TJS, Mathayo 21:33. Linganisha na Mathayo 21:32–33
Mwanadamu lazima atubu kabla ya kuamini katika Kristo.
33 Maana yule ambaye hakumwamini Yohana juu yangu, hawezi kuniamini mimi, isipokuwa ametubu kwanza.
TJS, Mathayo 21:47–56. Linganisha na Mathayo 21:45–46
Yesu anatamka kwamba yeye ndiye jiwe kuu la tao. Injili imetolewa kwanza kwa Wayahudi na baadaye kwa Wayunani. Waovu wataangamizwa wakati Yesu arudipo.
47 Na wakati makuhani wakuu na Mafarisayo waliposikia mifano yake, wakadhani kwamba alisema juu yao.
48 Nao wakasemezana wao kwa wao, Mtu huyu anafikiri ya kwamba yeye peke yake ataweza kuharibu ufalme huu mkubwa? Nao wakamkasirikia.
49 Lakini walipotafuta kumtia mikononi mwao, wakaogopa umati ule, kwa sababu walikuja kufahamu kwamba umati ulimchukulia yeye kuwa ni nabii.
50 Na sasa wanafunzi wake wakamjia, na Yesu akawaambia, Mwashangaa maneno ya mfano ule ambao niliwaambia?
51 Amini, ninawaambia, Mimi ndiye jiwe, na wale waovu wamenikataa.
52 Mimi ni jiwe kuu la pembeni. Wayahudi hawa wataanguka juu yangu nao watavunjika.
53 Na ufalme wa Mungu utaondolewa kutoka kwao, na utatolewa kwa taifa lizaalo matunda yake; (ikimaanisha Wayunani.)
54 Kwa hiyo, kwa yeyote ambaye jiwe hili litamwangukia, litamsaga hadi kuwa unga.
55 Na Bwana wa shamba la mizabibu ajapo, atawaangamiza watu wale wenye huzuni, waovu, na atalikodisha tena shamba lake la mizabibu kwa wakulima wengine, hata katika siku za mwisho, watakaompa matunda katika majira yao.
56 Na ndipo wakaelewa ule mfano ambao aliwaambia, kwamba Wayunani wataangamizwa pia, wakati Bwana ashukapo kutoka mbinguni ili kutawala katika shamba lake la mizabibu, ambalo ni dunia na wakazi wake.