2010
Baraka za Hekaluni
Agosti 2010


Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Agosti 2010

Baraka za Hekaluni

Bado naweza kukumbuka wakati wazazi wangu walipeleka famila yetu katika hekalu la Swiss lililokuwa limejengwa karibuni, la kwanza katika Uropa, kuwa familia ya milele. Nilikuwa umri wa miaka 16 na mdogo kati ya watoto wanne. Tulipiga magoti pamoja kwenye altari kufunganishwa hapa ulimwenguni kwa nguvu za ukuhani, kwa ahadi ya ajabu kwamba tunaweza kufunganishwa milele. Sitasahau kamwe tukio hili kuu.

Kama kijana nilivutiwa kwamba tulivuka mipaka ya mataifa kufunganishwa kama familia. Kwangu inaonyesha jinsi kazi ya hekaluni inavuka mipaka ya kiulimwengu kuleta baraka za milele kwa wakazi wote wa duniani. Mahekalu ya Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho kwa kweli yamejengwa kwa manufaa ya ulimwengu wote, bila kujali uraia, tamaduni, au mrengo wa siasa.

Mahekalu ni ushahidi imara kwamba wema utashinda. Rais George Q. Cannon (1827–1901), Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza, wakati mmoja alisema, “Kila jiwe la msingi ambalo limewekwa kwenye Hekalu, na kila Hekalu lililomalizika … linapunguza uwezo wa Shetani hapa duniani, na kuongeza uwezo wa Mungu na Uungu.”1

Hali kila hekalu linaongeza ushawishi wa wema katika dunia, baraka kuu, kwa kweli, uwajia hasa wale wanaoshirki hekaluni. Hapo tunapokea nuru zaidi na elimu na kufanya maagano matakatifu ambayo, kama yatafuatiwa, yatatusaidia kutembea katika njia ya ufuasi. Kwa ufupi, hekalu utufunza sisi juu ya madhumuni matakatifu ya maisha na kutusaidia kupata rahamani ya kweli ya kimwili na kiroho.

Hatushiriki hekaluni kwa niaba yetu tu, hata hivyo. Kila wakati tunaingia katika haya majumba matakatifu, tunachukua nafasi katika kazi takatifu, ya ukombozi wa wokovu uliotolewa kwa watoto wote wa Mungu kama matokeo ya Upatanisho wa Mzaliwa wa Pekee wa Baba. Hii ni huduma ya kujitolea na takatifu na ambayo inatuwezesha sisi kama watu kushiriki katika kazi tukufu ya kuwa kama waokozi kwenye Mlima Sayuni.

Kwa wale ambao hawawezi kushiriki hekaluni sasa kwa sababu yoyote ile, nawahimiza mfanye kila kitu katika nguvu zenu muwe na kibali cha hekalu cha sasa. Kibali cha hekalu ni ishara ya uaminifu na jitihada zetu za kutumikia Bwana. In ishara ya upendo wetu kwa Bwana, kama vile Yesu alivyofundisha, “Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu, nami nitampenda na kujidhirihisha kwake” (Yohana 14:21).

Kama vile Maandhari ya ulimwengu yanavyoendelea kurembeshwa ni haya majengo matakatifu yaliowekwa wakfu kwa Bwana, ni maombi yangu kwamba tutatimiza wajibu wetu katika kuleta mbingu karibu na dunia kwa kustahiki kwa kuwa na kibali cha hekaluni na kukitumia. Tunapofanya hivyo, wema kwa kweli utaongezeka sio tu kwa maisha yetu na nyumba zetu bali katika jamii na ulimwenguni kote.

Muhtasari

  1. George Q. Cannon, in “The Logan Temple,” Millennial Star, Nov. 12, 1877, 743.

Kufundisha kutoka kwa Ujumbe Huu

Watu wengi hujifunza vyema na kukumbuka muda mrefu wakati unapofunza mambo kwa kutumia vyombo vya picha badala ya kuongea tu (ona Teaching, No Greater Call [1999], 182). Wakati wa somo hili, fikiria kuonyesha picha ya hekalu. Baada ya kusoma makala haya, zungumzia kwa nini hekalu ni muhimu kwa Rais Uchtdorf. Waalike watoto wadogo katika familia kuchora picha ya familia yao katika hekalu.

Teaching, No Greater Call insema, “Wahimize wale unaowafunza kuweka lengo moja ua mengi ambayo yanaweza kuwasaidia kuishi kanuni ambazo umefunza” (159) Fikiria kusoma ujumbe wa Rais Uchtdorf pamoja na familia na kuwaalika wanafamilia kuandika lengo lao la kibinafsi ambalo litawasaidia kuwa wastahiki na kuwa na kutumia kibali cha hekalu.