Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Julai 2013
Kufundishia na Kujifunzia Injili
Soma nyenzo hii kwa maombi na kama ifaavyo, ukijadili pamoja na kina dada unaowatembelea. Tumia maswali ili kukusaidia kuwaimarisha dada zako na kuufanya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kuwa sehemu hai ya maisha yako mwenyewe. Kwa taarifa zaidi, nenda kwenye www.reliefsociety.lds.org.
Yesu Kristo alikuwa mwalimu bora. Aliweka mfano kwetu sisi wakati “alipofundisha wanawake katika makundi ya watu na kama watu binafsi, katika barabara na ufukoni, katika kisima na katika makazi yao. Alionyesha fadhili mbele yao na kuwaponya na familia zao.”1
Aliwafundisha Martha na Maria na “kuwaalika wao kuwa wafuasi wake na kushiriki wokovu, ‘kile kilicho bora’ [Luka 10:42] ambayo kamwe haitaondolewa kutoka kwao.”2
Katika maandiko yetu ya siku za mwisho, Bwana alituamuru “kufundishana mafundisho ya ufalme” (M&M 88:77). Kuhusiana na kufundisha na kujifunza mafundisho, Cheryl A. Esplin, mshauri wa pili katika urais mkuu wa Msingi, alisema, “Kujifunza ili kuelewa kikamilifu mafundisho ya injili ni mchakato wa maisha na inakuja ‘mstari juu ya mstari, amri juu ya amri, hapa kidogo na pale kidogo’ (2 Nefi 28:30).”3
Tunapojifunza, kusoma, na kuomba, tutajifunza kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, ambaye hupeleka ujumbe wetu “katika mioyo ya watoto wa watu [na wanawake]” (2 Nefi 33:1).
Kutoka kwa Maandiko
Kutoka kwa Historia Yetu
Manabii wetu wa zamani wametukumbusha kama wanawake kwamba tuna jukumu muhimu kama walimu nyumbani na Kanisani. Mnamo Septemba 1979, Rais Spencer W. Kimball (1895–1985) alituuliza tuwe “akina dada waandishi.” Alisema: “Kuweni wataalamu wa maandiko—si kuwaweka wengine chini, lakini kuwainua juu! Baada ya yote, ni nani ambaye ana mahitaji makuu ya ‘kuthamini’ kweli za injili (ambazo wanaweza kugeukia wakati wao wa mahitaji) zaidi ya wanavyofanya wanawake na akina mama wanaofanya ulezi na mafundisho mengi?”4
Sisi sote ni walimu na wanafunzi. Tunapofundisha kutoka kwa maandiko na maneno ya manabii wetu hai, tunaweza kusaidia wengine kuja kwa Kristo. Tunaposhiriki katika mchakato wa kujifunza kwa kuuliza maswali ya maana na kisha kusikiliza, tunaweza kupata majibu ambayo yanakidhi mahitaji yetu binafsi.
© 2013 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Imechapishwa USA. Kiingereza kiliidhinishwa: 6/12. Tafsiri iliidhinishwa: 6/12. Tafsiri ya Visiting Teaching Message, July 2013. Swahili. 10667 743