Vijana
Asante kwa Mwalimu Wangu wa Shule ya Jumapili
Shule yangu ya Jumapili si shwari wakati wote. Napendelea kusikiliza somo kila wiki, lakini wakati mwingine linaonekana kama wengine kwenye darasa langu hawakuwa wanasikiliza. Mara nyingi wanazungumza au wanacheza michezo ya vyombo vya eletroniki wakati mwalimu wetu anapojaribu kutufunza. Cha kuhuzunisha, mara nyingine najipata nikiwa sehemu ya hii shida.
Wiki moja tulikuwa wabaya kuzidi kawaida, na mwishoni wa darasa, mwalimu wetu alibakia kudondokwa na machozi kwa sababu hakuna mtu aliyekuwa anasikiliza somo lake. Tulipokuwa tunaondoka darasani, nilihisi vibaya kwa sababu yake.
Jumapili iliyofuata mwalimu wetu alieleza kwamba alikuwa ameomba sana wiki hiyo, akitafuta maelekezo, na ikamjia kwake kwamba alihitaji kutuonyesha filamu ya Kanisa. Yeye akaanzisha sinema, ambayo ilikuwa juu ya maisha ya Yesu Kristo na miujiza aliyotenda.
Nilipofikira kuhusu hiyo filamu jioni hiyo, nilihisi kitu tofauti. Ghafla niligundua kwamba nilikuwa nikihisi Roho, zaidi sana kuliko nilivyosikia awali. Mara nikaamua kwamba nilikuwa nataka kubadilisha maisha yangu ili kuwa zaidi kama Mwokozi, na niligundua uzoefu katika Shule ya Jumapili siku ile ulikuwa umeimarisha pa kubwa ushuhuda wangu. Ninashukuru sana kwa Mwalimu wangu wa Shule ya Jumapili na kila kitu anachofanya kwa darasa letu kila wiki.