Upendo—Asili ya Injili
Hakika hatuwezi kumpenda Mungu kama hatuwapendi wasafiri wenzetu katika safari hii ya maisha duniani.
Ndugu na dada zangu wapendwa, wakati Mwokozi wetu alipohudumu miongoni mwa wanadamu, Yeye aliulizwa na wakili aliyetaka kujua, “Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu?
Mathayo imeandikwa kwamba Yesu alijibu:
“Yesu akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.
“Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.
“Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.1
Marko anamalizia tukio kwa kauli ya Mwokozi: “Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.”2
Hakika hatuwezi kumpenda Mungu kama hatuwapendi wasafiri wenzetu katika safari ya hapa duniani. Vile vile, sisi hatuwezi kikamilifu kuwapenda wenzetu kama sisi hatumpendi Mungu, Baba wa sisi sote. Mtume Yohana alitwambia sisi, “Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake pia.”3 Sisi sote ni watoto wa kiroho wa Baba yetu wa Mbinguni, hivyo basi, sisi ni kaka na dada. Tunapokuwa na ukweli huu katika mawazo yetu, kuwapenda watoto wote wa Mungu kutakuwa rahisi.
Hakika, upendo ni asili kabisa ya injili, na Yesu Kristo ni Mfano wetu. Maisha yake ni urithi wa upendo. Wagonjwa aliwaponya; waliogandamizwa aliwainua; mwenye dhambi alimwokoa. Mwishoni kundi la watu wenye hasira likaangamiza maisha Yake. Na bado kuna mwangwi kutoka kilima cha Golgotha ya maneno: “Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo.” 4— maonyesho ya kipeo katika huruma na upendo wa maisha ya duniani.
Kuna sifa nyingi ambazo ni maonyesho ya upendo, kama vile ukarimu, subira, kujitolea, kuelewa, na msamaha. Katika mahusiano yetu yote, sifa hizi na zinginezo kama hizo zitasaidia kufanya kuwa wazi upendo katika mioyo yetu.
Kwa kawaida upendo wetu utaonyeshwa katika mainginiliano yetu na wengine ya siku hadi siku. Kitakachokuwa muhimu sana kitakuwa uwezo wetu wa kutambua mahitaji ya mtu na kisha kujibu. Mimi daima ninafurahia mawazo yanayoonyeshwa katika hili shairi fupi:
Nimelia usiku mzima
Kwa ukosefu wa maono
Hayo kwa mahitaji ya mtu yalinifanya mimi kipofu.
Lakini kamwe sijaweza
Kusikia athari ya majuto
Kwa kuwa mkarimu kiasi.5
Hivi majuzi nilifahamishwa juu ya mfano wa kugusa sana wa upendo mkarimu—mmoja ambao ulikuwa na matokeo yasiyotarajiwa. Ulikuwa mwaka 1933, ambapo kwa sababu ya Mdororo Mkuu, nafasi za ajira zilikuwa nadra. Eneo lilikuwa sehemu ya mashariki mwa Marekani. Arlene Biesecker alikuwa tu ndiye alikuwa amehitimu kutoka shule ya upili. Baada ya kutafuta ajira kwa muda mrefu, yeye hatimaye aliweza kupata kazi katika kiwanda cha nguo kama mshonaji. Wafanya kazi wa kiwanda walikuwa wanalipwa tu kwa vile vipande walivyoshona pamoja kwa ukamilifu kila siku. Jinsi vipande vingi walivyoshona, ndivyo walivyolipwa.
Siku moja baada ya kuanza kazi katika kiwanda, Arlene alipambana na utaratibu ambao ulimkanganya na kumvunja moyo. Yeye alikaa kwenye mashini akijaribu kufumua majiribio yaliyoshindikana ili kukamilisha kipande ambacho alikuwa anafanyia kazi. Ilionekana kama hamna mtu wa kumsaidia, kwani washonaji wengine walikuwa wanaharakisha kukamilisha vipande vingi inavyowezekana. Arlene alihisi kukosa usaidizi na matumaini. Kimya, alianza kulia.
Upande mwengine kutoka kwa Arlene alikaa Bernice Rock. Alikuwa mzee na mwenye ujuzi zaidi kama mshonaji. Akiangalia masumbuko ya Arlene, Bernice aliacha kazi yake mwenyewe na kwenda upande wa Arlene, kwa ukarimu kutoa maelezo na msaada. Alikaa mpaka Arlene akapata kujiamini na kuweza kukamilisha kipande kimoja. Bernice akarudi kwa mashini yake, baada ya kukosa nafasi ya kukamilisha vipande vingi sana ambavyo angeweza kutengeneza, kama hangesaidia.
Kwa tendo hili moja la upendo wa dhati, Bernice na Arlene wakawa marafiki wa maisha. Wote wakaolewa na kuwa na watoto. Wakati fulani katika miaka ya 1950, Bernice, ambaye alikuwa mshiriki wa Kanisa, alimpatia Arlene na familia yeke nakala ya Kitabu cha Mormoni. Mnamo 1960, Arlene na mumewe na watoto wake walibatizwa kama washiriki wa Kanisa. Baadaye walifunganishwa katika hekalu la Mungu.
Kama matokeo ya ukarimu ulioonyeshwa na Bernice alipokwenda kusaidia mtu ambaye yeye hakumjua lakini ambaye alikuwa kwenye masumbuko na alihitaji msaada, watu wasio na hesabu, wote walio hai na wafu, sasa wanafurahia ibada za ukoaji ya injili.
