Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Aprili 2012
Penda, Uchunge na Uimarishe
Soma kifaa hiki, na kama ifaavyo, ukijadili pamoja na kina dada unaowatembelea. Tumia maswali ili kukusaidia kuwaimarisha dada zako na kuufanya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kuwa sehemu hai ya maisha yako mwenyewe.
Kama Mwokozi, waalimu watembelezi huhudumia mmoja kwa mmoja (ona 3 Nefi 11:15). Tunajua tumefaulu katika huduma yetu kama waalimu watembelezi wakati akina dada zetu wanaweza kusema,: (1) Mwalimu wangu mtembelezi ananisaidia kukua kiroho (2) Ninajua kuwa mwalimu wangu mtembelezi ananijali sana, mimi na familia yangu; na (3) nikiwa na shida ninajua mwalimu wangu mtembelezi atachukua hatua bila kuulizwa.1
Tunawezaje kama waalimu watembelezi kumpenda, kumchunga na kumuimarisha dada? Mapendekezo haya tisa yanayopatikana katika sura ya 7 ya Daughters in My Kingdom: The History and Work of Relief Society ni ya kuwasaidia waalimu watembelezi kuwahudumia akina dada zao:
-
Omba kila siku kwa ajili yake na familia yake.
-
Tafuta msukumo kumjua na familia yake.
-
Mtembelee mara kwa mara ili kujua anavyoendelea na kumfariji na kumwimarisha.
-
Kuwa mawasiliano ya mara kwa mara kupitia matembezi, simu, barua, barua pepe, ujumbe mfupi, na matendo ya kawaida ya wema.
-
Msalimie katika mikutano ya Kanisa.
-
Msaidie akiwa na dharura, ugonjwa au mahitaji mengine ya dharura.
-
Mfundishe maandiko na Jumbe za Ualimu Tembelezi.
-
Mpatie Msukumo kwa kuwa mfano mwema.
-
Fahamisha kiongozi wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kuhusu huduma yako na wema wa kiroho na kimwili ya dada yule.
Kutoka kwa Maandiko
Kutoka kwa Historia Yetu
Ualimu tembelezi umekuwa njia ya akina mama Watakatifu wa Siku za Mwisho kupenda, kulea na kuhudumia—kutenda kulingana na zile huruma ambazo Mungu amepanda mioyoni [mwetu],’ kama Joseph Smith alivyofundisha.”2
Dada ambaye hivi karibuni amekuwa mjane alisema kuhusu waalimu watembelezi: “Walisikiliza. Walinifariji. Walilia nami. Na walinikumbatia. … [Wao] walinisaidia kutoka kwenye dhiki kuu na mateso ya miezi ya kwanza ya upweke.”3
Usaidizi kwa kazi za wakati pia ni njia ya kuhudumu. Katika mkutano mkuu wa Oktoba 1856, Rais Brigham Young alitangaza kuwa Watangulizi wa mikokoteni walikuwa wamekwama katika barafu nzito umbali wa maili 270–370 (435–595 km). Alitoa mwito kwa Watakatifu wa Siku za Mwisho waliokuwa Salt Lake kuwaokoa na “kushughulikia sana ya mambo tunayoita ya muda.”4
Lucy Meserve Smith alirekodi kuwa wanawake walivua sketi zao za ndani na soksi ndefu pale katika tabenakulo na kuyarundika katika mabehewa na kuyatuma kwa watangulizi waliokuwa wanakufa baridi. Kisha wakakusanya malazi na nguo kwa wale hatimaye wangekuja na mali kidogo. Wakati kampuni za mikokoteni zilipofika, jumba moja mjini lilikuwa limejaa bidhaa kwa ajili yao.5
© 2012 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa Imechapishwa USA Kiingereza kiliidhinishwa: 6/11. Tafsiri iliidhinishwa: 6/11. Tafsiri ya Visiting Teaching Message, April 2012. Swahili. 10364 743