Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Juni 2012
Ualimu Tembelezi—Kazi Takatifu
Soma kifaa hiki, na kama ifaavyo, ukijadili pamoja na kina dada unaowatembelea. Tumia maswali ili kukusaidia kuwaimarisha dada zako na kuufanya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kuwa sehemu hai ya maisha yako mwenyewe.
Kama waalimu tembelezi, tuna misheni muhimu ya kiroho ya kutimiza. “Askofu, ambaye ndiye mchungaji aliyetawazwa wa kata, hawezi kuchunga kondoo wa Bwana wote katika wakati mmoja. Yeye anategemea waalimu tembelezi wenye maongozi kumsaidia yeye.”1 Kutafuta na kupokea ufunuo wa nani atakaye patiwa wajibu wa kutunza kila dada ni muhimu.
Maongozi yanaanza washiriki wa urais wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama wanapojadiliana kwa maombi juu ya mahitaji ya watu binafsi na familia. Kisha, kwa idhini ya askofu, urais wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama hugawa kazi kwa njia ambayo itasaidia kina dada kuelewa kwamba ualimu tembelezi ni jukumu muhimu la kiroho.2
Waalimu watembelezi kwa uaminifu wapata kumjua na kumpenda kila dada, kumsaidia yeye kuimarisha imani yake, kutoa huduma wakati inapohitajika. Wanatafuta maongozi ya kibinafsi kujua jinsi ya kutenda kwa mahitaji ya kiroho na muda ya kila dada wanayemtembelea.3
“Ualimu tembelezi unakuwa kazi ya Bwana tunapolenga watu badala ya asilimia. Kwa kweli, ualimu tembelezi hauwezi kumalizika kamwe. Zaidi ni njia ya maisha badala ya shughuli.”4
Kutoka kwa Maandiko
Kutoka kwa Historia Yetu
Eliza R. Snow, rais mkuu wa pili wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama alifunza, “Naichukulia ofisi ya mwalimu kuwa ofisi kuu na takatifu.” Yeye aliwashauri waalimu tembelezi “wajazwe na Roho wa Mungu, na hekima, na unyenyekevu, na upendo” kabla ya kuwatembelea watu ili waweze kutathimini na kikidhi mahitaji ya kiroho pamoja na muda. Yeye alisema, “Unaweza kuhisi kuzungumza maneno ya amani na faraja, na kama unampata dada akihisi baridi, mchukue hata kwenye moyo wako kama unavyomfanya mtoto kifuani mwako na kumchangamsha [yeye].”5
Tunapoenenda mbele katika imani kama vile kina dada wa awali wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, tutakuwa na Roho Mtakatifu kuwa nasi na tutapata maongozi ya kujua jinsi ya kumsaidia kila dada tunayemtembelea. “Acha [sisi] tutafute hekima badala ya uwezo,” alisema Dada Snow, “na [sisi] tutakuwa na uwezo wote [sisi] tutakuwa na hekima ya kutenda.”6
© 2012 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Imechapishwa USA. Kiingereza kiliidhinishwa: 6/11. Tafsiri iliidhinishwa: 6/11. Tafsiri ya Visiting Teaching Message, June 2012. Swahili. 10366 743