2013
Ujumbe wa Kimungu wa Yesu Kristo:Muumbaji
Oktoba 2013


Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Oktoba 2013

Ujumbe wa Kiungu wa Yesu Kristo: Muumbaji

Kwa maombi jifunze kifaa hiki na kama inavyofaa, jadiliana na akina dada utaowatembelea. Tumia maswali ili kukusaidia kuwaimarisha dada zako na kuufanya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kuwa sehemu hai ya maisha yako mwenyewe. Kwa maelezo zaidi, nenda kwenye www.reliefsociety.lds.org.

Imani • Familia • Usaidizi

Yesu Kristo” Aliumba mbingu na nchi” (3 Nefi 9:15). Alifanya hivyo kupitia nguvu ya ukuhani, chini ya maelekezo ya Baba yetu wa Mbinguni (Ona Musa 1:33).

“Jinsi gani tunapaswa kuwa wenye shukrani kwamba muumbaji mwenye busara aliiunda dunia na kutuweka sisi hapa” alisema Rais Thomas S. Monson,… kwamba tuweze kupata uzoefu wa muda wa kujaribiwa, na nafasi ya kujithibitisha wenyewe ili tuweze kusitahili yale yote Mungu ametutayarishia kuyapokea.1 Tunapotumia wakala wetu kutii amri za Mungu na kutubu, tunapata kustahili kurudi na kuishi Naye.

Kuhusu uumbaji, Rais Dieter F.Uchtdorf, Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza, alisema:

“Sisi ndiyo sababu Yeye aliumba Ulimwengu! …

Huu ni ukweli kinza kwa mtu: akilinganishwa na Mungu, mtu si chochote, na hali sisi ni kila kitu kwa Mungu.2 Kujua kwamba Yesu Kristo aliumba dunia kwa ajili yetu kwa sababu sisi ni kila kitu kwa Baba yetu wa mbinguni kunaweza kutusaidia sisi kuongeza upendo wetu Kwao.

Kutoka kwenye Maandiko

Yohana 1:3; Wahebrania 1:1–2; Mosia 3:8; Musa 1:30–33, 35–39; Ibrahimu 3:24–25

Kutoka kwenye Historia Yetu

Tumeumbwa kwa mfano wa Mungu (Ona Musa 2:26–27), na tuna uwezo wa kiungu Nabii Joseph Smith aliwaonya akina dada walio kwenye Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama waishi kwa kufuatana na wajibu wao.3 Pamoja na ushawishi ule kama msingi, akina dada katika kanisa la Yesu Kristo la watakatifu wa siku za mwisho wamefundishwa kuishi kufuatana na uwezo wao wa kiuungu kwa kukamilisha madhumuni ya Mungu kwa ajili yao. “Wanapokuja kufahamu wao ni nani hasa–Wasichana wa Mungu, wenye tabia toka kuzaliwa ya kupenda na kulea—wanapofikia uwezo wao kama wanawake watakatifu.4

Mnawekwa sasa katika hali ambayo mnaweza kufanya kufuatana na huruma hizo ambazo Mungu amezipanda ndani ya mioyo yenu” Alisema Nabii Joseph Smith Kama mtaishi kufuatana na kanuni hizi ni ukuu na utukufu jinsi gani! —Kama utaishi kwa nafasi yako maalumu, malaika hawatazuiliwa kuwa washirika wako.”5

Muhtasari

  1. Thomas S.Monson, ”Mbio za maisha” Liahona, May 2012, 91.

  2. Dieter F. Uchtdorf, ”Una maana Kwake” Liahona, Nov. 2011, 20

  3. Joseph Smith, in Daughters in My Kingdom: The History and Work of Relief Society (2011), 171.

  4. Daughters in My Kingdom, 171.

  5. Joseph Smith, katika, Daughters in My Kingdom, 169.

Nifanye nini?

  1. Kutafuta kufahamu uwezo wetu wa kiungu unaongeza upendo wetu kwa Mwokozi kwa njia gani?

  2. Tunawezaje kuonyesha shukrani zetu kwa uumbaji wa Mungu?

Chapisha