Ujumbe Wa Urais wa Kwanza, Aprili 2011
Hayupo Hapa, ila Amefufuka
Hivi leo, magofu yamebaki Kapernaumu, mji huo wa pwani, kiini cha kazi ya Mwokozi huko Galilaya. Hapa, alihubiri kwenye sinagogi., akafundisha ukingoni mwa bahari, na kuponya nyumbani.
Katika mwanzo wa huduma yake, yesu alichukua maandishi kutoka kwa Isaya: “roho ya Bwana Mungu i juu yangu Kwa sababu Bwaba amenitia mafuta niwahubirie wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao na hao waliofungwa habari ya kufunguliwa kwao” (Isaya 61:1; ona pia Luka 4:18) tamko dhahiri ya mpango wa kiungu wa kuokoa wana na mabinti wa Mungu
Lakini kuhubiri kwa Yesu huko Galilaya kulikuwa ni utangulizi tu. Mwana wa Adamu alikuwa na makutano ya kutisha kwenye mlima uitwao Golgotha.
Baada ya kutiwa nguvuni katika bustani la Gethsemane baada ya kushiriki chakula cha jioni cha mwisho, kuachwa na wafuasi wake, akitemewa mate, kuhukumiwa na kudunishwa, Yesu alipepesuka chini ya msalaba Wake Mkuu akielekea Kalvari. Alitoka katika ushindi na kuingia kwenye usaliti, mateso na kifo msalabani.
Katika maneno ya wimbo “The Holy City.”
Upeo ulibadilika. …
Asubuhi ilikuwa ya baridi na baridi kali,
Wakati vivuli vya msalaba vilipoinuka
Juu ya mlima pweke.1
Kwa ajili yetu Baba wa Mbinguni alimtoa mwanawe Kwa ajili yetu, Ndugu wetu Mkubwa alitoa maisha yake.
Katika wakati wa mwisho Bwana angegeuka Lakini hakufanya hivyo. Alipitia mambo yote ili aweze kuokoa vitu vyote: Binadamu, dunia, na uzima wote uliyowahi kuishi humo.
Hamna maneno katika Ukristo yaliyo na maana kuliko yale yaliyosemwa na malaika kwa Maria Magdalena aliyekuwa akilia na yule Maria mwingine walipokaribia kaburi ili kuuhudumia mwili wa Bwana wao. “Kwa nini mnamtafuta aliye hai katika wafu?” Hayupo hapa, amefufuka.
Mtamshi haya yaliponenwa, wale waliokuwa wameishi na kufa, wale wanaoishi sasa na siku moja watakufa, na wale walio bado hawajazaliwa na bado kufa walikombolewa.
Kutokana na ushindi wa Kristo dhidi ya mauti, sote tutafufuliwa. Huu ni ukombozi wa roho. Paulo aliandika:
Tena kuna miili ya mbinguni(selesitia), na miili ya duniani(telesitia): lakini fahari yake ile ya mbinguni(selestia) ni mbali , na fahari ya ile ya duniani(telestia) ni mbali.
“Kuna fahari moja ya jua, na fahari nyingine ya mwezi, na fahari nyingine ya nyota, maana iko tafauti ya fahari hata kati ya nyota na nyota.
“Kadhalika na kiyama ya watu” (1 Wakorintho 15:40–42).
Tunatafuta fahari ya mbinguni(selestia). Ni kwenye uwepo wa Mungu ndipo tunapotamani kukaa. Ni familia ya milele ndiyo tunataka kushiriki.
Kumhusu yeye aliyetukomboa kila mmoja wetu kutoka kwa kifo cha milele ndiyo nashuhudia kuwa ndiye mwalimu wa kweli, lakini ni zaidi ya mwalimu. Ni kielelezo cha maisha makamilifu, lakini ni zaidi ya kielelezo. Ni tabibu mkuu—lakini ni zaidi ya tabibu.Ni Mwokozi halisi wa ulimwengu, Mwana wa Mungu, Mfalme wa Amani, Mtakatifu wa Israeli, hata yeye Bwana aliyefufufka ambaye alitangaza, ‘Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, mimi ni yeye aliye hai, mimi ni yule aliyeuawa, Mimi ni Mwombezi wenu kwa Baba” (M&M 110:4).
“Ah, Raha inayoletwa na maneno haya:’ Ninajua Mkombozi wangu yu hai!’”2
Kwa haya nashuhudia.
© 2011 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa Imechapishwa USA Kiingereza kiliidhinishwa: 6/10. Tafsiri iliidhinishwa: 6/10. Tafsiri ya First Presidency Message, April 2011. Swahili. 09764 743