Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Juni 2010
Kurumbiza wenye rangi Kijivu kwenye Mabawa Yao
Karibu miaka sitini iliopita, wakati nilipokuwa nikihudumu kama askofu kijana, Kathleen McKee, mjane katika kata yangu, aliaga dunia. Miongoni mwa vitu vyake kulikuwa na kurumbiza wa kulea Wawili, walikuwa rangi jano halisi, walipeanwa kwa marafiki zake. Wa tatu, Billie, alikuwa na rangi kijivu ilioparara kwenye mabawa yake. Dada McKee alikuwa ameandika barua kwangu mimi: “Wewe na familia yako mtamtafutia nyumba huyu? Yeye sio mrembo, lakini nyimbo zake ni bora.”
Dada McKee alikuwa sana kama kurumbiza wake wa rangi njano mwenye rangi kijivu kwenye mabawa yake. Hakuwa amebarikwa na urembo, kipawa cha umbo, au kuheshimika kwa uzao. Hata hivyo nyimbo zake ziliwasaidia wengine kuwa upendeleo wa kubeba mzigo yao na kupata uwezo wa kubeba shida zao.
Ulimwengu umejaa kurumbiza wa rangi njano na rangi kijivu kwenye mabawa yao. Yakusikitisha ni kwamba ni wenye thamani wachache waliojifunza kuimba. Kati yao ni vijana ambao hawajui wao ni kina nani, kile wanachoweza kuwa, au hata wanachotaka kuwa; kile wanachotaka ni kuwa mtu tu. Wengine wamepinda migongo kwa uzee, mzigo ya taabu au wamejawa na shaka—wakiishi maisha ya kiwango cha chini ya uwezo wao.
Ili kuishi vyema, sharti tufanyinze uwezo wa kukabiliana na taabu kwa ujasiri, masikitiko kwa furaha, na ushindi kwa unyenyekevu. Unaweza kuuliza, “Je tunawezaje kuyafikia malengo haya?” Nami najibu, “Kwa kupata mwelekeo wa kweli wa kuwa sisi ni kina nani!” Sisi ni wana na mabinti wa Mungu aliye hai, katika umbo lake sisi tumeumbwa. Tafakari juu ya hayo: kuumbwa katika umbo la Mungu. Hatuwezi kwa kweli kushikilia uthibitisho huu bila ya kupata mhemko mpya wa nguvu na uwezo.
Katika ulimwengu wetu, hulka ya maadili sana sana hutelekezwa kuwa kitu cha pili baada ya urembo au haiba. Lakini kutoka zamani sana ushauri wa Bwana kwa nabii Samweli unarudia: “Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo” (1 Samweli 16:7).
Wakati Mwokozi alipokuwa akitafuta mtu wa imani, Hakumchagua kutoka kwa umati wa watu wenye kujidai wema, waliopatikana kila mara kwenye sinagogi. Hakika, alimwita kutoka miongoni mwa wavuvi wa Kapernaumu. Simioni aliye na shaka, asiye na elimu, mwenye haraka akawa Petro, Mtume wa imani. Kurumbiza wa njano mwenye rangi kijivu kwenye mabawa yake alihitimu katika imani kuu na upendo wa kudumu wa Bwana
Wakati Mwokozi alichagua mmisionari wa ari na nguvu, hakumpata miongoni mwa watetezi wake bali kati ya washindani Wake. Saulo mtesaji akawa Paulo mhamasishaji.
Mkombozi aliwachagua watu wasio kamili kufundisha njia ya ukamilifu Alifanya hivyo wakati huo. Anafanya hivyo sasa—hata kurumbiza wa njano wenye rangi kijivu kwenye mabawa yao. Anakuita wewe na mimi kumhudumia Yeye hapa chini. Msimamo wetu sharti uwe kamili. Na katika mapambano yetu, tutakapojikwaa, acha tusihi: “Tuongoze sisi, ewe tuongoze sisi, Mfinyazi mkuu wa watu.”1
Ombi langu ni kwamba tutafuata mfano wa Mtu wa Galilaya, ambaye angepatikana akichanganyikana na maskini, waliodhalilishwa, waliodhulumiwa, na walioteseka. Na wimbo wa kweli uje kutoka mioyoni mwetu tunapofanya hivyo.
© 2010 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa Imechapishwa USA Kiingereza kiliidhinishwa: 6/09. Tafsiri iliidhinishwa: 6/09. Tafsiri ya First Presidency Message, June 2010. Swahili. 09366 743