2013
Zawadi ya Jen
Oktoba 2013


Vijana

Zawadi ya Jen

Mwandishi anaishi Utah,USA.

Nilifanya misururu ya chaguzi zenye makosa katika mwaka wangu wa pili katika shule ya upili. Chaguzi hizo zilisababisha matokeo mabaya na huzuni, na niliamua kutumia mapumziko yangu ya msimu wa joto kuanza kufanya mabadiliko. Wakati shule ilipoanza tena, nilikula chakula cha mchana katika chumba cha bafu au kwenye baraza iliyo tupu kuepuka mahusiano mabaya yaliyokuwa yakinisubiri kunikaribisha tena.

Sijawahi kabisa kuhisi mpweke hivi.

Ndipo Mungu akanipa zawadi: Akanitumia Jen. Hakunihukumu kwa makosa yangu lakini badala yake alinishawishi niendelee katika mwelekeo sahihi. Kujua atakuwepo shuleni kulinisaidia kuendelea kusoma maandiko yangu matakatifu na kutunza ushuhuda wangu. Wakati wa mahafali ulipofika nilikuwa, nimejihakikishia mwenyewe kwamba nimeamua kubadilika.

Nashangaa wakati mwingine ningekuwa wapi leo kama Jen asingekuwa nami. Ningeweza kushikilia kanuni zangu bila yeye? Kwa bahati mzuri, siwezi kujua kwa sababu alikuwa pale na moyo wake wote, tayari na kwa hiari yake kunisaidia.

Chapisha