2013
Utiifu Huleta Baraka
Mei 2013


Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Mei 2013

Utiifu Huleta Baraka

Elimu ya ukweli na majibu ya maswali makuu huja kwetu tunapokuwa watiifu kwa amri za Mungu.

Ndugu na dada zangu wapendwa, nina shukrani jinsi gani kuwa pamoja nanyi asubuhi hii. Nawaomba imani na maombi yenu ninapojibu fursa ya kuwahutubia ninyi.

Katika nyakati zote, wanaume na wanawake wametafuta elimu na uelewa kuhusu kuweko kwa maisha ya duniani haya na nafasi zao na madhumuni yaliyopo ndani yake pamoja na njia ya amani na furaha. Kutafuta kama huku kunafanywa na kila mmoja wetu.

Elimu na uelewa unapatikana kwa wanadamu wote. Unapatikana katika kweli ambazo ni za milele. Katika Mafaundisho na Maagano , sehemu ya 1, mstari wa 39, tunasoma: Kwani tazama, na lo, Bwana ni Mungu, na Roho hushuhudia, na ushuhuda wake ni wa kweli, na ukweli hudumu milele na milele”

Mtunga shairi aliandika:

Ingawaje mbingu zinaondoka na chemichemi za dunia zinapasuka,

Ukweli, maana ya maisha, utastahimili ugumu wote,

Milele, usiobadilika, daima.1

Baadhi wanaweza kuuliza, “Ukweli kama huu unapatikana wapi, na tunaweza kuutambua vipi?” Katika ufunuo uliotolewa kupitia kwa Nabii Joseph Smith huko Kirtland, Ohio, mnamo Mei mwaka wa 1833, Bwana alitangaza:

“Ukweli ni maarifa ya mambo kama yalivyo, na kama yalivyokuwa, na kama yatakavyokuwa. …

“Roho wa ukweli ni wa Mungu. …

“ Na hakuna mtu apokeyae utimilifu isipokuwa amezishika amri zake.

“Yule azishikaye amri zake hupokea kweli na nuru, hadi ametukuzwa katika kweli na kujua mambo yote.”2

Ni ahadi tukufu jinsi gani! “Yule azishikaye amri zake hupokea kweli na nuru, hadi ametukuzwa katika kweli na kujua mambo yote.”

Hakuna haja kwako au kwangu katika miaka hii ya ujuzi, wakati ujalivu wa injili umerejeshwa, kusafiri kwenye bahari geni au kusafiri kwenye barabara isiotumiwa katika utafutaji wa chemichemi ya ukweli. Kwa kuwa Baba mpendwa wa Mbinguni ametengeneza njia yetu na kupeana ramani halisi—utiifu. Elimu ya ukweli na majibu ya maswali makuu huja kwetu tunapokuwa watiifu kwa amri za Mungu.

Tunajifunza utiifu kote maishani mwetu. Kuanzia tunapokuwa wadogo sana, wale walio na jukumu la kutunza huweka miongozo na sheria za kuhakikisha usalama wetu. Maisha yangekuwa rahisi kwetu sote kama tungetii sheria kama hizo kwa ukamilifu. Wengi wetu, hata hivyo, wanajifunza kupitia matokeo hekima ya kuwa mtiifu.

Nilipokuwa nikikua, kila majira ya joto kutoka mapema Julai hadi mapema Septemba, familia yetu ilikwenda kwenye nyumba ya mbao huko Vivian Park katika Provo Canyon katika Utah.

Mojawapo wa marafiki zangu wa dhati siku hizo za uhuru mwingi katika korongo alikuwa Danny Larsen, ambaye familia yake pia ilikuwa na nyumba ya mbao huko Vivian Park. Kila mara yeye nami tulizurura katika hii paradiso ya mvulana, tukivua samaki katika kijito na mto, tukikusanya mawe na vitu vingine vya thamani, tukitembea, na kukwea, na basi tukifurahia kila dakika ya kila saa ya kila siku.

Asubuhi moja Danny nami tuliamnua tunataka kuwa na kambi moto jioni hio pamoja na marafiki zetu wote wa korongoni. Tulihitaji kufweka eneo katika uwanda ulio karibu ambapo sisi sote tungekusanyika. Manyasi ya Juni ambayo yalizangaa kote uwandani yalikuwa yamekauka na kuwa yanachomachoma, kufanya uwanda usifae kwa madhumuni yetu. Tulianza kukata nyasi zile ndefu, tukudhamiria kufweka sehemu kubwa ya duara. Tulivuta na kung’oa kwa nguvu zetu zote, lakini tungeweza kuondosha magugu kidogo sana. Tulijua kazi hii ingechukua siku nzima, na tayari nguvu zetu na ari yetu ilikuwa inafifia.

