Misaada ya Kujifunza
TJS, 1 Wakorintho 7


TJS, 1 Wakorintho 7:1–2, 5, 26, 29–33, 38. Linganisha na 1 Wakorintho 7:1–2, 5, 26, 29–38

Paulo anafundisha kwamba ndoa ni jambo la kutamanika. Wale walioitwa kama wamisionari, hata hivyo, humtumikia Mungu vyema zaidi kama watabaki waseja wakati wa huduma yao.

1 Sasa kulingana na mambo yale mliyoniandikia, mkisema, Ni vyema mwanamume asimguse mwanamke.

2 Hata hivyo, ninakuambieni, ili kuepuka uasherati, acha kila mwanamume awe na mke wake mwenyewe, na acha kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.

5 Msitengane, isipokuwa mmekubaliana kwa muda, ili mpate kujitoa wenyewe kwa kufunga na maombi; na kurudiana tena, ili Shetani asikujaribu tena kwa kutokuwa na kiasi kwenu.

26 Kwa hiyo naona hili kuwa ni jema kwa ajili ya shida iliyopo, kwa mtu kubaki hivyo ili apate kutenda mema zaidi.

29 Lakini nasema nanyi mlioitwa kwa huduma hii. Maana hii nasema, ndugu, muda ubakiao ni mfupi, kwamba mtapelekwa katika huduma. Hata wale walio na wake, watakuwa kama hawana; maana ninyi mmeitwa na kuchaguliwa kufanya kazi ya Bwana.

30 Na itakuwa kwao waliao, kama hawalii; na wale wafurahio, kama hawafurahi, na wale wanunuao, kama hawana kitu;

31 Na wale wautumiao ulimwengu huu, kama hawautumii; kwa maana ya mtindo wa ulimwengu huu yanapita.

32 Lakini ningetaka, ndugu zangu, kwamba utukuzeni wito wenu. Ningetaka msiwe na masumbufu. Maana yule asiyeoa, hujishughulisha na mambo yaliyo ya Bwana na jinsi gani anaweza kumpendeza Bwana; kwa hiyo yeye hushinda.

33 Lakini yeye aliyeoa, hujishughulisha na mambo ambayo ni ya ulimwengu huu, jinsi atakavyompendeza mke wake; kwa hiyo iko tofauti, maana yeye anazuiwa.

38 Basi kwa hiyo yule anayeoa anafanya vyema; bali yule asiyeoa anafanya vyema zaidi.