Misaada ya Kujifunza
TJS, Kutoka 4


TJS, Kutoka 4:21. Linganisha na Kutoka 4:21; 7:3, 13; 9:12; 10:1, 20, 27; 11:10; 14:4, 8, 17; Kumbukumbu la Torati 2:30

Bwana hahusiki na ugumu wa moyo wa Farao. Ona pia TJS, Kutoka 7:3, 13; 9:12; 10:1, 20, 27; 11:10; 14:4, 8, 17; kila rejeo, likitafsiriwa kwa usahihi, linaonyesha kwamba Farao alishupaza moyo wake yeye mwenyewe.

21 Na Bwana akamwambia Musa, hapo utakaporudi Misri, angalia kwamba ukayafanye mbele ya Farao maajabu yale yote, niliyoyatia mkononi mwako, nami nitakufanikisha; lakini Farao atashupaza moyo wake, na hatawapa ruhusa watu waondoke.

TJS, Kutoka 4:24–27. Linganisha na Kutoka 4:24–27

Wakati Bwana anapotishia kumuua Musa kwa kutomtahiri mwana wake, Sipora anaokoa maisha yake kwa kuifanya ibada yeye mwenyewe. Musa anaungama dhambi yake.

24 Na ikawa kwamba, Bwana alimtokea alipokuwa njiani, karibu na nyumba ya wageni. Bwana alikuwa amemkasirikia Musa, na alitaka kumuua; kwani alikuwa haja mtahiri mwanawe.

25 Ndipo Sipora alipochukuwa jiwe lililochongoka na kumtahiri mwanae, na kulitupa jiwe miguuni pake, na akasema, Hakika wewe ni mume wa damu kwangu.

26 Na Bwana akamhurumia Musa na akamwacha aende, kwa sababu Sipora, mke wake, alimtahiri mtoto. Na alisema, wewe ni mume wa damu. Na Musa aliona aibu na akaficha uso wake kutoka kwa Bwana na kusema, nimetenda dhambi mbele za Bwana.

27 Na Bwana akamwambia Haruni, Nenda nyikani ukakutane na Musa, na alikwenda na akamkuta, juu ya mlima wa Mungu; juu ya mlima ambapo Mungu alimtokea; na Haruni alimbusu.