Misaada ya Kujifunza
TJS, Mathayo 27


TJS, Mathayo 27:3–6. Linganisha Mathayo 27:3–5; Matendo 1:18

Kifo cha Yuda chaelezwa.

3 Basi Yuda, ambaye alimsaliti, alipoona kwamba anahukumiwa, akajuta mwenyewe, na akarudisha vipande vile thelathini vya fedha kwa wakuu wa makuhani na wazee,

4 Akisema, katika hilo nimetenda dhambi nimeisaliti damu isiyo na hatia.

5 Nao wakamwambia, Haya yatupasa nini sisi? Yaangalie haya wewe mwenyewe; dhambi zako na ziwe juu yako.

6 Akavitupa chini vile vipande vya fedha katika hekalu, na akaondoka, na akaenda, na akajinyonga juu ya mti. Na akaanguka chini, na matumbo yake yakapasuka, naye akafa.