2011
Nafasi za Kutenda Wema
Mei 2011


Nafasi za Kutenda Wema

Njia ya Bwana kuwasaidia wale walio na mahitaji ya maisha ya sasa huhitaji watu ambao, kwa upendo hujitenga na kutenga yale waliyo nayo kwa Mungu na kazi yake.

Kina ndugu na dada zangu wapendwa, nia ya maongezi yangu ni kuheshimu na kusherehekea kile ambacho Bwana ametenda na anaendela kutenda kuwahudumia watoto wake walio maskini na wenye mahitaji hapa duniani. Anawapenda watoto wake walio na mahitaji na walio na haja ya usaidizi Na ameweka njia za kuwabariki wote walio na mahitaji na pia wale wanaotoa usidizi huo.

Baba yetu wa Mbinguni husikia maombi ya watoto wake ulimwenguni wanaoomba kwa ajili ya chakula, nguo za kufunika miili yao na kwa heshima inayotokana na kuweza kujikimu. Maombi hayo yamemfikia tangu alipowaweka waume na wake ulimwenguni.

Unajifunza kuhusu mahitaji hayo mahali unapoishi na ulimwenguni kote. Mara nyingi moyo wako unaguswa na hisia za huruma. Ukikutana na mtu anayejitahidi kupata ajira, unahisi haja ya kumsaidia. Unapata hisia hiyo unapoenda katika nyumba ya mjane na kuona kuwa hana chakula. Unahisi unapoona picha ya watoto wakilia wakikaa katika vifusi vya nyumba yao iliyoangamizwa kwa moto au kwa mtetemeko wa ardhi.

Kwa sababu Bwana husikia kilio chao na kuhisi huruma wako kwao, kutoka mwanzo wa nyakati ametoa njia kwa wafuasi wake kusaidia. Amewaalika watoto Wake kuweka wakfu wakati wao, mali yao na nafsi zao na kuungana naye katika kuwahudumia wengine.

Njia yake ya kuwasaidia wakati mwingine huitwa kuishi maisha ya kuweka wakfu. Katika kipindi kingine, njia yake iliitwa njia ya muungano. Katika nyakati zetu unaitwa mpango wa ustawi wa Kanisa

Majina na mbinu za utendaji kazi umebadilishwa ili kufaa mahitaji na hali za watu. Lakini kila wakati njia ya Bwana ya kusaidia wenye mahitaji ya sasa huhitaji watu ambao, kwa upendo wamejiweka wakfu na mali yao kwa Mungu na kufanya kazi yake.

Ametualika na kutuamrisha kushiriki katika kazi yake ili kuwainua walio na mahitaji. Tunafanya maagano kufanya hayo katika maji ya ubatizo na katika mahekalu matakatifu ya Mungu. Tunaweka upya agano siku ya Jumapili tunaposhiriki sakramenti.

Nia yangu siku ya leo ni kueleza baadhi ya nafasi ambazo ametoa kwetu ili tuwasaide wengine wenye mahitaji. Siwezi kuzungumzia yote haya katika wakati wetu mfupi. Matumaini yangu ni kuweka upya na kuimarisha kujitolea kwako kwa kutenda.

Kuna wimbo kuhusu mwaliko wa Bwana kwa kazi hii ambao nimeuimba tangu nilipokuwa mvulana mdogo. Katika utotoni wangu nilizingatia sana sauti tamu kuliko nguvu ya maneno. Naomba kuwa utahisi maneno haya moyoni mwako hivi leo. Sikiliza maneno haya tena:

Je nimetenda wema wowote hivi leo?

Je, nimesaidia yeyote aliye na mahitaji?

Je, nimechangamsha walio na huzuni na kufanya mtu kuhisi furaha?

Ikiwa sivyo nimekosea sana

Je, mzigo ya yeyote umerahisihwa leo

kwa nilikuwa radhi kushiriki?