Na basi kile nilifikiria kuwa suluisho zuri likaja kwa akili ya mwenye umri wa miaka minane. Nilimwambia Danny, “Kile tunachohitaji ni kuchoma haya magugu kwa moto. Sisi tutachoma duara katika magugu!” Yeye alikubali mara moja, na mimi nilikimbia nyumbani kuchukua viberiti vichache.

Na yeyote hasifiri kwamba katika umri wangu wa miaka minane tuliruhusiwa kutumia viberiti, Ninataka kusema wazi kwamba sote Danny nami hatukuruhusiwa kuvitumia bila usimamizi wa mtu mzima. Sote tulikuwa tumeonywa mara nyingi kuhusu hatari ya moto. Hata hivyo, nilijua pale familia yangu ilikuwa inaweka viberiti, na tulikuwa tunataka kutengeneza uwanda huu. Bila kufikiria tena, nilikimbia nyumbani kwetu na kuchukua viberiti vichache, nikihakikisha hakuna mtu anayeniona. Nikavificha upesi katika moja kati ya mifuko yangu.

Nikakimbia kwa Danny, nikiwa mchangamfu kwamba mfukoni mwangu nilikuwa na suluisho la shida yetu. Nakumbuka nikifikiria kwamba moto ungechoma tu vile tulivyotaka na kisha kwa namna fulani kimiujiza ungejizima.

Nikawasha kiberiti kwenye mwamba na kuwasha manyasi ya Juni. Yalichomeka kama vile yalikuwa yamemwagiwa petroli. Hapo mwanzoni Danny nami tulifurahia sana tulipokuwa tunatazama magugu yakichomeka, lakini punde ikaonekana kwamba hautazima peke yake. Tukaingia wasi wasi tulipogundua hakuna chochote tungefanya kuuzima. Miale mikali ilianza kufuata nyasi mwitu juu pande za milimani, kuhatarisha miti ya misonobari na kila kitu njiani mwake.

Mwishowe hatukuwa na budi bali tu kukimbilia msaada. Punde wanaume na wanawake walioweza kupatikana huko Vivian Park wakaja mbio, kwenda na kurudi wakiwa na mfuko ya turubai iliyolowa wakipiga miale katika kujaribu kuizima. Baada ya masaa kadhaa miale ya mwisho iliyobakia ikazimwa. Miti ya misonobari ya miaka mingi ikaokolewa, vile vile nyumba ambazo miale ingefikia hatimaye.

Danny nami tulijifunza masomo magumu kadhaa lakini muhimu siku hio—sehemu kuu ambayo ilikuwa umuhimu wa utiifu.

Kuna sheria na amri za kutusaidia kuhakikisha usalama wetu. Vile vile, Bwana amepatiana miongozo na amri za kuhakikisha usalama wetu wa kiroho ili kwamba tuweze kusafiri kwa ufanisi katika maisha ya muda haya hatari na hatimaye kurudi kwa Baba yetu wa Mbinguni.

Karne zilizopita, kwa kizazi kilichozingatia kwa dhati utamaduni wa dhabihu ya mnyama, Samueli alitangaza kwa uthabiti, “Kutii ni bora kuliko dhabihu, na kusikia kuliko mafuta ya beberu.”3

Katika kipindi hiki, Bwana alifunua kwa Nabii Joseph Smith kwamba Yeye huhitaji “moyo na akili yenye kukubali, na wenye kukubali na kutii watakula mema ya Sayuni katika siku za mwisho.”4

Manabii wote, wa kale na wa kisasa, wanajua kwamba kutii ni muhimu kwa wokovu wetu. Nefi alitangaza, “Nitaenda na kutenda vitu ambavyo Bwana ameamuru”5 Inagawa wengine walipepesuka katika imani yao na utiifu wao, kamwe hata mara moja Nefi hakushindwa kufanya kile Bwana alitaka kutoka kwake. Vizazi visivyo na hesabu vimebarikiwa kama matokeo yake.

