Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Julai 2010
Kuimarisha Familia na Nyumba
Soma kifaa hiki, na kama ifaavyo, ukijadili pamoja na kina dada unaowatembelea. Tumia maswali ili kukusaidia kuimarisha akina dada zako na kuufanya Muungano wa Usaidizi wa kina Mama kuwa sehemu hai ya maisha yako.
Kutoka kwenye Maandiko: Mwanzo18:19; Mosia 4:15; M&M 93:40; Musa 6:55–58
Kuimarisha katika Kila Nafasi
“Kila mmoja wetu yuko katika hali tofauti ya kifamilia. Familia zingine zina mama na baba pamoja na watoto nyumbani. Wenzi wengine kwa sasa hawana watoto nyumbani. Washiriki wengi wa Kanisa hawana wenzi, na wengine ni wazazi wasio na wenzi. Wengine ni wajane wanawake au wajane wanaume wanaoishi pekee yao.
“Haijalishi jinsi familia zetu zilivyo, kila mmoja wetu anaweza kufanya kazi ili kuimarisha familia zetu au kusaidia katika kuimarisha zingine.
“[Wakati mmoja] Nilikaa katika nyumba ya mpwa wangu na familia yake. Jioni hiyo kabla ya watoto kuelekea kitandani, tulikuwa na mkutano mfupi wa jioni wa familia na hadithi ya maandiko. Baba yao alielezea kuhusu familia ya Lehi na jinsi alivyowafundisha watoto wake kwamba ni lazima washikilie imara fimbo ya chuma, ambayo ni neno la Mungu. Kushikilia imara fimbo ya chuma kungewaweka salama na kuwaongoza kwenye shangwe na furaha. Ikiwa wataachilia fimbo ya chuma, kuna hatari ya kuangamia katika mto wa maji chafu.
“Ili kuonyesha haya kwa watoto, mama yao alikuwa ‘fimbo ya chuma’ ambayo ni lazima washikilie, na baba yao aliwakilisha nafasi ya shetani, akijaribu kuvuta watoto kutoka kwa usalama na furaha. Watoto walipenda hadithi na kujifunza jinsi ni muhimu kushikilia imara fimbo ya chuma. Baada ya hadithi ya maandiko ilikuwa ni wakati wa maombi ya familia. …
“Maandiko, mkutano wa Jioni wa familia nyumbani, na maombi ya familia yataimarisha familia. Tunahitaji kuchukua kila nafasi ili kuimarisha familia na kusaidiana mmoja kwa mwingine ili kukaa kwenye njia sahihi.”1
Barbara Thompson, mshauri wa pili katika urais mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa kina Mama.
Tunaweza Kufanya Nini?
-
Ni mawazo yapi ya kuimarisha familia na nyumba ambayo utashirikisha pamoja na kina dada zako? Unavyowaza juu ya hali zao za kibinafsi, Roho anaweza kuleta mawazo akilini mwako.
-
Ni mambo gani muhimu ambayo unaweza kubadilisha mwezi huu ili kuimarisha vyema familia na nyumba yako?
Kutoka kwa Historia yetu
Tangu mwanzo Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kumekuwa na maagizo ya kuimarisha familia na nyumba. Nabii Joseph alifundisha kina dada kwenye mkutano wa awali wa Muungano wa Usaidizi wa kina Mama, “Ukienda nyumbani, usiwahi kupeana neno la kukasirisha au baya kwa waume wenu, lakini acha ukarimu, hisani na upendo utawale kazi zako siku zote za usoni.”2
Mnamo 1914 Rais Joseph F. Smith aliwaambia kina dada wa Muungano wa Usaidizi wa kina mama, “Panapokuwa na ujinga au pengine ukosefu wa ujuzi kuhusiana na familia, … hapo muungano huu upo au ipo karibu mno, na kupitia kwa baraka asili na maongozi ya shirika wamejitayarisha na tayari kupeana maelekezo kwa marejeo kwa majukumu hayo muhimu.”3
© 2010 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Imechapishwa USA. Kiingereza kiliidhinishwa: 6/09. Tafsiri iliidhinishwa: 6/09. Tafsiri ya Visiting Teaching Message, July 2010. Swahili. 09367 743