Je, wagonjwa na wadhaifu wamesaidiwa njiani mwao?

Walipohitaji usaidizi, je nilikuwepo?

Basi amka na kutenda jambo zaidi

Ya kufikiria makao yako juu

Kufanya wema ni raha, furaha kupita kipimo

Baraka ya jukumu na upendo.1

Bwana mara kwa mara hutuma wito kwetu sote. Wakati mwingine inaweza kuwa hisia ya ghafla ya huruma kwa mtu aliye na mahitaji Baba anaweza kuhisi alipoona mtoto akianguka na kuumia goti. Mama anaweza kuhisi anaposikia kilio chenye uoga cha mtoto wake usiku. Mwana au binti anaweza kuhisi huruma kwa mtu aliyeonekana kuwa mwenye huzuni au uoga shuleni.

Sisi sote tumeguswa na hisia za huruma kwa wengine hata tusiowajua. Kwa mfano, uliposikia taarifa za mawimbi yaliyopiga pacific baada ya tetemeko la ardhi huko Japan, ulihisi huruma kwa walioweza kuwa waliumia.

Hisia za huruma ziliwajia maelfu wenu waliojua kuhusu mafuriko katika Queensland, Australia. Ripoti za habari zilikuwa hasa ni idadi ya watu wenye mahitaji. Lakini wengi wenu walihisi uchungu wa watu. Ujumbe wa mwito ulijibiwa na washiriki 1500 au zaidi wa Kanisa wa kujitolea huko Australia ambao walikuja kusaidia na kufariji.

Waligeuza hisia zao za huruma kuwa uamuzi wa kutenda kulingana na maagano yao. Nimeona baraka zinazomjia mtu mwenye shida anayepokea msaada na kwa mtu anachukua fursa ya kutoa msaada huo.

Wazazi wenye hekima uona katika kila mahitaji ya wengine njia ya kuleta baraka katika maisha ya wana na mabinti zao. Watoto watatu juzi walibeba mikasha yenye chakula kitamu kwenye mlango wetu wa mbele. Wazazi wao walijua kuwa tulihitaji msaada na waliwajumuisha watoto wao katika fursa ya kutuhudumia.

Wazazi walibariki familia yetu kwa huduma yao karimu. Kwa chaguo lao la kuwaruhusu watoto wao kushiriki kwa kutoa, walieneza baraka kwa wajukuu wao. Tabasamu za watoto walivyotoka nyumbani mwetu zilinipa hakikisho kwamba wajukuu hawa watabarikiwa. Watawaambia watoto wao kuhusu furaha waliohisi kwa kupeana huduma njema kwa Bwana. Nakumbuka hisia hiyo tulivu toka utotoni nilipong’oa magugu kwa jirani kwa mwaliko wa baba yangu. Wakati wowote ninapoalikwa kuwa mtoaji, Naukumbuka na kuamini wimbo, “Kazi ndio tamu, Mungu wangu, Mfalme wangu.”2

Najua mashairi hayo yaliandikwa ili kuelezea furaha inayokuja kwa ajili ya kumwabudu Bwana siku ya Sabato. Lakini watoto hao mlangoni mwetu walikuwa wakihisi jioni siku ya juma furaha ya kufanya kazi ya Bwana. Na wazazi wao waliona fursa hiyo ili kuweza kutenda wema na kueneza furaha kwa vizazi.

Njia ya Bwana ya kuhudumia wenye shida inatoa fursa nyingine kwa wazazi kubariki watoto wao. Niliona kanisani Jumapili moja. Mtoto mdogo alimpa askofu toleo la bahasha alivyokuwa akiingia kanisani kabla ya mkutano wa sakramenti.

