2013
Ulimwengu unahitaji Waanzilishi Leo
Julai 2013


Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Julai 2013

Ulimwengu unahitaji Waanzilishi Leo

Picha
Rais Thomas S. Monson

Kwa wengi, safari ya waanzilishi wa 1847 haikuanza katika Nauvoo, Kirtland, Mbali Magharibi, au New York lakini badala yake nchini Uingereza, Scotland, Scandinavia, au Ujerumani. Watoto wadogo hawakuweza kuelewa kikamilifu imani yenye nguvu iliyowapa motisha wazazi wao kuacha nyuma familia, marafiki, starehe, na usalama.

Mtoto mdogo anaweza kuuliza, “Mama, kwa nini tunaondoka nyumbani? Tunaenda wapi?”

“Njoo nami, uliye mwema; tunakwenda Sayuni, mji wa Mungu wetu.”

Kati ya usalama wa nyumbani na ahadi ya Sayuni palisimama maji yenye hasira na ya kutisha ya bahari kuu ya Atlantiki. Ni nani anayeweza kueleza hofu iliyoshika moyo wa binadamu wakati huo wa mivuko ya hatari? Wakishawishiwa na minong’ono kimya ya Roho, kuendelezwa kwa imani rahisi lakini ya kudumu, Watakatifu hao waanzilishi walimwamini Mungu na kuanza safari yao.

Hatimaye walifika Nauvoo na kutoka mara nyingine kisha kupata shida njiani. Mawekaburi ya mimea na miamba zilitanda kote njiani kutoka Nauvoo hadi Mji wa Salt Lake. Hiyo ndiyo ilikuwa thamani ambayo waanzilishi wengine walilipa. Miili yao imezikwa kwa amani, lakini majina yao yanaishi milele.

Ngombe wachovu walijikokota, magurudumu ya magari yalilia, watu wajasiri walivuja jasho, ngoma za kivita zililia na mbwa mwitu wakabweka Lakini waanzilishi walioongozwa kwa imani na dhoruba walisonga mbele. Waliimba mara nyingi:

Njooni, Njooni, ninyi Watakatifu, hakuna machovu, wala hofu ya kazi;

Bali kwa furaha ielekeze njia yenu.

Ingawa safari hii inaweza kuonekana kwenu kuwa vigumu,

Neema itakuwa kama siku yenu. …

Yote ni sawa! Yote ni sawa!1

Waanzilishi hawa walikumbuka maneno ya Bwana: “Watu wangu ni lazima wajaribiwe katika mambo yote, ili wapate kutayarishwa kupokea utukufu ule nilionao kwa ajili yao, hata utukufu wa Sayuni”2

Kupita kwa wakati kunapunguza kumbukumbu zetu na kupoteza shukrani zetu kwa wale ambao walipitia njia za maumivu, na kuacha nyuma nyayo zenye alama za machozi zenye makaburi yasiyojulikana. Lakini ni vipi kuhusu changamoto za leo? Je, hakuna barabara zenye miamba za kusafiria, hakuna milima zenye mawemawe za kupanda, hakuna ghuba za kuvuka, hakuna mito ya kuvuka? Au kuna haja sana ya sasa kwa yule roho wa waanzilishi kutuongoza mbali na hatari zinazotishia kutumeza na kutuongoza kwa Sayuni ya usalama?

Katika miongo tangu mwisho wa Vita vya Dunia II, viwango vya maadili vimedorora tena na tena. Uhalifu umeongezeka zaidi; adabu kupunguka. Wengi wamo katika mtelezo mkuu wa mwambao wa maafa, wakitafuta raha ya muda wakati wakijinyima furaha ya milele. Hivyo tunapoteza amani.

Tunasahau jinsi Wagiriki na Warumi walivyofanikiwa kiajabu katika ulimwengu katili na jinsi ushindi huo ulivyomalizika—jinsi uzembe na unyonge ulivyowashinda hadi uharibifu wao. Mwishowe, zaidi ya walivyotaka uhuru, walitaka usalama na maisha ya starehe; na walipoteza zote—faraja na usalama na uhuru.

Usikubali ushawishi wa Shetani; badala yake, simama imara kwa ajili ya ukweli. Tamaa isioridhisha ya nafsi haitatimizwa kwa utafutaji wa furaha kwa dhati kukiwa na msisimko wa hisia na uovu. Uovu kamwe haielekezi kwa wema. Chuki kamwe haikuzi upendo. Uwoga kamwe hauleti ujasiri. Shaka kamwe haiimarishi imani.

Wengine wanaipata kuwa vigumu kuhimili hotuba yenye dhihaka na uchafu ya wale wajinga ambao wanakejeli usafi, uaminifu na utiifu kwa amri ya Mungu. Lakini ulimwengu umedunisha uzingatiaji wa kanuni. Wakati Nuhu alipoamuriwa kujenga safina, wale watu wajinga walitazama anga kavu na kisha kudhihaki na kucheka—hadi mvua ikaja.

Ni lazima tujifunze masomo ghali kama hayo tena tena? Wakati unabadilika, lakini ukweli unadumu. Tunaposhindwa kufaidika kutokana na uzoefu wa zamani, tunaweza kuyarudia pamoja na huzuni wake wote, mateso, na dhiki. Je, hatuna hekima ya kumtii Yeye ambaye anajua mwanzo kutoka mwisho—Bwana wetu, ambaye aliunda mpango wa wokovu—badala ya yule nyoka, ambaye alidharau uzuri wake?

Kamusi inafafanua mwanzilishi kama “mtu anayetangulia mbele ili kuandaa au kutengeneza njia kwa wengine kufuata.”3 Je, sisi kwa namna fulani tunaweza kupata ujasiri na uthabiti wa azma ambayo ilikuwa sifa bainifu ya waanzilishi wa kizazi cha zamani? Je wewe na mimi, kwa kweli, tunaweza kuwa waanzilishi?

Najua tunaweza kuwa. Aha, jinsi gani ulimwengu unahitaji waanzilishi leo!

Muhtasari

  1. “Njooni, Njooni, ninyi Watakatifu,” Wimbo, namba. 30.

  2. Mafundisho na Maagano 136:31.

  3. Kamusi ya Kiingereza ya Oxford, 2nd ed. (1989), “pioneer.”

Kufundisha kutoka kwa Ujumbe huu

Maandiko yanaeleza kwamba waalimu wa nyumbani wanapaswa “kuonya, kuelezea, kushawishi, na kufundisha, na kuwakaribisha wote kuja kwa Kristo,” (M&M 20:59). Fikiria kuzungumzia juu ya maonyo na mialiko iliyomo katika ujumbe wa Rais Monson kwa wale unaowatembelea. Unaweza kutaka kujadili pamoja nao njia ya kutambua na kufuata mifano ya haki, kuepuka udanganyifu, na kujifunza kutokana na makosa ya wengine. Waulize wale unaowafundisha jinsi wanavyoweza kuwa waanzilishi leo.

Chapisha