2011
Kama Tusipokuwa na shaka
Oktoba 2011


Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Oktoba 2011

Kama Tusipokuwa na Shaka

Julie B. Beck, Rais mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa akina Mama

Soma kifaa hiki, na kama ifaavyo, ukijadili pamoja na kina dada unaowatembelea. Tumia maswali ili kukusaidia kuwaimarisha dada zako na kuufanya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kuwa sehemu hai ya maisha yako mwenyewe.

Imani • Familia • Usaidizi

Katika kitabu cha Mormoni, tunasoma kuhusu vijana wenye mfano waliokuwa imara sana, wajasiri na wenye nguvu. “Ndio walikuwa watu wa ukweli na wenye busara kwani walikuwa wamefundishwa kutii amri za Mungu na kutembea wima mbele zake” (Alma 53:21). Vijana hawa waaminifu walisifu akina mama zao waliokuwa mifano na waalimu wao.

Akina mama wa wapiganaji wa Helamani waliishi katika nyakati zisokuwa sawa na zetu. Hali zao zilikuwa ngumu na hatari, na vijana walikuwa wakiitwa kulinda uhuru wa kimwili na kiroho. Hivi leo, tunaishi katika ulimwengu ambapo “kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama bali ni juu ya falme na mamlaka juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho” (Waefeso 6:12)

Nyakati zenye changamoto zinahitaji wazazi imara na walio mifano, wanaofundisha ukweli ambao wapiganaji wa Helamani walijua: “Ikiwa hawakuwa na shaka, Mungu angewakoa” (Alma 56:47) Kufundisha na kutoa mfano wa kweli hii kunahitaji uangalifu. Hata hivyo, hatufai kuogopa tunapofahamu kuwa sisi ni nani na kuwa Mungu ni nani, na tumefanya maagano naye, sisi, kama akina mama wa wapiganaji tutakuwa na ushawishi mkuu kwa mema.

Huenda ikawa, kila mmoja wa wapiganaji 2060 wa Helamani alishawishiwa na mama. Lakini kina mama hawa hawakufanya hivyo peke yao. Pamoja na wanaume na wanawake wengine wenye haki, akina mama hao ni lazima waliunganisha imani na mfano wao kufundisha nguvu za maagano. Vijana wa nyakati hiyo walifahamu agano ambalo wazazi wao walifanya kutoshiriki katika vita Na hata inapoonekana kutowezekana, Baba wa Mbinguni mwenye upendo alifungua njia kwa wazazi hawa kuweka maagano yao na kutunza uhuru wao. (ona Alma 56:5–9). Nasi vivyo hivyo ni sharti tuheshimu maagano yetu ili watoto na vijana, —watoto wetu na wale walio katika kata, matawi na ujirani na jamii zetu—waelewe na kuimarisha uwekaji wa maagano.

Tunapoheshimu maagano yetu, Baba wa Mbinguni ataweza kutayarisha njia kwa ajili yetu. Tunafaa kuishi maagano yetu kwa ukamilifu. Tunaweza, kwa mfano, kuwa wakamilifu katika kusoma maandiko, kuwa na sifu ya hekaluni na katika kuvaa kwa heshima na kuheshimu Sabato. Tunapofanya hivi watoto wetu watajua na kuweza kusema “hatuna shaka mama zetu walijua” (Alma 56:48).

Akina mama watakatifu wa siku za mwisho wanaotambua kuwa nguvu zao zinatoka kwa Upatanisho wa Bwana hawafi moyo wakati wa matatizo na kuvunjika moyo. Kama wawekaji wa Maagano, tunafaulu katika kuinua, kulea, na kuwalinda watoto na vijana ili siku moja tunaweza kusema hivi kuhusu kizazi hiki kinachoinuka, “Kamwe sijaona ujasiri mkubwa hivyo, hapana, sio miongoni mwa wote” (Alma 56:45).

Kutoka kwa Maandiko

Alma 53; 56–58

Ninaweza Kufanya Nini?

  1. Ninawezaje kusaidia dada zangu kutambua na kutumia uwezo walio nao ili kushawishi kizazi kinachokua?

  2. Ni mwongozo upi nitakaopata katika kitabu cha Mormoni ili kujibu changamoto ninazokumbana nazo leo?

Chapisha