2011
Dhamira ya Muungano wa Usaidizi wa kina Mama
Aprili 2011


Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Aprili 2010

Dhamira ya Muungano wa Usaidizi wa kina Mama

Soma kifaa hiki, na kama ifaavyo, ukijadili pamoja na kina dada unaowatembelea. Tumia maswali ili kukusaidia kuwaimarisha dada zako na kuufanya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kuwa sehemu hai ya maisha yako mwenyewe.

Imani • Familia • Usaidizi

Wakati Urais wetu ulipoitwa, tulipewa vifaa kuhusu historia ya Muungano wa usaidizi wa Kina Mama. Tulisoma kwa maombi, kutaka kujua dhamira ya Muungano wa Usaidizi wa kina mama na Kile ambacho Bwana angetaka tufanye. Tulijifunza kwamba dhamira ya Muungano wa Usaidizi wa kina Mama ilivyopangwa na Bwana ni kupanga, kufundisha, na kihimiza mabinti zake ili kuwatayarisha kwa baraka za uzima wa milele.

Ili kutimiza dhamira hii ya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama Bwana amemtuma kila dada na muungano kwa ujumla:

  1. Kuongeza Imani na Wema wa Kibinafsi

  2. kuimarisha familia na nyumba

  3. Kutoa usaidizi kwa kumhudumia Bwana na watoto Wake.

Tunaweza kufanya hivi kwa njia ya Bwana ikiwa tutatafuta, tutapokea na kutenda kulingana na ufunuo wa kibinafsi. Bila ufunuo wa kibinafsi, hatuwezi kufaulu. Tukifuata ufunuo wa kibinafsi, hatuwezi kushindwa. Nabii Nefi anatuagiza kwamba Roho Mtakatifu atauonyesha “Vitu vyote tunavyosahili kutenda.” (2 Nefi 32:5). Ni sharti tukubali kuacha na kuwa kimya hivi kwamba tunaweza kusikia sauti ya Roho.

Akina dada tuna jukumu mihimu katika kusaidia kujenga ufalme wa Mungu na kuutayarisha kwa kuja kwake Bwana. Kwa hakika,kazi ya Bwana haiwezi kutimia bila usaidizi wa mabinti zake. Kwa sababu hiyo, Bwana anatutarajia kuzidisha matoleo yetu. Anatutarajia kutimiza dhamira yake ya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama sasa kuliko wakati wowote mwingine

Julie B. Beck, Rais wa Urais mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa akina Mama

Kutoka kwa Maandiko

Kumbukumbu ya Torati 6:5–7; Luka 10:30–37; Yakobo 1:27; 2 Nefi 25:26 ; Mosia 3:12–13

Kutoka kwa Historia Yetu

Katika mkutano wa Juni 9, 1842, wa Muungano wa Usaidizi wa Kina mama, Nabii Joseph Smith alifunza kina dada kwamba kitengo chao hakikuwa “tu kutuliza maskini, bali kuokoa nafsi.”1 Hii taarifa ya madhumuni ya kiroho pia ya kimwili imekuwa kielelezo cha Muungano wa Usaidizi wa Kina mama katika historia yake yote. Katika mwaka wa 1906 Rais Joseph F. Smith (1838–1918) alifunza: “[Muungano wa Usaidizi] haushughulikii tu mahitaji ya masikini, wagonjwa, na wenye mahitaji, bali sehemu ya kazi zake—na sehemu kubwa, pia—ni kushughulikia utunzaji wa kiroho na wakovu wa kina mama na mabinti wa Sayuni; ili kuona kwamba hamna yeyote aliyetelekezwa, bali kwamba wote wamelindwa dhidi ya mikosi, majanga, uwezo wa giza, na uovu ambao unaowatisha katika ulimwengu.2 Katika mwaka wa 2001 Mzee M. Russell Ballard wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili alisisitiza, “Kila dada katika Kanisa ambaye amefanya maagano na Bwana ana jukumu takatifu la kusaidia kuokoa nafsi, na kuongoza wanawake wa ulimwengu, kuimarisha nyumba za Sayuni, na kujenga ufalme wa Mungu.”3

Muhtasari

  1. Joseph Smith, katikaHistory of the Church, 1:78.

  2. Teachings of Presidents of the Church: Joseph F. Smith (1998), 185 xiv, 21–22

  3. M. Russell Ballard, “Women of Righteousness,” Liahona, Des. 2002, 39.

Ninaweza Kufanya Nini?

  1. Ni ari gani niliyopokea ili kuwasaidia dada zangu kuongeza imani na utakatifu wa kibinafsi na kuimarisha familia ma nyumba zao? Naweza kutoa usaidizi gani?

  2. Nitatumiahje ujumbe huu kuimarisha imani yangu na kuongeza kujitolea kwangu ka ajili ya utakatifu wa kibinafsi?