Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Agosti 2012
Kuchukua Hatua Wakati wa Haja
Soma kifaa hiki kwa maombi na kama ifaavyo, ukijadili pamoja na kina dada unaowatembelea. Tumia maswali ili kukusaidia kuwaimarisha dada zako na kuufanya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kuwa sehemu hai ya maisha yako mwenyewe.
Kama waalimu watembelezi, mojawapo wa dhamira zetu ni kusaidia kuimarisha familia na nyumba. Kina dada tunaowatembelea wanapaswa kuweza kusema, “Ikiwa nina shida, ninajua waalimu wangu watembelezi watasaidia bila kugojea kuulizwa.” Ili kuweza kuhudumu, tuna jukumu la kujua mahitaji ya kina dada tunaowatembelea. Tunapotafuta mwongozo, tutajua jinsi ya kushughulikia mahitaji ya kiroho na kimwili ya kila dada tulioteuliwa kutembelea. Kisha, kutumia muda wetu, ujuzi, vipawa, maombi ya imani, na usaidizi wa kiroho na hisia, tunaweza kusaidia kupeana huduma ya upendo wakati ugonjwa, kifo, na hali nyingine maalum.1
Kupitia kwa usaidizi wa ripoti kutoka kwa waalimu watembelezi, urais wa Muungano wa Usaidizi wa kina Mama hutambua wale walio na mahitaji maalum kwa sababu ya ugonjwa wa kimwili au kihisia, dharura, uzazi, ulemavu, ukiwa, au changamoto zingine. Rais wa Muungano wa Usaidizi wa kina Mama kisha anaripoti matokeo yake kwa askofu. Chini ya uongozi wake, yeye hupanga usaidizi.2
Kama waalimu watembelezi tunaweza kuwa na “sababu kiasi gani… ya kutufanya tufurahi” kwa sababu ya “baraka ambayo tumeteremshiwa, kwamba tumetengenezwa kuwa vyombo mikononi mwa Mungu kuimarisha kazi hii kubwa” (Alma 26:1, 3).
Kutoka kwa Maandiko
Mathayo 22:37–40; Luka 10:29–37; Alma 26:1–4; Mafundisho na Maagano 82:18–19
Kutoka kwa Historia Yetu
Katika miaka ya zamani ya Kanisa, ushiriki ulikuwa mdogo na kwenye eneo moja. Washiriki wangeitika haraka wakati mtu alikuwa na shida. Leo ushiriki wetu ni zaidi ya millioni 14 na umetapakaa kote ulimwenguni. Mafundisho ya Utembelezi ni sehemu ya mpango wa Bwana wa kupeana usaidizi kwa watoto Wake wote.
“Mpango pekee unaoweza kupeana usaidizi na faraja kwa Kanisa nzima kubwa hivi katika ulimwengu wenye mchanganyiko inaweza kuwa ni kupitia kwa watumishi binafsi walio karibu na watu wenye shida,” alisema Rais Henry B. Eyring, Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza.
“… Kila askofu na kila rais wa tawi ana rais wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama wa kutegemea,” aliendelea. “Anao waalimu watembelezi, wanaojua majaribu na shida za kila dada. Anaweza, kupitia wao, kujua mioyo ya watu binafsi na familia. Anaweza kutimiza mahitaji na kusaidia askofu katika mwito wake wa kuelimisha watu binafsi na familia.”3
© 2012 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Imechapishwa USA. Kiingereza kiliidhinishwa: 6/11. Tafsiri iliidhinishwa: 6/11. Tafsiri ya Visiting Teaching Message, August 2012. Swahili.10368 743