2010
Jukumu letu la Kushiriki katika Kazi ya Hekalu na Historia ya Familia
Desemba 2010


Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Desemba 2010

Jukumu letu la Kushiriki katika Kazi za Hekalu na Historia ya Familia

Soma kifaa hiki, na kama inavyostahili kizungumzie pamoja na kina dada unaowatembelea. Tumia maswali ili kukusaidia kuwaimarisha dada zako na kuufanya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kuwa sehemu hai ya maisha yako mwenyewe.

Relief Society seal

Imani • Familia • Usaidizi

Kwa karne nyingi zilizopita watu wengi walikufa bila elimu ya injili. Wengine kati ya watu hao ni jamii ya karibu na wa mbali. Wanakungojea wewe ufanye utafiti unaohitajika wa kuunganisha familia zenu pamoja na kufanya maagizo ya kuokoa kwa niaba yao.

Mahekalu mengi ulimwenguni hayatumika vya kutosha. Bwana ameahidi kwamba mioyo yenu itageuikia mababu ili kwamba ulimwengu hautaharibiwa wakati wa ujio Wake (ona M&M 2:2–3)

Kuna baraka za kibinafsi unazopokea kama matokeo ya ushiriki katika kazi ya hekalu na historia ya familia. Moja wa hizi ni furaha unayohisi unapowahudumia wahenga wako. Ingine ni kwamba utaweza kuhitimu kwa kibali cha hekalu, inayoonyesha ustahilivu wako mbele ya Bwana. Wale wasiowastahilivu leo wana nafasi ya kuwa na kibali wanafaa kushughulika pamoja na askofu au rais wa tawi ili kuhitimu mara moja iwezekanavyo. Tafadhali usiwe bila hii sifa muhimu. Nashuhudia kwamba Upatanisho ni kweli na kwamba dhambi zinaweza kusamehewa palipo toba sahihi.

Tunaposhiriki katika kazi ya hekalu na historia ya familia, kwa kweli tutapata Roho wa kutufariji katika changamoto zetu na kutuongoza katika maamuzi muhimu. Kazi ya hekalu na historia ya familia ni sehemu ya kazi yetu ya kutoa msaada, au huduma, kwa wahenga wetu.

Kutoka kwa Historia Yetu

“Nabii Joseph Smith alisema, ‘Jukumu kuu katika ulimwengu huu ambalo Mungu ameweka juu yetu ni kuwatafuta wafu wetu’ (Historia ya Kanisa,6:3:13) Tangu mwanzoni, kina dada wa Muungano wa Usaidizi wa akina Mama walihimili kazi hii kuu. Katika Nauvoo mnamo 1842, tamaa ya Sarah M. Kimball ya kuwasaidia wajenzi wa hekalu kulifanya kikundi cha kina dada kujipanga wenyewe ili kwamba waweze kuhudumu vya kufaa zaidi. Walipoanza kukutana, Nabii … alianzisha Muungano wa kwanza kulingana na mfano wa ukuhani. Kutoka wakati huo kuendelea mbele, kina dada wa Muungano wa Usaidizi wa kina Mama walisaidia kuendeleza kazi kwenye Hekalu la Nauvoo. …

Mnamo 1855, miaka minane baada ya watakatifu wa kwanza kuwasili katika Utah, Nyumba ya Endaumenti ilianzishwa. Eliza R. Snow, ambaye alikuwa mmoja wa washiriki wa waanzilishi wa Muungano wa Usaidizi wa kina Mama wa kwanza na alikuwa amehifadhi kumbukumbu za kikundi hicho, aliitwa na Rais Brigham Young mnamo 1866 kuwa rais wa Muungano wa Usaidizi wa kina Mama. Yeye na kina dada wengine walikuwa wafanyikazi waaminifu katika Nyumba ya Endaumenti. Basi, jinsi mahekalu ya St. George, Logan na Manti yalipomalizika, kina dada hawa walisafiri hata kwenye kila hekalu ili waweze kufanya kazi ya wafu hapo.”1

Muhtasari

  1. Mary Ellen Smoot, “Family History: A Work of Love,” Ensign, Mar. 1999, 15.

Ninaweza Kufanya Nini?

  1. Niwezaje kuwasaidia kina dada zangu kutafuta wahenga wao na kufanya maagizo ya hekalu kwa niaba yao? Fikiria hali ya kila dada unapotafakari jinsi ya kutimiza mahitaji yake. Unaweza kufikiria kwamba kazi ya familia inaweza kila mara kuwaimarisha washiriki wapya, wanaorejea, na wale wasio washiriki kamili.

  2. Ni wakati gani ambapo kazi ya hekalu na historia ya familia ilinifariji mimi katika changamoto zangu au kuniongoza katika maamuzi muhimu?

Kwa maelezo zaidi, nenda kwenye www.reliefsociety.lds.org.