2011
Ahadi za thamani za Kitabu cha Mormoni
Oktoba 2011


Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Oktoba 2011

Ahadi za thamani za Kitabu cha Mormoni

Miaka mingi iliyopita nilisimama katika upande wa kitanda wa baba kijana aliponing’nia kati ya uzima na kifo Mke wake mwenye huzuni na watoto wao wawili walisimama karibu Aliuchukua mkono wangu kwake, na kwa mtazamo wa huruma, alisema, “Askofu, Ninajua kuwa niko karibu kufa. Niambie kitakachofanyika kwa moyo wangu nitakapokufa.”

Nilifanya maombi ya kimya kwa maongozi ya mbinguni na nikaona katika sehemu ya kitanda nakala ya muungano wa utatu wa maandiko. Nilichukua kitabu hicho na kufungua kurasa mara nikagundua kuwa, bila bidii kwa upande wangu nilitua katika sura ya 40 katika Alma kwenye Kitabu cha Mormoni. Nilisoma maneno haya kwake:

“Tazama, nimejulishwa na malaika kwamba roho za watu wote, mara zinapotoka kwa mwili huu wa muda … zinachukuliwa nyumbani kwa yule Mungu ambaye alizipatia uhai.

“Na …roho za wale walio haki zinapokelewa kwa hali ambayo ni ya furaha, ambayo inaitwa peponi, hali ya kupumzika, hali ya amani, ambapo zitapumzikia kutoka kwa taabu zao zote na kutoka kwa mashaka yote na masikitiko” (Alma 40:11–12).

Nilipoendelea kusoma kuhusu Ufufuo, mng’aro ulijia uso wa kijana huyo na tabasamu likavaa midomo yake. Nilipohitimisha matembelezi yangu, niliaga familia hii nzuri.

Nilimwona mke na watoto mara nyingine katika mazishi. Ninafikikiria tena kuhusu usiku huo wakati ambapo kijana aliomba ukweli na kutoka kwa Kitabu cha Mormoni alisikia jibu kwa swali lake.

Kutoka katika Kitabu cha Mormoni, uja ahadi zingine zenye thamani, zikiwemo ahadi za amani, uhuru, na baraka “ikiwa tutatumikia Mungu wa pekee katika Nchi, ambaye ni Yesu Kristo” (Etheri 2:12).

Kutoka kwa kurasa zake hutoka “ahadi ya furaha isiyo na kikomo” kwa “wale wanaotii amri za Mungu. Kwani tazama, wanabarikiwa katika vitu vyote, vya muda na vya kiroho” (Mosia 2:41).

Kutoka kwa kurasa zake uja ahadi za ‘furaha isiyo na kifani’ kwa wale wanaokuwa “vyombo mikononi mwa Mungu” katika kuwaokoa wana na binti zake wenye thamani. (Alma 28:8; 29:9).

Kutoka kwa kurasa zake uja ahadi kwamba Israeli iliyotawanyika itakusanywa katika kazi ambayo tunajihusisha nayo kupitia kwa juhudi zetu kuu za umisionari duniani kote. (ona 3 Nefi 16; 21–22).

Kutoka kwa kurasa zake uja ahadi kwamba tunapoomba kwa Baba katika jina takatifu la Yesu Kristo familia zetu zitabarikiwa. (ona 3 Nefi 18:21).

Kutoka kujifunza kutoka kwa kurasa zake uja utimilifu wa unabii kwamba “kutakuwa maishani mwenu na nyumbani mwenu ongezeko la uwepo wa Roho wa Bwana, uamuzi imara wa kutembea katika utii wa amri zake na ushuhuda imara wa uhalisi wa kuishi kwa Mwana wa Mungu.”1

Na kutoka kwa kurasa za Kitabu cha Mormoni, uja ahadi ya Moroni kwamba kupitia kwa maombi, na nia ya kweli, na imani katika Kristo, tunaweza kufahamu ukweli wa ahadi hizi “kwa nguvu za Roho Mtakatifu” (ona 3 Nefi 18:21).

Pamoja na manabii wengine wa siku za mwisho, nashuhudia ukweli wa “kitabu kilicho sahihi kuliko vingine vyote duniani,”2 hata Kitabu cha Mormoni, ushuhuda mwingine wa Yesu Kristo. Ujumbe wake unajumlisha dunia na kuwaletea wasomaji elimu ya ukweli Ni ushuhuda wangu kwamba Kitabu cha Mormoni hubadili maisha. Hebu na kila mmoja wetu akisome na kukisoma tena. Na hebu tushiriki kwa furaha shuhuda zetu za ahadi zake za thamani na watoto wote wa Mungu

Muhtasari

  1. Gordon B. Hinckley, “Ushuhuda Imara na wa Kweli,” Liahona, Agosti. 2005, 6.

  2. Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith (2007), 64.

Kufundisha kutoka kwa Ujumbe huu

Katika maandiko, “tunapata kanuni za kweli ambazo zitatatua utata na mataizo yoyote na kila utanzu utakaokumba jamii ya wanadamu” (Teaching, No Greater Call [1999], 51). Unaposhiriki ujumbe wa Rais Monson na familia, waalike kusikiliza ‘ahadi za thamani’ anazotambulisha katika kitabu cha Mormoni. Unaweza kushiriki ahadi katika Kitabu cha Mormoni ambazo zimekuwa na maana kwako.