Niliijua familia hiyo na kijana yule. Familia walikuwa wametambua kuhusu mtu katika kata mwenye mahitaji. Baba wa mvulana huyu alikuwa amesema kitu kama hiki kwa mtoto alivyoongezea zaidi toleo lake la kufunga katika bahasha. “Tulifunga leo na kuomba kwa wenye mahitaji. Tafadhali peana bahasha hii kwa askofu kwa niaba yetu. Najua kuwa ataipeana ili kusaidia wenye mahitaji makubwa kuliko yetu.”

Badala ya uchungu wowote wa njaa Jumapili hiyo kijana atakumbuka siku hiyo kwa hisia za furaha. Ningeweza kutambua kutokana na tabasamu lake na jinsi alivyoshikilia bahasha ile kwa nguvu kiasi kwamba alihisi uaminifu mkubwa wa baba yake ili kuweza kubeba toleo la familia kwa ajili ya maskini. Ataikumbuka siku hiyo alipokuwa shemasi, na pengine milele.

Niliona furaha hiyo sawa katika nyuso za watu binafsi waliosaidia watu kwa ajili ya Bwana huko Idaho miaka iliopita. Bwawa la Teton libomoka Jumamosi, Juni 5, 1976. Watu kumi na moja waliuawa. Maelfu iliwabidi kuhama maboma yao kwa masaa machache. Boma zingine zilisombwa na maji. Na mamia ya makazi yangeweza kufanywa pa kuishi kupitia kwa kazi na mpangilio zaidi ya uwezo wa wenyeji.

Wale waliosikia kuhusu janga hilo waliona huruma na kuhisi mwito wa kutenda wema. Majirani, maaskofu, marais wa Muungano wa Usaidizi wa kina Mama, viongozi wa jamii, waalimu wa nyumbani na watembelezi waliacha makazi na kazi ili kuweza kusafisha nyumba za wengine zilizofurika.

Mmoja wa wachumba alirudi Rexburg kutoka mapumzikoni baada ya mafuriko. Hawakuenda kuona nyumba yao. Badala yake, walipata askofu wao na kuuliza mahali ambako wangesaidia. Aliwaelekeza kwa familia iliyokuwa na mahitaji.

Baada ya siku chache walienda kuangalia nyumba yao. Haikuwepo, ilisombwa katika mafuriko. Walitembea kurudi kwa askofu na kuuliza, “Sasa ungetaka tufanye nini?”

Popote mnapoishi, mmeona mwujiza huo wa huruma ukigeuzwa kuwa tendo la upendo. Pengine si kwa sababu ya janga kuu la asili. Nimeuona katika jamii za ukuhani ambapo ndugu anaamka kuelezea mahitaji ya mwanamume au mwanamke anayetafuta nafasi ya ajira ili kujimudu au kumudu familia yake. Ningeweza kuhisi huruma chumbani, bali wengine walidokeza majina ya watu ambao wangeajiri mtu aliyehitaji ajira.

Kilichofanyika katika jamii hiyo ya ukuhani na kilichofanyika katika nyumba zilizofurika za Idaho ni dhihirisho la njia ya Bwana ya kuwasaidia wenye mahitaji makubwa kuweza kujitegemea. Tunahisi huruma na tunajua jinsi ya kutenda kwa njia ya Bwana ili kusaidia

Tunasherehekea maadhimisho ya 75 ya mpango wa ustawi wa Kanisa mwaka huu. Ulianzishwa kutimiza mahitaji ya wale walipoteza ajira, mashamba na hata makazi kwa kile kilichokuja kujulikana kama “The Great Depression.”

Mahitaji makubwa ya kidunia ya watoto wa Baba wa Mbinguni yamerudi tena katika nyakati zetu jinsi yalivyokuwa na jinsi yatakavyokuwa wakati wote. Kanuni katika msingi wa Mpango wa Ustawi wa Kanisa sio tu kwa wakati moja au mahali moja. Ni kwa wakati wote na pahali pote.

Kanuni hizi ni za kiroho na za milele. Kwa sababu hiyo, kuzielewa kuziweka mioyoni mwetu kutatuwezesha kuona na kutumia fursa za kusaidia wakati wowote na popote Bwana anapotualika.

