“Jane Elizabeth Manning James” Mada za Historia ya Kanisa
“Jane Elizabeth Manning James”
Jane Elizabeth Manning James
Jane Elizabeth Manning (circa 1822–1908) alikuwa angalau mmoja wa watoto watano waliozaliwa na wanandoa Waafrika Waamerika huru huko Connecticut nyakati ambazo watu weusi wengi katika Marekani walikuwa watumwa.1 Kama kijana mdogo, alijiunga na Jumuia ya Kanisa la Canaan mnamo 1841, lakini miezi 18 baadae, nyakati za baridi mnamo1842–43,yeye pamoja na wengi wa wanafamilia walibatizwa katika Kanisa la Yesu Kristo La Watakatifu wa Siku za Mwisho. Jane pamoja na wengine katika familia baadae walitamani kujiunga na Watakatifu huko Nauvoo, hivyo walisafiri kutoka Connecticut hadi New York, wakipanga kusafiri kwa vyote boti za kutumia mvuke na boti za kupita kwenye mifereji. Ingawa ,walikataliwa kusafiri kwenye boti sababu ya asili yao, kwahivyo walitembea maili 800 zilizobakia. Katika Peoria, Illinois, mamlaka za mji husika ziliwahoji akina Mannings kama wakimbizi watumwa na kudai maandishi kuthibitisha hali yao ya uhuru. Ubaguzi kilikuwa ni kikwazo ambacho Jane angekabiliana nacho maisha yake yote.
Akiwa Nauvoo, Jane kwa haraka alianzisha urafiki na Joseph na Emma Smith. Aliishi nao na alifanya kazi katika nyumba yao. Katika nyakati fulani, Emma alimualika Jane aweze kuasiliwa kama mtoto katika familia ya Smith kwa uunganishwaji kupitia ukuhani.2 Jane alikataa, kwa kutokuelewa tamaduni ngeni lakini kwa uimara aliamini katika wajibu wa kinabii wa Joseph. “Nilimjua Nabii Joseph,”baadae alishuhudia. “Alikuwa mwanaume mzuri sana niliyewahi kumwona duniani. … Nilikuwa na uhakika alikuwa nabii sababu nilijua hivyo.”3
Kupitia mazungumzo na Joseph na mama yake, Lucy Mack Smith, Jane alijifunza zaidi kuhusu Kitabu cha Mormoni na tafsiri yake na kupata uelewa wa na heshima kwa ibada za hekaluni.
Jane aliolewa na Isaack James, mwenye asili ya weusi aliyekuwa huru na mwongofu kutoka New Jersey. Wao, pamoja na Sylvester mtoto wa kiume wa Jane, waliondoka Nauvoo mwaka 1846 kuelekea magharibi pamoja na Watakatifu. Mnamo Juni mwaka huo, mtoto wa kiume wa Jane na Isaak Silas alizaliwa. Mwaka uliofuata familia ilipita nyanda, na kuwasili katika Bonde la Salt Lake katika majira ya majani kupukutika ya mwaka wa 1847. Isaac na Jane walikuwa na watoto sita zaidi, wawili tu kati yao waliishi zaidi ya Jane. Kama wakazi wa mwanzo wa Bonde la Salt Lake, Jane na Isaac walifanya kazi kwa bidii kukidhi mahitaji ya familia. Isaac alifanya kazi kama kibarua na mwalimu wa muda kwa Brigham Young, na Jane akisokota nyuzi, kushona nguo, na kufua nguo, kama alivyofanya Nauvoo.
Mgogoro wa kindoa ulisababisha Jane na Isaac kutalikiana katika mnamo mwaka 1870. Jane baadae alikuwa na ndoa ya muda mfupi ya miaka miwili na mtumwa wa zamani, Frank Perkins, ila baadae alirudia maisha kama mzazi pekee na bibi. Mahitaji ya kifedha na vifo vya watoto wake watatu vilimlazimisha Jane kurudi kufanya kazi. Alitengeneza na kuuza sabuni, wakati watoto wake wawili wa kiume walikodishwa kama vibarua. Mnamo1890, baada ya miaka 20 ya kuwa mbali, Isaac alirudi Salt Like Cicty, na kurudia upya uanachama wake wa Kanisa,na kufanya maridhiano ya mahusiano na Jane. Alipofariki mwaka mmoja baadae, mazishi yalifanyika nyumbani kwake.
Kipindi chote cha magumu ya maisha yake, Jane alibakia mwaminifu katika imani yake katika mafundisho ya injili na alithamini uanachama wake katika Kanisa. Alichangia ujenzi wa hekalu na kushiriki katika kubana matumizi ya Ushirika wa akina Mama na Mabinti Wadogo .4 Jane kwa wingi alipata uzoefu wa karama za Roho , ikiwa ni pamoja na maono, ndoto, kuponya kwa imani, na kuongea kwa lugha nyingi. Aliandika baadae katika maisha yake, “imani yangu katika Injili ya Yesu Kristo,” ni imara leo, laa, ni , kama inawezekana, imara kuliko ilivyokua siku nilipobatizwa mara ya kwanza.”5
Kati ya mwaka 1884 na 1904, Jane kwa nyakati tofauti aliwasiliana na viongozi wa Kanisa—John Taylor, Wilford Woodruff, Zina D. H. Young, na Joseph F. Smith—na kuomba ruhusa ya kupata endaumenti yake ya hekaluni na kuunganishwa.6 Wakati huo, Watakatifu wa siku za mwisho wenye asili ya weusi wanaume kwa wanawake walikuwa hawaruhusiwi kushiriki katika ibada nyingi za hekaruni. Mnamo 1888, raisi wa kata Angus M. Cannon alimuruhusu Jane kufanya ubatizo kwa niaba ya ndungu zake waliokufa.7 Viongozi wa Kanisa hatimae walimruhusu kuunganishwa kwa uwakilishi katika familia ya Joseph Smith kama mtumishi mnamo 1894, tukio la kipekee. Ingawa hakupokea endaumenti ya hekaluni au kuunganishwa na familia katika maisha yake, ibada hizi zilifanyika kwa niaba yake mnamo 1979.8
Alifariki Aprili 16, 1908, akiwa na umri wa miaka 95, mara zote akiwa Mtakatifu mwaminifu wa Siku za Mwisho. Habari za Deseret ziliarifu,“Watu wachache walitambulika zaidi kwa imani na uaminifu kuliko alivyokuwa Jane Mainning James, na ingawa wa unyenyekevu wa dunia alikuwa na marafiki wengi na wengi aliowafahamu kwa mamia.”9