Tukio la kusisimua nafsi la utiifu ni lile la Ibrahimu na Isaka. Lazima ilikuwa uchungu na vigumu jinsi gani kwa Ibrahimu, katika utiifu kwa amri ya Mungu, kumtwaa mpendwa wake Isaka katika nchi ya Moria ili kumtoa yeye kama dhabihu. Je! Unaweza kufikiria uzito wa moyo wa Ibrahimu alipokuwa anasafiri hadi sehemu iliyopangwa? Hakika uchungu lazima ulikuwa umevunjavunja mwili wake na kutesa akili yake alipomfunga Isaka, na kumweka yeye kwenye altari, na kutwaa kisu ili kumchinja. Kwa imani isiyotingika na kumwamini Bwana, yeye alijibu amri ya Bwana. Ilikuwa ni utukufu jinsi gani matangazo haya, na kwa mshangao wa makaribisho yaliyokuja. “Usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno; kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, iwapo hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee.”6

Ibrahimu alikuwa amejaribiwa na kupatwa na majaribu, na kwa imani yake na utiifu wake Bwana alimpatia yeye hii ahadi tukufu: “Katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.”7

Ingawa sisi hatujaulizwa kuthibitisha utiifu wetu katika njia ya kidrama na njia ya kuchoma moyo sana, utiifu unahitajika kutoka kwetu pia.

Rais Joseph F. Smith katika Oktoba 1873 alitangaza, “Utiifu ndio sheria ya kwanza ya mbinguni.”8

Rais Gordon B. Hinckley alisema, “Furaha ya Watakatifu wa Siku za Mwisho, amani ya Watakatifu wa Siku za Mwisho, maendeleo ya Watakatifu wa Siku za Mwisho, ufanisi wa Watakatifu wa Siku za Mwisho, na wokovu wa milele na kuinuliwa kwa watu hawa kunategemea katika kutembea katika utiifu kwa ushauri wa … Mungu.”9

Utiifu ni silika ya manabii; umewapatia nguvu na elimu wao kote katika vipindi vyote. Ni muhimu kwetu kutambua kwamba sisi, tuna haki ya hii nyenzo ya nguvu na elimu. Inapatikana kwa urahisi kwetu siku hizi tunapotii amri za Mungu.

Miaka yote mimi nimejua watu wasiohesabika ambao wamekuwa waaminifu hasa na watiifu. Nimebarikiwa na kupata motisha kutoka kwao. Acha nishiriki nanyi tukio la watu kama hao wawili.

Walter Krause alikuwa mshiriki thabiti wa Kanisa ambaye, pamoja na familia yake, waliishi katika ile ilijulikana kama Ujerumani Mashariki kufuatia Vita vya Dunia vya Pili. Licha ya ungumu aliokabiliana nao kwa sababu ya kukosa uhuru katika sehemu hio ya ulimwengu wakati huo, Ndugu Krause alikuwa mtu aliyempenda na kutumikia Bwana. Yeye kwa uaminifu na uthabiti alifanya kila kazi aliyopatiwa.

Mtu mwengine ni Johann Denndorfer, wenyeji wa Hungaria, aliyeongolewa katika Kanisa katika Ujerumani na kubatizwa huko mnamo mwaka wa 1911 akiwa umri wa miaka 17. Punde alirudi Hungaria. Kufuata Vita vya Dunia vya Pili, yeye alijipata mateka katika nchi yake ya asili, katika mji wa Debrecen. Uhuru ulikuwa umeondolewa kutoka kwa watu Hungaria.

Ndugu Walter Krause, ambaye hakuwa anamjua Ndugu Denndorfer, alipokea kazi ya kuwa mwalimu wa nyumbani na kumtembelea yeye kila wakati. Ndugu Krause alimuita mwenzi wake wa ualimu wa nyumbani na kumwambia, “Sisi tumepokea kazi ya kumtembelea Ndugu Johann Denndorfer. Je! Utakuwa na nafasi ya kwenda pamoja nami wiki hii kumuona na kumpatia ujumbe wa injili?” Na kisha akaongezea “Ndugu Denndorfer anaiishi katika Hungaria.”

Mwenzi aliyeshituka alisema, “Tutaondoka lini?

“Kesho,” jibu likaja kutoka kwa Ndugu Krause.

“Tutarudi nyumbani lini?” mwenzi wake akauliza.

Ndugu Krause akajibu, “Ee, katika wiki—kama sisi tutarudi.”

