TJS, Luka 16:16–23. Linganisha na Luka 16:16–18
Sheria na manabii humshuhudia Yesu. Mafarisayo wanatafuta kuangamiza ufalme. Yesu anaelezea mfano wa mtu tajiri na Lazaro.
16 Nao wakamwambia, Sisi tunayo sheria, na manabii; lakini juu ya mtu huyu sisi hatutampokea kuwa mtawala wetu; maana yeye ajifanya kuwa mwamuzi juu yetu.
17 Kisha Yesu akawaambia, Sheria na manabii hunishuhudia mimi; ndiyo, na manabii wote walioandika, hata hadi Yohana, wametabiri juu ya siku hizi.
18 Tangu wakati ule, ufalme wa Mungu unahubiriwa, na kila mtu atafutaye ukweli, hujiingiza ndani yake.
19 Na ni rahisi zaidi kwa mbingu na dunia kupita, kuliko kwa nukta moja ya sheria kutanguka.
20 Na kwa nini ninyi mnafundisha sheria, na kukana kile kilichoandikwa; na kumhukumu yeye ambaye Baba amempeleka ili kutimiza sheria, ili wote mpate kukombolewa?
21 Enyi, wajinga! maana mmesema mioyoni mwenu, Hakuna Mungu. Nanyi mnazipotoa njia za haki; na ufalme wa mbingu hupatikana kwa nguvu; nanyi mwawatesa wanyonge; na katika nguvu zenu mnatafuta kuuangamiza ufalme; na mnawatwaa watoto wa ufalme kwa nguvu. Ole wenu, ninyi wazinzi!
22 Nao wakamlaani tena, kwa sababu walikuwa wamekasirika kwa kuwaambia kwamba wao walikuwa wazinzi.
23 Lakini yeye aliendelea, akisema, Kila amwachaye mkewe, na kumwoa mke mwingine, azini; naye amwoaye yeye aliyeachwa na mumewe, azini. Amini ninawaambia, Nitawalinganisha na mtu tajiri.