2012
Mwito wa Mwokozi wa Kuhudumu
Agosti 2012


Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Agosti 2012

Mwito wa Mwokozi wa Kuhudumu

Rais Thomas S. Monson.

Wote ambao wamesomea hesabu wanajua maana nambari asili. Kwa Watakatifu wa Siku za Mwisho, kuna nambari asili inayotuunganisha pamoja. Hio nambari asili ni mwito wa binafsi ambao kila mmoja wetu anapokea ili kutekeleza majukumu katika ufalme wa Mungu hapa duniani.

Je, umewahi kuwa na kosa la kunung’unika wakati mwito unapokujia? Ama unakubali kwa shukrani kila fursa ya kutumikia ndugu na dada zako, ukijua kwamba Baba yetu wa Mbinguni atawabariki wale ambao amewaita?

Ningetarajia kwamba hatungepoteza lengo halisi la fursa zetu zenye thamani za kuhudumu. Lengo hilo, lengo hilo la milele, ni lile lililoongelewa na Bwana na linapatikana katika Lulu ya Thamani Kuu: “Kwa maana tazama, hii ndiyo kazi yangu na utukufu—kuleta kutokufa na uzima wa milele wa mwanadamu.”1

Tuweze kukumbuka milele kwamba joho la ushiriki katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho sio pazia ya faraja bali vazi la majukumu. Jukumu letu, kwa kuongezea ya kujiokoa wenyewe, ni kuwaelekeza wengine kwa ufalme wa selestia wa Mungu.

Kwa kutembea kwa upendeleo kwenye njia ya huduma ielekeayo kwa Mungu, hatutawahi kuwa katika hali ya Kadinali Wolsey wa Shakespeare. Akiwa amenyang’anywa uwezo wake baada ya miaka ya huduma kwa mfalme wake, alilia kwa huzuni:

Laiti ningemtumikia Mungu wangu kwa nusu ya ari

Nilimtumikia mfalme wangu, Hangeweza katika umri wangu

Kaniacha mimi uchi kwa maadui wangu.2

Ni aina gani ya huduma inayohitajika mbinguni? “Bwana anahitaji moyo na akili yenye kukubali; na wenye kukubali na kutii watakula mema ya Sayuni katika siku za mwisho.”3

Mimi hutua kwa muda ninapofikiria juu ya maneno ya Rais John Taylor (1808–87): “Ikiwa haujakuza miito yako, Mungu atakuweka kuwajibikia wale ambao ungewaokoa kama ungefanya jukumu lako.”4

Kama vile kurunzi inayong’ara ya wema ndivyo maisha ya Yesu alipohudumu miongoni mwa watu. “Mimi kati yenu ni kama atumikaye,”5 Yesu alitangaza alipoweka nguvu kwa miguu ya mlemavu, kuona kwa macho ya kipofu, kusikia kwa masikio ya kiziwi, na maisha kwa mwili ya wafu.

Kwa fumbo la Msamaria mwema, Bwana alitufundisha kupenda majirani zetu kama sisi wenyewe.6 Kwa jibu lake kwa mwana sheria tajiri, Alitufundisha kutupilia mbali uchoyo.7 Kwa kulisha watu 5000, Alitufundisha kuona mahitaji ya wengine.8 Na kwa Mahubiri Mlimani, Alitufundisha kutafuta kwanza ufalme wa Mungu.9

Katika Ulimwengu Mpya, Bwana aliyefufuka alitangaza, “Mnajua vitu ambavyo mnahitajika kufanya katika Kanisa langu, kwani vitendo mmeniona nikifanya, hivyo pia mtafanya; kwani yale ambayo mmeniona nikifanya hata hivyo nyinyi mtafanya.”10

Tunawabariki wengine tunapohudumu katika kivuli cha “Yesu wa Nazareti … akazunguka huko na huko akitenda kazi njema.”11 Mungu tubariki ili tupate furaha katika kumtumikia Baba yetu aliye Mbunguni tunapowatumikia watoto Wake duniani.

Kufundisha kutoka kwa Ujumbe huu

“[Bwana] hataturuhusu kushindwa ikiwa tutatekeleza upande wetu. Atatukuza hata zaidi ya talanta na uwezo wetu. … Ni mojawapo wa uzoefu wa kupendeza unaoweza kuja kwa mwanadamu” (Ezra Taft Benson, katika Teaching, No Greater Call [1999], 20). Fikiria kushirikisha uzoefu wakati wewe au mtu unayemjua amehisi Bwana akikuza talanta na uwezo wake. Alika familia kushirikisha baadhi ya uzoefu wao mzuri walipoitika kwa “mwito wa Mwokozi wa kuhudumu.”