Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Juni 2010
Kufanya upya Maagano kupitia Sakramenti
Funza maandiko na dondoo hizi, au, ikihitajika, kanuni nyingine ambayo itabariki akina dada unaowatembelea. Toa ushuhuda wa fundisho hili. Alika wale unaowafundisha kushirikisha walichohisi na kujifundisha.
Yesu Kristo Alianzisha Sakramenti
“Yesu alichukua mkate, akaubariki na akaumega na kuwapa Mitume wake, akasema “Twaeni, mle’ (Mathayo 26:26). ‘Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu: fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu’ (Luka 22:19). Katika njia hiyo hiyo akatwaa kikombe cha kileo, kwa desturi kilikuwa kimezimuliwa kwa maji, akasema baraka za shukrani juu yake, na kukipeana kwa wale waliokuwa wamekusanyika karibu naye: ‘Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu,’ ‘inayomwagika … kwa ondoleo la dhambi.’ ‘Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.’ …
Tangu zoezi hilo la chumba cha juu mkesha wa Gethesemane na Golgotha, watoto wa ahadi wamekuwa chini ya agano la kukumbuka toleo la Kristo katika hii njia upya, ya juu, tukufu na ya kibinafsi.”1
Mzee Jeffrey R. Holland wa Jamii ya wale Mitume Kumi na Wawili.
Tunafanya upya Maagano Yetu ya Ubatizo kupitia Sakramenti
“Tunapobatizwa, tunajichukulia juu yetu wenyewe jina takatifu la Yesu Kristo. Kujichukulia juu yetu jina Lake ni mojawapo wa uzoefu muhimu tuliyonao katika maisha. …
Kila wiki katika mkutano wa sakramenti tunafanya ahadi ya kukumbuka toleo la upatanisho la Mwokozi wetu jinsi tunavyofanya upya agano letu la ubatizo. Tunaahidi kufanya kama vile Mwokozi alivyofanya kuwa watiifu kwa Baba na daima kuziweka amri zake. Baraka tunazopokea kama matokeo yake ni kuwa na Roho wake daima kuwa nasi”2
Mzee Robert D. Hales wa Jamii ya wale Mitume Kumi na Wawili.
“Nilikuwa na msichana wa umri wa miaka minane katika siku ya ubatizo wake. Mwishoni wa siku hiyo alisema kwa imani kuu, “Nimebatizwa kwa siku nzima, na sijatenda dhambi hata mara moja!’Lakini siku yake kamilifu haikuendea milele, na nina hakika anajifunza hata sasa, kama vile sisi tunavyojifunza, kwamba hata kama tukijaribu kwa nguvu sana, hatuwezi kuepuka kila tukio mbaya, kila chaguo mbaya. …
“… Haiwezekani kufanya mabadiliko yote halisi sisi wenyewe. Dhamira zetu wenyewe na utashi mwema wetu hautoshi. Tunapofanya makosa au uchaguzi mbaya, lazima tunahitaji msaada wa Mwokozi wetu ili kurudi njiani. Tunapokea sakramenti wiki baada ya wiki kuonyesha imani yetu kwa uwezo Wake wa kutubadilisha. Tunakiri dhambi zetu na kuahidi kuziacha kabisa.”3
Julie B. Beck, Rais mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama.
© 2010 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa Imechapishwa USA Kiingereza kiliidhinishwa: 6/09. Tafsiri iliidhinishwa: 6/09. Tafsiri ya Visiting Teaching Message, June 2010. Swahili. 09366 743