Vijana
Mtu Mgeni
Nilikuwa na wakati mgumu kuhisi kama nimeingiana. Familia yangu majuzi ilihamia mbali nchini. Kata tuliyoingia ilikuwa na kundi kubwa la vijana, lakini hii ilikuwa ni mara ya kwanza ningekuwa “mtu mgeni” Sehemu mbaya zaidi ilikuwa ni kwamba ilibidi niende kwa shule mpya, na wazo likaingia mara moja akilini mwangu, “Ninani ambaye nitaketi pamoja naye wakati wa chakula cha mchana?” Pengine nitaona mtu kutoka kanisani, lakini sikutaka kujiingiza kwenye meza ya chakula cha mchana ya mtu mwingine, haswa vile sikujua hata kama watanitaka pale!
Siku ya kwanza shuleni ilionekana kujivuta milele. Hatimaye kengele ya chakula cha mchana ikalia. Nilivyokuwa nikiingia kwenye chumba cha chakula cha mchana, Niliomba kwa Baba wa Mbinguni ili kunisaidia kupata mtu ninayemjua. Niliangalia kwote ili kuona ikiwa ningetambua mtu yeyote. Hakuna mmoja. Basi nilielekea kwenye meza upande wa kando wa chumba cha chakula cha mchana na kula chakula changu.
Baadaye siku hiyo wakati wa darasa la hesabu, Niliona sura nilioifahamu. Nilikuwa nimemuona David kwenye seminari asubuhi hiyo. Aliuliza ili kuona ratiba yangu na aligundua kwamba sote tulikuwa na wakati moja wa chakula cha mchana. “Ala, ulikuwa wapi wakati wa chakula cha mchana leo?” alisema.
“Nilikula upande ule mwingine wa chumba.” Nilijibu.
“Vyema, kesho njoo na ukae pamoja nami wakati wa chakula cha mchana,” alisema.
Nashukuru kwa Baba wa Mbinguni mwenye upendo, anayejua mahitaji ya kila mmoja wetu na anajibu kila maombi yetu. Nashukuru pia kwa mtu aliyekubali kunyoosha mkono wa urafiki. Kitu rahisi kama mwaliko kinaweza kuleta mabadiliko yote.