Mambo Haya Ninajua
Kwa yale yote nimesoma na kufundisha na kujifunza, moja ya thamani kubwa na ukweli mtakatifu ambao ninatoa ni ushuhuda wangu wa kipekee wa Mwokozi Yesu Kristo.
Mwaka 1992, baada ya kuhudumu miaka tisa kama Msaidizi wa Wale Kumi na Wawili na miaka 22 kama mshiriki wa Wale Kumi na Wawili, nilifika umri wa 68. Nilihisi hisia kuanza kile nilichokiita “Utunzi ambao Haukukamilika.” Sehemu ya kwanza ya kazi hiyo inaenda hivi:
Nilikuwa na wazo usiku uliopita
Wazo muhimu na la kina
Lilikuja wakati mimi nilikuwa nimechoka sana
Nikiwa nimechoka zaidi kwenda kulala
Nilikuwa nimekuwa na siku yenye kazi nyingi
Na nikatafakari juu ya hatma yangu
Wazo lilikuwa hili:
Nilipokuwa mdogo, Sikuwa miaka 68!
Ningetembea bila kuchopea;
Sikuwa na maumivu ya bega.
Ningeweza kusoma mstari kupitia mara mbili
Na kisha kuunukuu tena
Ningefanya kazi kwa masaa mengi
Na kamwe sikutua ili kupumua.
Na mambo ambayo kwa sasa siwezi kuyafanya
Niliyatawala kwa urahisi
Kama ningeweza sasa kurudisha miaka nyuma,
Kama hiyo ingekuwa yangu kuchagua
Singebadilisha uzee kwa ujana
Ningekuwa na mengi kupoteza
Hakika ninafuraha kusonga mbele,
Kuwacha ujana wangu, ingawa ni mkuu vipi
Vitu nigepotenza ningalirudi nyuma
Ndiyo ninaelewa.
Miaka kumi baadaye, niliamua kuongeza mistari michache zaidi kwenye shairi hilo:
Miaka kumi imepita sijui kuenda wapi.
Nazo kuna uchungu mwingi
Kiuno cha chuma kilifuta kuchokomea kwangu
Ninatembea wima tena
Chuma kingine kinashikilia mifupa ya shingo sawa--
Uumbaji mzuri!
Ilitupilia polio yangu mbali;
Nimejiunga na kizazi chenye shingo-ngumu.
Dalili za kuzeeka zinaweza kuonekana.
Mambo hayo hayatakuwa bora.
Kile kinachokuwa tu katika nguvu.
Nami ni msahaulizi wangu
Unauliza, “Je, ninakukumbuka?”
Bila shaka, wewe uko vile vile
Sasa usikasirike
Ikiwa siwezi kumbuka jina lako.
Nakubali nimejifunza mambo kadhaa.
Ambayo sikutaka kujua,
Lakini umri umeleta kweli hizo za thamani
Ambazo hufanya roho kunawiri.
Kwa baraka zote zilizokuja,
Kile bora zaidi katika maisha yangu.
Ni urafiki na faraja.
Ninaupata kutoka kwa mkeyangu mpendwa.
Watoto wetu wote wameoa vyema,
Wana familia zao wenyewe,
Wana watoto na wajukuu,
Jinsi gani kwa upesi wamekuwa.
Sijabadili mawazo yangu kamwe.
Kuhusu kurejesha ujana
Tunapaswa kuzeeka, kwa kuwa nao.
Huja ujuzi wa ukweli.
Unauliza, “ Je!Kesho italeta nini?”
Nini itakuwa hatma yangu?”
Nitaendelea mbele na sitalalamika.
Uliza nikiwa miaka 88!
Na mwaka jana niliongeza mistari hii:
Na sawa mnaona niko miaka 88.
Miaka imepita kwa kasi sana.
Nilitembea, nilichechea, nilishikilia fimbo,
Na sasa hatimaye ninaendesha.
Mimi husinzia mara kwa mara.
Lakini nguvu ya ukuhani inabaki.
Kwa vitu vyote vya kimwili ninavyokosa.
Kuna faida kubwa ya kiroho.
Nimeshasafiri duniani maili milioni.
Na milioni ingine tena
Na kwa usaidizi wa Setaliti,
Safari zangu hazijakamilika.
Sasa naweza nikasema kwa uhakika.
Kwamba namjua na kumpenda Bwana.
Naweza kushuhudia na wale wa kale.