Wale walimu wa nyumbani wawili wakaondoka kumtembelea Ndugu Denndorfer, wakisafiri kwa gari la moshi na basi kutoka eneo la kasikazini mashariki mwa Ujerumani hadi Debrecen, Hungaria—safari ndefu. Ndugu Denndorfer alikuwa hajapata walimu wa nyumbani tangu vita vianze. Sasa, alipowaona hawa watumishi wa Bwana, yeye alizidiwa na shukrani kwamba wamekuja. Hapo mwanzo alikataa kuwasalimia wao kwa mikono. Badala yake, yeye alienda katika chumba chake cha kulala na kuchukua kutoka kwa kabati ndogo kijisaduku kidogo kilichokuwa na fungu la kumi lake ambalo alikuwa ameifadhi kwa miaka mingi. Aliwasilisha fungu la kumi kwa walimu wake na kusema, “Mimi sasa niko sawa mbele za Bwana. Sasa ninahisi mstahiki kusalimiana kwa mikono ya watumishi wa Bwana!” Ndugu Krause aliniambia baadaye kwamba aliguswa kushinda maneno yanavyoweza kuelezea kufikiria kwamba huyu ndugu mwaminifu, ambaye hakuwa anakutana na yeyote wa Kanisa kwa miaka mingi, alikuwa mtiifu na kwa uthabiti alichukua kutoka kwa mapato yake duni asilimia 10 pamoja ambayo kwayo alilipa fungu la kumi. Yeye alikuwa amelihifadhi bila kujua ni lini au kama angepata nafasi ya kuilipa.

Ndugu Walter Krause aliaga dunia miaka tisa iliyopita katika umri wa miaka 94. Yeye alihudumu kwa uaminifu na utiifu maishani mwake mwote na alikuwa mfano mzuri kwangu na kwa wote waliomjua yeye. Alipoulizwa kutimiza kazi, kamwe hauliza, kamwe hakunung’unika, kamwe hakutoa visababu.

Ndugu na dada zangu, jaribio kuu la maisha haya ni utiifu. “Nasi tutawajaribu kwa njia hii, ili kuona kama wao watafanya mambo yote yale ambayo Bwana Mungu wao atawaamuru.”10

Mwokozi alitangaza: “Kwani wote watakaopata baraka mikononi mwangu wataitii sheria iliyowekwa kwa ajili ya baraka hiyo, na masharti yake, kama yalivyowekwa tangu kabla ya kuwekwa kwa misingi ya ulimwengu.”11

Hamna mfano mkuu wa utiifu uliopo kushinda ule wa Mwokozi wetu. Juu Yake Paulo alisema:

“Na, ingawa ni Mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompata;

“Naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii.”12

Mwokozi alionyesha upendo halisi wa Mungu kwa kuishi maisha makamilifu, kwa kuheshimu misheni yake takatifu ambayo ilikuwa ni Yake. Kamwe Yeye hakuwa na kiburi. Kamwe hakujifurisha kwa kiburi. Kamwe Yeye hakukosa kuwa mwaminifu. Daima alikuwa mnyenyekevu. Daima Yeye alikuwa mwaminifu. Daima Yeye alikuwa mtiifu.

Ingawa alijaribiwa na bwana wa undangayifu, hata ibilisi; ingawa Yeye alikuwa mdhaifu kwa ajili kufunga kwa siku 40 mchana na usiku na kuwa na njaa, hali wakati yule muovu alimpatia Yesu mapendekezo ya kuvutia na ya kutamanisha, Yeye alitupatia mfano mtakatifu wa utiifu kwa kukataa kuondoka kutoka kwa kile Yeye alijua kilikuwa sahihi.13

Alipokabiliwa na maumivu makuu ya Gethsemane, ambako alivumilia uchungu kiasi kwamba jasho Lake lilikuwa kama matone makubwa ya damu yakianguka chini kwenye ardhi,”14 Alionyesha mfano wa Mwana mtiifu kwa kusema, “Ee, Baba, ikiwa ni mapenzi Yako, uniondolee kikombe hiki: walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke.”15

Kama Mwokozi alivyowaelekeza Mitume Wake wake wa mapema, kwa hivyo Yeye hutuelekeza wewe na mimi: “Wewe nifuate mimi.”1614 Je! tuko tayari kutii?

Elimu ambayo sisi tunatafuta, majibu ambayo sisi tunatafuta, na nguvu ambazo tunatamani leo ni kukabiliana changamoto za ulimwengu changamani na unaobadilika unaweza kuwa wetu ambao tunaokuwa tayari kutii amri za Bwana. Mimi nitanukuu mara ingine tena maneno ya Bwana: “Yule azishikaye amri [za Mungu] hupokea kweli na nuru, hadi ametukuzwa katika kweli na kujua mambo yote.”17

Ni maombi yangu ya unyenyekevu kwamba sisi tutabarikiwa kwa zawadi kuu zilizoahidiwa kwa watiifu. Katika jina la Yesu Kristo, Bwana na Mwokozi wetu, amina.

Chapisha