Hapa kuna kanuni zingine zilizoniongoza nilipotaka kusaidia kwa njia ya Bwana na wakati nimeweza kusaidiwa na wengine.

Kwanza, watu wote wana furaha na wanahisi kuheshimika kibinafsi wanapoweza kujikimu na kukimu familia zao na halafu kufikia ili kutunza wengine. Nimekuwa na shukrani kwa wale walionisaidia kutimiza mahitaji yangu. Nimekuwa na shukrani zaidi kwa miaka iliyopita kwa wale walionisaidia kuweza kujitegemea. Na nimekuwa hata na shukrani zaidi kwa wale walionielekeza jinsi ya kutumia masalio yangu kwa kuwasaidia wengine.

Nimejifunza kwamba njia ya kupata masalio ni kutumia kidogo kuliko ninavyopata. Kwa masalio hayo nimeweza kudhibitisha katika nyakati za furaha kwamba ni vyema kupeana kuliko kupokea. Hiyo kwa kiwango ni kwa sababu tunapopeana usaidizi kwa njia ya Bwana, Yeye hutubariki.

Rais Marion G. Romney alisema kuhusu kazi ya ustawi, “Katika kazi hii huwezi kutoa na kubakia masikini.” Halafu akadokeza rais wake wa misheni, Melvin J. Ballard, kwa njia hii: “Mtu hawezi kumpatia Bwana gamba la mkate bila kupokea mkate kamili badala yake.”3

Nimegundua hiyo kuwa kweli maishani mwangu. Ninapokuwa mkarimu kwa watoto wa Baba wa Mbinguni wenye mahitaji, Yeye ni mkarimu kwangu.

Kanuni ya pili ambayo imekuwa ni mwongozo kwangu katika kazi ya ustawi ni uwezo na baraka ya umoja. Tunapoungana mikono kuwahudumia walio na mahitaji, Bwana huunganisha mioyo yetu. Rais J. Reuben Clark, Jr. alisema hivi: “Kwamba kutoa … kumeleta … hisia ya undugu kwa sababu watu wa aina yote ya mafunzo na kazi wameweza kufanya kazi kwa karibu katika bustani la Ustawi au kazi nyingine.”4

Hisia hiyo iliyoongezeka ya undugu ni kweli kwa mpokeaji vile vile kwa mtoaji. Hadi siku ya leo, mwanaume ambaye nilichimba matope pamoja naye nyumbani mwake iliofurika huko Rexburg ni rafiki yangu. Na anahisi heshima kuu ya kibinafsi kwa kuweza kufanya yote ambayo awezayo kwake mwenyewe na kwa familia yake. Kama tungefanya peke yetu, sisi sote tungepoteza baraka ya kiroho.

Hiyo inaelekeza kwa kanuni ya tatu kwangu ya matendo kwa kazi ya ustawi: Jumuisha familia yako kwa kazi pamoja nawe ili waweze kujifunza kutunzana wanavyotunza wengine. Wana na Mabinti zenu wanaofanya kazi pamoja nanyi ili kuhudumia wengine wenye mahitaji wataweza kwa urahisi kuwasaidia wengine wanapokuwa kwa shida.

Kanuni ya nne ya Ustawi wa Kanisa niliyojifunza kama askofu. Ilitoka kwa amri ifuatayo ya maandiko ya kuwasaidia masikini. Ni jukumu la askofu kupata na kupeana usaidizi kwa wale ambao bado wanahitaji usaidizi baada ya yote ambayo wao na familia yao inaweza kufanya. Nilipata kuwa Bwana hutuma Roho Mtakatifu ili kuwezesha “Ombeni, nanyi mtapewa” katika kutunza masikini kama ilivyo katika kupata ukweli.5 Lakini pia nilijifunza kuhusisha Rais wa Muungano wa Uasidizi wa Kina Mama katika utafutaji huo. Anawaza kupata ufunuo mbele yako.