Nikihubiri neno Lake tukatifu.
Ninajua kile alichohisi Gethsemane.
Ni kuu kufahamu
Najua alifanya yote kwa ajili yetu;
Hatuna rafiki mkubwa zaidi yake.
Najua kuwa Yeye atarudi tena.
Kwa nguvu na katika utukufu.
Najua nitamuona Yeye mara nyingine tena.
Katika hatima ya hadidhi ya maisha yangu.
Nitapiga magoti mbele ya miguu yake iliyojeruhiwa.
Nitahisi Roho Wake ukiangaza.
Sauti yangu yenye kunong’ona, kutetemeka itasema,
“Bwana wangu, Mungu wangu, Najua.”1
Na mimi ninajua!
Madirisha ya nyuma ya nyumba yetu yanaangalia bustani ndogo ya maua na miti ilio mpakani mwa mkondo mdogo. Ukuta mmoja ya nyumba unafikia mpaka wa bustani na umefunikwa kabisa na mwefeu wa Uingereza. Zaidi ya miaka mwefeu huu imekuwa mahali pa kukalia pa shorewanda wa nyumba. Viota katika mizabibu viko salama kutokana na mbweha na rakuni na paka ambao huwa hapa na pale.
Siku moja kulikuwa na vurugu kubwa katika mwefeu. Vilio vya hatari vilileta shorewanda 8 au 10 kutoka msitu jirani kujiunga katika kilio hiki cha kamsa. Punde niliona chanzo cha vurugu. Nyoka alikuwa ameteremka nje na kuning’inia mbele ya dirisha kwa muda ya kutosha tu kwangu mimi kumvuta nje. Sehemu ya katikati ya mwili wa nyoka ilikuwa na uvimbe mara mbili---ushahidi wa wazi kumhukumu kuwa alichukua vifaranga wawili kutoka kiotani. Hatukuwahi kuona jambo kama hili kwa muda wa miaka 50 tuliokuwa tumeishi katika nyumba yetu. Ilikuwa ni tukio la mara-moja-kwa-maisha---ama kwamba tulidhania hivyo.
Siku chache baadaye kulikuwa na vurugu ingine, wakati huu katika mizabibu inayofunika mkimbio wa mbwa wetu.Tulisikia kilio kile kile na kuona mkusanyiko huo huo wa majirani. Tulijua muaji alikuwa nani. Mjukuu alipanda kwenye mkimbio na kuvuta nyoka mwingine ambaye alikuwa bado ameshikilia kwa nguvu ndege yule mama ambaye alikuwa amemshika kwenye kiota na kumua.
Mimi nikajiuliza, “Ni nini kinachoendelea? Je, Bustani la Edeni linavamia tena?
Kukaja akilini mwangu maonyo yasemwayo na manabii. Hatukakuwa salama kutokana na ushawishi wa adui daima, hata ndani ya nyumba zetu wenyewe. Tunahitaji kulinda vifaranga vyetu.
Tunaishi katika ulimwengu hatari sana ambao unatishia yale mambo ambayo ni ya kiroho sana. Familia, shirika la msingi katika wakati na milele, iko chini ya mashambulizi kutoka kwa vikosi vya dhahiri na vya siri. Adui yu kazini. Lengo lake ni kusababisha majeraha. Kama anaweza kudhoofisha na kuharibu familia, atakuwa amefanikiwa.
Watakatifu wa Siku za Mwisho wanatambua umuhimu mkuu wa familia na hujitahidi kuishi katika njia kwamba adui hawezi kuiba katika nyumba zetu. Tunapata ulinzi na usalama kwa ajili yetu wenyewe na watoto wetu kwa kuheshimu maagano ambayo tumefanya na kuishi hadi matendo ya kawaida ya utiifu yanayostahili kwa wafuasi wa Kristo.
Isaya alisema, “Kazi ya haki itakuwa amani; na athari ya haki utulivu na matumaini milele.”2
Amani hiyo inaahidiwa pia katika funuo ambapo Bwana anasema, “ikiwa mko tayari hamtahofia.”3
Nguvu kamilifu ya Ukuhani imetolewa ili kulinda familia na wakaazi wake. Baba ana mamlaka na jukumu la kuwafundisha watoto wake na kubariki na kutoa kwa ajili yao idada za Injili na ulinzi wowote mwingine muhimu wa ukuhani. Anapaswa kuonyesha upendo na uaminifu na heshima kwa mama ili watoto wao waweze kuona upendo .
