa sababu aliifanya siku ya Sabato. TJS, Marko 3Yesu atawasamehe wenye dhambi wote wanaotubu isipokuwa wale wanaokufuru dhidi ya Roho Mtakatifu. TJS, Marko 7Yesu awalaani wale wanao wakataa manabii na hawatii sheria ya Musa. TJS, Marko 8Yeyote aliye tayari kufa kwa ajili ya Yesu atapokea wokovu. TJS, Marko 9Yohana Mbatizaji akiwa katika Mlima wa Kugeuka Sura. TJS, Marko 12Mungu siyo Mungu wa wafu, kwa sababu Yeye huwafufua wafu kutoka katika makaburi yao. TJS, Marko 14Yesu anaanzisha sakramenti kamaukumbusho wa mwili na damu Yake. TJS, Marko 16Malaika wawili wanawasalimu wale wanawake kwenye kaburi la Mwokozi. TJS, Luka Yaliyomo TJS, Luka 1Zakaria, baba wa Yohana Mbatizaji, anatekeleza wajibu wa ukuhani. TJS, Luka 2Wasomi katika hekalu wanamsikiliza Yesu na kumwuliza Yeye maswali. TJS, Luka 3Kristo atakuja kama unabii ulivyotolewaili kuleta wokovu kwa Israeli na kwa Wayunani, Katika utimilifu nyakati Yeye atakuja tena kuhukumu ulimwengu. TJS, Luka 6Yesu anafundisha kwamba ni bora kuvumilia mateso kuliko kupambana na adui. TJS, Luka 9Kupata utajiri wa kidunia hakustahili kuipoteza nafsi yako. TJS, Luka 11Utimilifu wa maandiko matakatifu ni ufunguo wa maarifa. TJS, Luka 12Yesu anaelezea kwamba kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu haitasamehewa. TJS, Luka 14Wale wanaomjua Musa na manabii wanamwamini Yesu. TJS, Luka 16Sheria na manabii humshuhudia Yesu. Mafarisayo wanatafuta kuangamiza ufalme. Yesu anaelezea mfano wa mtu tajiri na Lazaro. TJS, Luka 17Ufalme wa Mungu umekwisha kuja. TJS, Luka 18Kutumaini katika utajiri humzuia mtu kuingia katika ufalme wa Mungu. TJS, Luka 21Yesu anasema juu ya baadhi ya ishara za ujio Wake. TJS, Luka 23Yesu anawaombea msamaha askari wa Kirumi Wanaomsulubisha. TJS, Luka 24Wanawake wanawaona malaika wawili kwenye kaburi la Yesu. TJS, Yohana Yaliyomo TJS, Yohana 1Injili ya Yesu Kristo imekuwa ikihubiriwa kutoka mwanzo. Yohana Mbatizaji ndiye Elia mtayarisha njia kwa ajili ya Kristo, na Yesu Kristo ndiye Elia ambaye hurejesha mambo yote na kupitia yeye wokovu huja. TJS, Yohana 4Mafarisayo wanatamani kumuua Yesu. Yeye anafanya baadhi ya ubatizo, lakini wanafunzi wake wanafanya zaidi. TJS, Yohana 6Mapenzi ya Baba ni kwamba wote wampokee Yesu. Wale wafanyao mapenzi ya Yesu watainuliwa katika ufufuo wa wenye haki. TJS, Yohana 13Yesu anaosha miguu ya Mitume ili kutimiza sheria ya Wayahudi. TJS, Yohana 14Mfalme wa giza, au Shetani, ni wa ulimwengu huu. TJS, Matendo Yaliyomo TJS, Matendo 9Wale walio pamoja na Paulo wakati wa uongofu wake wanaona mwanga, lakini hawasikii sauti au kumwona Bwana. TJS, Matendo 22Jemadari akamfungua Paulo kamba alizofungwa. TJS, Warumi Yaliyomo TJS, Warumi 3Paulo anafundisha kwamba mtu hawezi kufanya uovu kusababisha mema. TJS, Warumi 4Watu wanaweza tu kuokolewa kwa neema ya Yesu Kristo, sio kwa kutenda yale yanayo husiana na kushika sharia ya Musa. TJS, Warumi 7Ni Kristo pekee aliye nauwezo wa kufanya mageuzi ya kudumu ya roho za wanadamu. TJS, Warumi 8Wale waishio kulingana na njia za mwili hawawezi kumpendeza Mungu. TJS, Warumi 13Wale wanaoheshimu mamlaka za serikali wanafanya heshima yao kubwa