2012
‘Amefufuka’ —Ushuhuda wa Nabii
Aprili 2012


Ujumbe Wa Urais wa Kwanza, Aprili 2012

“Amefufuka”

Ushuhuda wa Nabii

“Mwito wa Ukristo,” Rais Thomas S Monson ametangaza, ni kwamba Yesu wa Nazareti alifufuka kutoka kwa wafu. “Uhalisi wa Ufufuo unatoa kwa wote amani inayoshinda fahamu zote” (Ona Wafilipi 4:7).1

Katika vidondoo vifuatavyo, Rais Monson anashiriki ushuhuda wake na shukrani kwa ufufuo wa Mwokozi na kutangaza kuwa kwa sababu Mwana alishinda kifo, watoto wote wa Baba yetu wa Mbinguni wanaokuja ulimwenguni wataishi tena.

Maisha baada ya Maisha ya Muda

“Ninaamini kuwa hakuna hata mmoja kati yetu anayeweza kuelewa umuhimu halisi wa kile Kristo alitufanyia kule Gethsemane, lakini nina shukrani kila siku ya maisha yangu kwa dhabihu Yake ya upatanisho kwa niaba yetu.

“Wakati wa mwisho, angerudi nyuma. Lakini hakufanya hivyo. Alipitia chini ya vitu vyote ili aweze kuokoa vitu vyote. Kwa kufanya hivyo, alitupatia maisha kupita hali ya kuwa katika maisha ya muda. Alitukomboa kutokana na Kuanguka kwa Adamu.

“Hadi katika kina cha moyo wangu, nina shukrani kwake. Alitufunza jinsi ya kuishi. Alitufunza jinsi ya kufa. Alihakikisha wokovu wetu.”2

Kuondosha Giza la Kifo

“Katika hali zingine, katika mateso makuu na kifo huja malaika wa huruma. Lakini mara nyingi tunafikiri kuwa ni adui wa furaha.

“Giza la kifo daima linaweza kuondoshwa kwa mwanga wa ukweli uliofunuliwa. ‘Mimi ni ufufuo na uhai,’ alisema Bwana. ‘Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi: Naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele.’

“Uhakikisho huu—ndiyo, hata uthibitisho—wa uhai baada ya kaburi unaweza kutoa amani iliyoahidiwa na Bwana alipowahakikishia wafuasi wake: ‘Amani nawaachieni, Amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu wala msiwe na woga.’”3

Hayuko hapa

“Mwokozi wetu aliishi tena. Tukio la kufariji, lenye hakikisho na tukufu zaidi kuliko yote katika historia ya wanadamu lilikuwa limetokea—ushindi juu ya kifo. Uchungu na mateso ya Gethsemani na Kalvari ulikuwa umefutiliwa mbali. Wokovu wa wanadamu ulikuwa umehakikishwa. Kuanguka kwa Adamu kulikuwa kumeongolewa.

“Kaburi iliyokuwa tupu asubuhi hiyo ya Pasaka ilikuwa jibu kwa swali la Ayubu, ‘Mtu akifa, je! Atakuwa hai tena?’ Kwa wote walio katika karibu kwa sauti yangu, Ninatangaza, Mtu akifa, atakuwa hai tena. Tunajua kwa sababu tuna nuru ya ukweli uliofunuliwa …

“Ndugu na dada zangu wapendwa, katika wakati wa huzuni wetu wa kina zaidi, tunaweza kupata amani ya ajabu kutoka kwa maneno ya malaika asubuhi hiyo ya kwanza ya Pasaka: ‘Hayupo hapa Kwani amefufuka.’”4

Wote Wataishi Tena

“Tunacheka, tunalia, tunafanya kazi, tunacheza, tunapenda, tunaishi. Kisha tunakufa …

“Na katika kifo tungebaki isipokuwa kwa ajili ya Mtu Mmoja na Kazi yake, hata Yesu wa Nazareti …

“Kwa roho yangu yote na dhati ya nafsi yangu, napaza sauti yangu katika ushuhuda kama shahidi maalum na kutangaza kuwa Mungu yu hai. Yesu Kristo ni mwanawe, Mwana wa Pekee wa Baba katika Mwili. Yeye ni Mwokozi wetu, Yeye ni Mwombezi kwa Baba. Ni yeye aliyekufa msalabani ili kupatanisha kwa ajili ya dhambi zetu. Alikuwa matunda ya kwanza ya Ufufuo Kwa sababu alikufa, wote wataishi tena.”5

Ushuhuda wa kibinafsi

“Ninatangaza ushuhuda wangu wa kibinafsi kwamba kifo kimeshindwa, Ushindi juu ya kaburi umepatikana Hebu, na maneno yaliyotakaswa Naye aliyeyatimiza kuwa ya elimu ya kweli kwa wote. Yakumbuke Yathamini Yaheshimu Amefufuka.6

Muhtasari

  1. “Amefufuka,” Liahona, Apr. 2003, 7.

  2. “Katika Kuachana,” Liahona, May 2011, 114.

  3. “Sasa Ndio Wakati,” Liahona, Jan. 2002, 68; Ona pia Yohana11:25–26; 14:27.

  4. “Amefufuka,” Liahona, Mei 2010, 89, 90; ona pia Ayubu 14:14; Mathayo 28:6.

  5. “ Najua Mkombozi Wangu yu Hai!” Liahona, Mei 2007, 24, 25.

  6. Liahona, Apr. 2003, 7.

Kufundisha kutoka kwa Ujumbe huu

Baada ya kushiriki dondoo kutoka kwa ujumbe wa Rais Monson, kumbuka ushuhuda anaotoa kuhusu maana ya kweli ya Pasaka. Unaweza kuwauliza wanafamilia maswali haya: “Inamaanisha nini kwamba Nabii aliye hai ameyashuhudia mambo haya hivi leo?” Unawezaje kuutumia katika maisha yako? Fikiria kuongeza ushuhuda wako.

Chapisha