2010
Njia Yako kuelekea Hekaluni
Oktoba 2010


“Njia Yako kuelekea Hekaluni,” Liahona, Okt 2010, 72–75

Kwa Ajili ya Watoto

Njia Yako kuelekea Hekaluni

Je, unajua ni hekalu lipi lipo karibu nawe? Chora picha ya hekalu hilo, na ining’inize mahali utakapoiona kila siku.

Hekalu ni nyumba ya Bwana. Ni mahali ambapo tunajifunza kuhusu Baba wa Mbinguni, kufanya maagano (au ahadi) na Yeye, na kupokea baraka kuu. Ndani ya hekalu tunafanya kazi muhimu kwa ajili yetu na kwa ajili ya wanafamilia ambao wamefariki. Kazi inayofanywa hekaluni inahusisha ubatizo kwa ajili ya wafu, endaomenti, na kuunganisha. Hizi zinaitwa ibada za hekaluni.

Kinachofanyika ndani ya Hekalu

Ubatizo kwa ajili ya Wafu

Ukiwa na umri wa miaka nane, unaweza kubatizwa na kuthibitishwa kuwa muumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Wengi wa mababu zako wamefariki bila kubatizwa na kuthibitishwa. Ingawa miili yao imekufa, roho zao zingali hai katika ulimwengu wa roho, mahali ambapo zinaweza kufunzwa injili ya Yesu Kristo.

Ukiwa na umri wa miaka 12, unaweza kwenda hekaluni na kuwasaidia watu hawa kwa kubatizwa na kuthibitishwa katika jina lao. Kisha wataweza kuchagua kama wanakubaliana na ubatizo na uthibitisho ama la. Utavalia mavazi meupe yote wakati unapobatizwa kwa ajili ya wafu, kama vile unavyofanya unapobatizwa kwa ajili yako mwenyewe.

Waombe wazazi wako wakusaidie kutengeneza orodha ya wanafamilia ambao wamefariki bila kubatizwa katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Chunguza kama kuna yeyote aliyewahi kwenda hekaluni ili kubatizwa kwa ajili yao.

Endaomenti

Moja ya baraka kubwa za hekalu ni endaomenti. Endaomenti inamaanisha “zawadi.” Unapopokea endaomenti yako, utajifunza zaidi kuhusu mpango wa wokovu na kufanya maagano. Maagano ni ahadi tunazoweka na Baba wa Mbinguni. Unapotunza maagano hayo, unajiandaa kuishi na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo siku moja.

Ndani ya hekalu kuna chumba kizuri, chenye amani kinachoitwa chumba cha selestia. Katika chumba cha selestia tunajihisi tu karibu na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo, na tunahisi kidogo jinsi itakavyokuwa kuishi Nao katika ufalme wa selestia.

Kuunganisha kwa Muda na Milele

Wakati mwanamume na mwanamke wanapofunga ndoa hekaluni, wanapiga magoti kwenye madhabahu na wanaunganishwa kwa muda na milele yote. Hii inamaanisha kwamba wao na watoto wao wanaweza kuunganishwa pamoja kama familia ya milele. Panga kufunga ndoa hekaluni siku moja. Hii ndio baraka kubwa sana ya hekaluni.

Kibali Cha Hekaluni

Hekalu ni mahali patakatifu. Maaskofu na marais wa tawi wanahakikisha kwamba wale wanaoingia hekaluni wamejiandaa na wanastahili. Kabla hujaenda hekaluni, utakuwa na mahojiano maalum na askofu wako au rais wa tawi. Atakuuliza kama una ushuhuda wa Kanisa, unashika amri, unawaunga mkono viongozi wa kanisa, unatii Neno la Hekima, unalipa Zaka, na u mwaminifu kwa yote unayofanya na kusema. Atakusaidia kujua nini cha kufanya ili kustahili kuingia hekaluni.

Jiandae Sasa Kuingia Hekaluni

Baba wa mbinguni hutoa baraka nyingi kwa wale wanaoishi kwa haki na kuhudhuria hekaluni. Ni muhimu kujiandaa kuingia hekaluni ukiwa bado mdogo.

Baba wa mbinguni anakupenda na anataka upokee baraka za hekaluni. Atakubariki kwa kufanya ibada za hekaluni kwa ajili yako na kwa ajili ya wengine. Ingawa huwezi kuingia ndani ya hekalu kwa sasa, kama kuna hekalu karibu, unaweza kutembelea maeneo ya nje ya hekalu na kuhisi roho aliyeko hapo. Pia unaweza kuweka picha ya hekalu nyumbani mwako ili kukukumbusha jinsi hekalu ni la muhimu. Ishi kwa haki ili ustahili kuingia kwenye nyumba ya Bwana.

Angalia kwenye kioo katika hii picha. Baadhi ya vyumba vya kuunganishia vina vioo kama hivi. Kwa sababu ya kuunganishwa katika hekalu, familia zetu, kama vile kuakisi katika hiki kioo, zinaweza kuendelea milele.

Angalia chumba cha selestia katika picha hili na katika picha iliyopo ukurasa wa 64. Unahisi vipi unapoona chumba cha selestia?

Hekalu la Boston Massachusetts. Liliwekwa wakfu Okt. 1, 2000.

Chumba cha kuunganishia, Hekalu la Aba Nigeria.

Chumba cha kuunganishia, Hekalu la Nuku’alofa Tonga.

Chapisha