Vijana
Kuongozwa kwa Imani
Mwandishi anaishi Kaskazini mwa Carolina, USA
Sitawahi kamwe kusahau kutembea viwanja vya Winter Quarters, Nebraska, USA, ambapo waanzilishi waliishi miaka ya kale. Kiwanja kilihisiwa kuwa kitakatifu, karibu kama nilikuwa nikitembelea hekalu la nje.
Macho yangu yakijawa na machozi, kutia ukungu kuona kwangu yangu. Niliona sanamu lakini sikuweza kutambua mwili. Nilipopangusa machozi yangu, niliona mwanamke na mwanaume ambao nyuso zao zilijawa na huzuni. Nilivyozidi kuangalia kwa karibu, niliona mwili wa yule mtoto mchanga imelazwa katika kaburi kwenye miguu yao.
Matendo haya yalinijaza na hisia nyingi: huzuni, hasira, shukrani, na furaha. Nilitaka kuondoa maumivu ambayo wale Watakatifu waliona, lakini wakati huo huo nilikuwa na shukrani kwa kile walichojitolea kwa ajili ya injili.
Uzoefu wangu katika Winter Quarters umenisaidia kutambua kwamba Baba wa Mbinguni anatoa Injili kwa watoto wake na anawapa wakala kuitumia jinsi watakavyo. Wazazi wa mtoto yule angelichagua kufuata njia rahisi. Kufuata nabii na kuishi injili iliwabidi waanzilishi hawa kusonga mbele hata kama ilimaanisha kuzika mtoto wao. Lakini walichagua kuweka injili katika maisha yao na kukubali changamoto zao. Nilijifunza kwamba kujitolea kwa Watakatifu kwa injili na uamuzi wao wa kusonga mbele ulisukumwa kwa imani na matumaini—matumaini ya maisha ya baadaye na imani kwamba Bwana aliwajua na angeweza kupunguza maumivu yao.