2010
Je, Tunaweza Kumuona Kristo?
Desemba 2010


Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Desemba 2010

Je, Tunaweza Kumuona Kristo?

Jioni moja babu alikuwa anamsomea hadithi binti mjukuu wake wa miaka minne wakati aliangalia juu na kusema, “Babu, tazama nyota!” Huyu mzee alitabasamu kwa ukarimu na kusema, “Tu ndani ya nyumba, mpenzi. Hamna nyota hapa.” Lakini huyu mtoto akasisitiza, “Una nyota katika chumba chako! Tazama!”

Babu akatazama juu na, kwa kustajabu kwake, aligundua kwamba dari lilikuwa limerebeshwa kwa chembe za chuma za mng’aro. Zilikuwa hazionekani wakati wote, lakini zilipopigwa na mwanga kwa njia fulani, hakika zilionekana kama mkusanyiko wa nyota. Ilichukua macho ya mtoto kuziona, lakini zilikuwa papo. Na kutoka wakati huo na kuendelea, wakati babu alipoingia chumbani mwake na kutazama juu, aliweza kuona kile ambacho hakuweza kuona hapo awali.

Tunaingia katika kipindi kingine cha ajabu cha Krismasi kilichojawa na muziki na mng’aro, sherehe na zawadi. Lakini kati ya watu wote, sisi kama washiriki wa kanisa ambao tunaobeba jina la Mwokozi tunahitaji kuona mbele ya mambo ya kipindi na kuona ukweli adhimu na urembo wa wakati huu wa mwaka.

Sielewi ni wangapi katika Bethlehemu waliojua kuwa papo hapo, karibu nao, Mwokozi alikuwa amezaliwa? Mwana wa Mungu, Masiya aliyetarajiwa na kuahidiwa—Alikuwa miongoni mwao!

Je! Unakumbuka kile malaika alichowambia wachungaji? “Maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana.” Na walisemezana wenyewe, “Haya, na twendeni mpaka Bethlehemu, tukalione hilo lililofanyika” (Luka 2:11, 15).

Kama wachungaji wa kale, tunahitaji kusema katika mioyo yetu. “Haya tulione hilo lililofanyika.” Tunahitaji kulitamani ndani ya mioyo yetu. Haya tumuone Mtukufu wa Israeli katika hori, katika hekalu, juu ya mlima, na juu ya msalaba. Kama wachungaji, acha tutukuza na kusifu Mungu kwa hizi habari njema za furaha kuu!

Wakati mwingine vitu vilivyo vigumu sana kuviona ni vile vilivyo mbele zetu siku zote. Kama vile babu ambaye aliyekosa kuona nyota kwenye dari lake, mara nyingine tunakosa kuona kile ambacho ni wazi.

Sisi ambao tumesikia ujumbe mtukufu wa ujio wa Mwana wa Mungu, sisi ambao tumechukua juu yetu jina Lake na kuweka maagano ya kutembea katika njia Yake kama wafuasi Wake—sharti tusikose kufungua mioyo yetu na akili zetu na kumuona Yeye kikweli.

Kipindi cha Krismasi ni cha ajabu kwa njia nyingi. Ni kipindi cha matendo ya hisani ya ukarimu na upendo wa kindugu. Ni kipindi cha kuwa zaidi tukiakisi juu ya maisha yetu wenyewe na juu ya baraka nyingi ambazo zilizo zetu. Ni kipindi cha kusamehe na kusamehewa. Ni kipindi cha kufurahia muziki na mng’aro, sherehe na zawadi. Lakini mmeremeto wa kipindi haufai kamwe kufifisha mtazamo wetu na kutuzuia sisi kumuona kikweli Mfalme wa Amani na utukufu Wake.

Acha sote tufanye kipindi cha Krimasi ya Mwaka huu wakati wa kufurahia na kusherekea, wakati ambapo tutatambua muujiza kwamba Mwenyezi Mungu alimtuma Mwanawe Mzaliwa wa Pekee, Yesu Kristo, kukomboa ulimwengu!

Mawazo ya kufundisha kutoka kwa Ujumbe huu

  1. “Vitendo vya kuvutia vinaweza kutumika ili kulea mvuto na kusaidia wanaojifunza kulenga usikivu wao kwenye maudhui ya somo. … Picha ni vyombo vya thamani vya kuimarisha wazo muhimu la somo na kusaidia wanaojifunza kubakia wasikilivu” Teaching, No Greater Call [1999],160, 176). Unapoanza kushirkisha ujumbe huu, fikiria juu ya kutumia vitendo vya usikilivu kama vile kuonyesha picha au kushirikisha maandiko na kuuliza familia kufikiria jinsi inavyohusu huu ujumbe.

  2. “Mojawapo wa malengo yako muhimu yanafaa kuwa ni kuwasaidia wengine kutumia kanuni za injili katika hali za kila siku. … Wasaidie wanaojifunza kutambua baraka ambazo zinazokuja tunapoishi injili” Teaching, No Greater Call, 159). Baada ya kushirikisha ujumbe huu, fikiria juu ya kuwaalika wanafamilia kushirikisha uzoefu ambao wamepata walipolenga juu ya Mwokozi wakati wa kipindi cha Krismasi.