Wengine wenu mtahitaji mwongozo huo katika miezi iliyo mbele. Ili kusherehekea maadhimisho ya 75 ya Mpango wa Ustawi wa Kanisa washiriki ulimwenguni kote wataalikwa kushiriki katika siku ya huduma. Viongozi na washiriki watatafuta ufunuo wanavyopanga miradi.

Nitatoa vidokezo vitatu unavyopanga mradi wako wa huduma.

Kwanza, jitayarishe na wale unaowaongoza kiroho. Ikiwa tu mioyo imelainishwa tu na Upatanisho wa Mwokozi ndipo utakavyoweza kuona wazi kwamba lengo la mradi ni kubariki maisha ya watoto wa Baba wa Mbinguni

Dokezo langu la pili ni kuchagua wapokeaji wa huduma yako wawe ni watu walio katika ufalme au katika jamii ambao mahitaji yao yatagusa mioyo ya wale watakaopeana huduma. Watu wanaowahudumia watahisi upendo wao. Hiyo itafanya kuhisi si furaha tu kama vile wimbo ulivyoahidi, kuliko kutimiza mahitaji yao ya kimwili.

Dokezo langu la mwisho ni kupanga kutumia uwezo wa umoja wa familia, wa jamii, miungano ya usaidizi, na watu unaowajua katika jamii zenu. Hisia za umoja zitaongeza matokeo mema ya huduma unayopeana. Na hisia hizo za umoja katika familia, katika Kanisa, na jamii zitakua na kuwa hiba ya kudumu miaka mingi baada ya kumalizika kwa mradi.

Hii ni fursa yangu ya kuwaambia ni kiasi gani ninawapenda. Kwa huduma ya upendo ambayo mmepeana kwa niaba ya Bwana nimekuwa mpokeaji wa shukrani za watu ambao mmesaidia kama vile nilivyokutana nao duniani.

Mlipata njia ya kuwainua juu mlivyohudumu katika njia ya Bwana. Ninyi na wanafunzi wakarimu wa Mwokozi kama ninyi mmetupa chakula chenu usoni pa maji katika huduma na watu mliowasaidia wamejaribu kunipatia mimi mkate wa shukrani.

Napokea onyesho la shukrani sawa na hilo kutoka kwa watu waliofanya kazi pamoja nanyi. Nakumbuka siku moja nikisimama kandoni mwa Rais Ezra Taft Benson. Tulikuwa tukizungumza juu ya huduma katika Kanisa la Bwana. Alinishangaza kwa ari yake ya ujana aliposema, akibonyeza mkono wake, “Naipenda kazi hii, na ni kazi!”

Kwa niaba ya Bwana naeneza shukrani kwa kazi yenu ya kuhudumia watoto wa Baba yetu wa Mbinguni. Anawajua na anaona juhudi zenu, bidii, na kujitolea kwenu. Naomba kwamba Atawapa baraka ya kuona mazao ya kazi yenu kwa furaha ya wale uliowasaidia kwa ajili ya Bwana.

Najua kuwa Mungu na Baba yu hai na husikiza maombi yetu. Najua kuwa Yesu ndiye Kristo. Ninyi na wale mnaowahudumia mnaweza kutakaswa na kuimarishwa kwa kumhudumia na kutii amri Zake. Mnaweza kujua namna ninavyojua, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, kwamba Joseph Smith alikuwa nabii wa Mungu wa kurejesha Kanisa la kweli na linaloishi, ambalo ni hili. Nashuhudia kuwa Rais Thomas S. Monson ni nabii hai wa Mungu. Yeye ni mfano wa kile Bwana alichokifanya: alienda akitenda wema Naomba kuwa tuchukue nafasi zetu “kuinua mkono iliyodhaifu na kuimarisha magoti yaliyo dhaifu”6 Katika jina tatakitu la Yesu Kristo, amina.