TJS, Mathayo 4:1, 5–6, 8–9. Linganisha na Mathayo 4:1, 5–6, 8–9; mabadiliko ya aina hiyo hiyo yamefanywa katika Luka 4:2, 5–11
Yesu anangozwa na Roho Mtakatifu, siyo na Shetani.
1 Kisha Yesu akaongozwa na Roho, kwenda nyikani, ili kuwa pamoja na Mungu.
5 Kisha Yesu akachukuliwa hadi mji mtakatifu, na Roho akamkalisha juu ya kinara cha hekalu.
6 Kisha ibilisi akamjia na kusema, Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini, kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake, na mikononi mwao watakuchukua, usije wakati wowote ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
8 Na tena, Yesu alikuwa katika Roho, naye akamchukua mpaka mlima mrefu mno, na akamwonyesha falme zote za ulimwengu na utukufu wake.
9 Naye ibilisi akamjia tena, na kusema, Haya yote nitakupa, ukianguka na kunisujudia.
TJS, Mathayo 4:11. Linganisha na Mathayo 4:11
Yesu anawatuma malaika kumhudumia Yohana Mbatizaji.
11 Na sasa Yesu alijua kwamba Yohana alikuwa ametupwa gerezani, naye akawatuma malaika, na, tazama, wakaja na wakamhudumia.
TJS, Mathayo 4:18. Linganisha na Mathayo 4:19
Manabii wa Agano la Kale wanena juu ya Yesu.
18 Naye akawaambia, Mimi ndiye ambaye imeandikwa na manabii; nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu.
TJS, Mathayo 4:22. Linganisha na Mathayo 4:23
Yesu anawaponya watu miongoni mwa wale waaminio katika jina Lake.
22 Naye Yesu alikwenda kote Galilaya akifundisha katika masinagogi yao, na kuhubiri injili ya ufalme; na kuponya kila aina ya maradhi, na magonjwa ya kila aina miongoni mwa watu ambao waliliamini jina lake.