na iliyo kamilika zaidi kwa Mungu. TJS, 1 Wakorintho Yaliyomo TJS, 1 Wakorintho 7Paulo anafundisha kwamba ndoa ni jambo la kutamanika. Wale walioitwa kama wamisionari, hata hivyo, humtumikia Mungu vyema zaidi kama watabaki waseja wakati wa huduma yao. TJS, 1 Wakorintho 15Kuna madaraja matatu ya utukufu katika Ufufuko. TJS, 2 WakorinthoPaulo anawaonya Watakatifu wasiishi kwa jinsi ya mwili. TJS, WagalatiaMusa ndiye mpatanishi wa agano la kwanza, au sheria. Yesu Kristo ndiye mpatanishi wa agano jipya. TJS, WaefesoHasira isiyo ya haki ni dhambi. TJS, WakolosaiAmri za binadamu zinaweza kuwa na manufaa katika kufundisha mambo kama kujiheshimu, bali hazimheshimu Mungu wala kumwokoa binadamu. TJS, 1 WathesalonikeWale watu wenye haki walio hai wakati wa kuja kwa Bwana hawatakuwa na nafasi zaidi ya wafu wenye haki. TJS, 2 WathesalonikeShetani atasababisha kupotoka au ukengeufu kabla ya Bwana hajarudi. TJS, 1 Timotheo Yaliyomo TJS, 1 Timotheo 2Kristo ndiye Mwana Pekee na Mpatanishi. TJS, 1 Timotheo 3Kanisa limeanzishwa juu ya kanuni kuu kwamba Yesu alikuwa mwili wa kufa, alifundisha injili, na alirudi kwa Baba yake. Angalizo: ugumu wa kueleza mabadiliko katika mistari ifuatayo inasisitiza kwamba “nguzo na msingi la ukweli” ni Yesu Kristo. TJS, 1 Timotheo 6Wale ambao wana nuru ya hali ya kutokufa (injili) ikiishi ndani yao wanaweza kumwona Yesu. TJS, Waebrania Yaliyomo TJS, Waebrania 1Malaika ni roho wanaohudumu. TJS, Waebrania 4Wale wanao shupaza mioyo yao hawataokolewa; wale wanaotubu wataingia katika pumziko la Bwana. TJS, Waebrania 6Kanuni za mafundisho ya Kristo hutupeleka katika ukamilifu. TJS, Waebrania 7Melkizedeki alikuwa kuhani kwa mfano wa Mwana wa Mungu. Wale wote wapokeao ukuhani huu wanaweza kuwa kama Mwana wa Mungu. TJS, Waebrania 11Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo. TJS, Yakobo (Bib.) Yaliyomo TJS, Yakobo (Bib.) 1Mateso, siyo majaribu, husaidia kututakasa. TJS, Yakobo (Bib.) 2Waumini hawapaswi kumwona mtu mmoja kuwa ni bora kuliko mwingine. TJS, 1 Petro Yaliyomo TJS, 1 Petro 3Baadhi ya roho zilizokuwa kifungoni zilikuwa roho zisizo kuwa na haki katika siku za Nuhu. TJS, 1 Petro 4Injili inahubiriwa kwa wale waliokufa. TJS, 2 PetroKatika siku za mwisho, watu wengi watamkana Bwana Yesu Kristo. Wakati atakapokuja, majanga mengi ya asili yatatokea. Kama tutavumilia katika haki, tutapokea dunia mpya. TJS, 1 Yohana Yaliyomo TJS, 1 Yohana 2Kristo ni mtetezi wetu kwa Baba kama sisi tunatubu. TJS, 1 Yohana 3Yeyote anayezaliwa kwa Mungu haendelei katika dhambi. TJS, 1 Yohana 4Ni watu wanaomwamini Mungu ndiyo wanaoweza kumuona Yeye. TJS, Ufunuo Yaliyomo TJS, Ufunuo 1Yohana Mtume anapokeamafunuo yaliyomo katika kitabu cha ufunuo. Anatembelewa na Yesu Kristo na malaika. TJS, Ufunuo 2Waovu wanatupwa jehanamu. TJS, Ufunuo 5Watumishi Kumi na Wawili wa Mungu wametumwa kote duniani. TJS, Ufunuo 12Yohana anaelezea juu ya zile ishara za mwanamke, mtoto, fimbo ya chuma, joka na Mikaeli. Ile vita iliyoanza mbinguni inaendelea hapa duniani. Angalia mabadiliko ya mfuatano wa mistari katika TSJ. TJS, Ufunuo 19Mungu hutumia neno la Kristo ili kuyapiga mataifa.