Historia ya Kanisa
Joseph Smith na Ndoa za Mitala


“Joseph Smith na ndoa za Mitala,” Mada za Historia ya Kanisa

“Joseph Smith na Ndoa za Mitala”

Joseph Smith na Ndoa za Mitala

Watakatifu wa Siku za Mwisho wanaamini kwamba ndoa ya mke mmoja—ndoa ya mme mmoja na mwanamke mmoja—ndio sheria ya Bwana inayosimamia ndoa.1 Katika nyakati za biblia, Bwana aliamuru baadhi ya watu wake kuwa na ndoa za wake wengi—ndoa ya mme mmoja na wake zaidi mmoja.2 Baadhi ya waumini wa mwanzo wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho pia walipokea na kutii amri iliyotolewa kupitia manabii wa Mungu.

Baada ya kupokea ufunuo ukimuamru utekelezaji wa ndoa za wake wengi, Joseph Smith alioa wake wengi na alitambulisha utaratibu huu kwa washirika wake wa karibu. Kanuni hii likuwa mojawapo ya jambo lenye changamoto kubwa za Urejesho—kwa Joseph binafsi na kwa waumini wengine wa Kanisa. Ndoa ya wake wengi ilijaribu imani na kuchochea mkanganyiko na upinzani. Watakatifu wa Siku za Mwisho wachache mwanzo walikaribisha urejesho wa desturi za kibiblia kwa ujumla jambo lililokuwa geni geni kwao. Ila wengi baadae walishuhudia uzoefu wa nguvu za kiroho ulio wasaidia kushinda kusita kwao na kuwapa ujasiri kukubali desturi hii.

Taarifa nyingi juu ya desturi ya zamani kuhusu ndoa za mitala hazifahamiki sababu washiriki walitakiwa kutunza siri ya matendo yao. Taarifa za kihistoria kuhusu ndoa za zamani za mitala ni finyu: taarifa chache za wakati huo hutoa undani, na baadae mara nyingi maandishi ya wasomi sio ya kutegemea.. SAints inatoa historia muhimu kuhusiana na desturi ya ndoa za mitala na Joseph Smith na Watakatifu wengine wa Siku za Mwisho. Kwa taarifa za ziada kuhusiana na ndoa za wake wengi, ona“Plural Marriage in The Church of Jesus Christ of Latter-day Saints,” Gospel Topics Essays, topics.lds.org.

Related Topics: Joseph Smith Jr., Emma Hale Smith, Fanny Alger, Nauvoo Expositor

Chapisha