Nimekuja kujua kwamba imani ni nguvu halisi si tu kielelezo cha amaza. Kuna mambo machache yenye nguvu zaidi kuliko maombi ya uaminifu ya mama mwenye haki.
Jifunze na ufundishe familia yako kuhusu kipawa cha Roho Mtakatifu na Upatanisho wa Yesu Kristo. Hutafanya kazi kuu zaidi ya milele kuliko ndani ya kuta za nyumba yako mwenyewe.
Tunajua kwamba sisi ni watoto wa kiroho wa wazazi wa mbinguni, tuko hapa duniani ili kupokea miili yetu inayokufa na kujaribiwa. Sisi ambao tuna miili ya kidunia tuna nguvu juu ya viumbe ambavyo havina.4 Tuko huru kuchagua kile tunachotaka, na kuchukua na kuchagua vitendo vyetu, lakini hatuko huru kuchagua matokeo. Huja yanavyokuja.
Wakala umefafanuliwa katika maandiko kama “wakala wa kimaadili,” ambayo ina maana kwamba tunaweza kuchagua kati ya mema na mabaya. Adui anatafuta kutujaribu tutumie vibaya wakala wa maadili wetu.
Maandiko yanatufundisha “kwamba kila mtu anaweza kutenda kulingana na mafundisho na kanuni zihusuzo hali yake ya baadaye, kulingana na haki ya kujiamulia ambayo nimempa, ili kila mtu aweze kuwajibika kutokana na dhambi zake mwenyewe katika siku ya hukumu.”5
Alma alifundisha kwamba “Bwana hawezi kuangalia dhambi na kuikubali hata kidogo.”6 Ili kuelewa hili, ni lazima tutenge dhambi kutoka mwenye kutenda dhambi.
Kwa mfano, walipomleta mbele ya Mwokozi mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, ikiwa wazi kuwa alikuwa na hatia, Aliifuta kesi kwa maneno matano: “Nenda, na usitende dhambi tena.”7 Hiyo nidio roho ya huduma Wake.
Kuvumiliana ni fadhila, lakini, kama fadhila zingine zote, inapovumishwa sana hugeuka na kuwa uovu. Tunahitaji kuwa makini kwa ajili ya “mtego wa uvumilivu” ili kwamba tusiangamizwe nao. Uhuru unaopewa na kudhoofika kwa sheria za nchi kuvumilia vitendo vya usherati vilivyoruhusiwa kisheria haipunguzi madhara makubwa ya kiroho ambayo hutokana na ukiukaji wa sheria ya Mungu ya usafi wa kimwili.
Wote huzaliwa na Nuru ya Kristo, ushawishi elekezi ambayo humkubalisha kila mtu kutambua haki kutoka kwa makosa. Kile tunachofanya na nuru hii na jinsi tunajibu ushawishi huo kuishi kwa haki ni sehemu ya mtihani wa maisha duniani.
“Kwani tazama, Roho ya Kristo imetolewa kwa kila mtu, ili ajue mema na maovu; kwa hivyo, ninawaonyesha njia ya kuhukumu; kwani kila kitu kinachokaribisha kufanya mema, na kushawishi kuamini katika Kristo, kinasababishwa na uwezo wa thawabu ya Kristo kwa hivyo mngejua na ufahamu kamili kwamba ni cha Mungu.”8
Kila mmoja wetu lazima abaki katika hali ili kujibu msukumo na ushawishi wa Roho Mtakatifu. Bwana ana njia ya kumwaga maarifa masafi ndani ya akili zetu ili kutuchochea, kutuongoza, kutufundisha, na kutuonya. Kila mwana au binti wa Mungu anaweza kujua mambo wanayohitaji kujua mara moja. Jifunze kupokea na kufuata uongozi na ufunuo.
Kwa yale yote nimesoma na kufundisha na kujifunza, moja ya thamani kubwa na ukweli mtakatifu ambao ninatoa ni ushuhuda wangu wa kipekee wa Yesu Kristo. Yeye anaishi. Najua Yeye anaishi. Mimi ni shahidi Wake. Na juu Yake ninaweza kushuhudia. Yeye ni Mwokozi wetu, Mkombozi wetu. Kwa hili nina uhakika. Kwa hili ninashuhudia katika jina la Yesu Kristo, amina.