Kila siku ya maisha yetu sisi tunapatiwa nafasi za kuonyesha upendo na ukarimu kwa wale walio karibu nasi. Alisema Rais Spencer W. Kimball: “Sisi sharti tukumbuke kwamba wale watu tuliokutana nao katika bustani, ofisi, lifti, na mahali pengine katika sehemu ya wanadamu Mungu ametupa sisi nafasi ya kupenda na ya kuhudumu. Itatusaidia kidogo kuongea juu ya undugu mkuu wa wanadamu kama hatuwezi kutuwathamini wale ambao waliokaribu nasi kama kaka na dada zetu.”6
Kila mara nafasi zetu za kuonyesha upendo wetu huja bila kutarajiwa. Mfano wa nafasi kama hizo ilitokea kwenye makala ya gazeti katika Oktoba ya 1981. Nilikuwa nimevutiwa na upendo na ukarimu kama huo uliosemwa hapo ambao nimeweka makala iliyokatwa katika faili zangu kwa zaidi ya miaka 30.
Makala yanaonyesha kwamba ndege ya Alaska Airlines ya moja kwa moja kutoka Anchorage, Alaska, hadi Seatle, Washington---ikibeba abiria 150 ---iligeuezwa kwenda mji mdogo wa Alaska ili kumsafirisha mtoto aliyejeruhiwa sana. Mvulana wa miaka miwili alikuwa amekatwa mshipa wa damu katika mkono wake wakati aliangukia kipande cha kioo akicheza karibu na nyumbani kwao. Mji ulikuwa maili 450 (725 kilometa) kusini mwa Anchorage na kwa hakika haikuwa njia ya safari za ndege. Hata hivyo, wahudumu wa hospitali huko walituma maombi ya msaada, na kwa hivyo ndege iligeuzwa kwenda kumchukua mtoto huyu na kumpeleka Seatle ili kwamba aweze kupata matibabu katika hospitali.
Wakati ndege ilipotua katika mji mdogo, wahudumu wa hospital walimtaarifu rubani kwamba mvulana alikuwa anavuja damu sana na hangeweza kusafiri hadi Seatle. Maamuzi yalifanywa ya kusafiri maili 200 (320 kilometa) mbali na njia hadi Juneau, Alaska, mji ulio karibu wenye hospitali.
Baada ya kumsafirisha mvulana hadi Juneau, ndege ilielekea Seatle, sasa ikiwa masaa mengi kama imechelewa. Hakuna abiria hata mmoja ambaye alilalamika, hata ingawa wengi wao walikosa miadi yao na ndege miunganisho. Kwa kweli, dakika na masaa yaliposonga mbele, walifanya michango, kupata kiwango kikubwa kwa mvulana na familia yake.
Ndege ilipokuwa karibu kutua katika Seatle, abiria walijawa na furaha wakati rubani alipotangaza kwamba amepokea habari kwa njia ya redio kwamba mvulana atakuwa salama.7
Akilini mwangu yanakuja maneno ya maandiko: “Lakini hisani ni upendo msafi wa Kristo, … na yeyote atakayepatikana nayo katika siku ya mwisho, itakuwa vyema kwake.”8
Ndugu na kina dada, baadhi ya nafasi kubwa za kuonyesha upendo wetu zitakuwa katika kuta za nyumbani mwetu wenyewe. Upendo unafaa kuwa kitovu cha maisha ya familia, na hali mara nyingi sivyo. Kunaweza kuwa na ukosefu wa subira, mabishano mengi, vita vingi sana, majonzi mengi sana. Rais Gordon B. Hinckley alisikitika: “Kwa nini [wale] tunaowapenda [sana] wanakuwa kila mara wanalengwa wa maneno yetu makali? Kwa nini [sisi] wakati mwengine tunasema kama kwa visu ambavyo vinakata upesi?”9 Majibu ya maswali haya yanaweza kuwa tofauti kwa kila mmoja wetu, na hali jambo la msingi ni kwamba sababu hazijalishi. Kama sisi tutaweka amri ya kupendana mmoja na mwengine, sisi sharti tutendeane kwa ukarimu na heshima.
Kwa kweli kutakuwa na nyakati ambapo nidhamu inahitajika kutolewa acha sisi tukumbuke, hata hivyo, ushauri unaopatikana katika Mafundisho na Maagano—hasa, ambapo inakuwa ni muhimu kwetu sisi kurudiana mmoja na mwengine, sisi baadaye kuonyesha ongezeko la upendo.10
Mimi ningetumaini kwamba sisi tungejitahidi daima kuwa wazingativu na kuwa wasikivu kwa mawazo na hisia na hali za wale walio karibu nasi. Acha sisi tusidharau au tusipuuze. Badala yake, acha tuwe na huruma na wenye kutia moyo. Sisi ni sharti tuwe makini kwamba tusiharibu kujiamini kwa mtu mwengine kupitia maneno au matendo ya kiholela.
Msamaha unafaa kwenda pamoja bega kwa bega na upendo. Katika familia zetu, vile vile na marafiki zetu, kunaweza kuwa na hisia za kuumizwa na kutoelewana. Tena, haijalishi sana jambo ni ndogo kiasi gani. Haiwezi na haifai kuachwa kuharibu, kereketa, na hatimaye kuangamiza. Lawama huacha vidonda kuwa wazi. Msamaha pekee ndio huponya.
Mwanamke mwema ambaye kwa sasa ameshaaga dunia alizungumza nami siku moja na bila kutarajia alisimulia majuto fulani. Aliongea juu ya tukio ambalo lilitokea miaka mingi iliyopita mapema na lilihusisha mkulima jirani, wakati mmoja rafiki mwema lakini ambaye yeye na mumewe walikuwa wamekosana mara nyingi. Siku moja mkulima aliomba atumie njia ya mkato kupitia katika shamba lake ili afike shambani mwake. Wakati huu alitua katika usimulizi wake kwangu na, kwa sauti ya kutetemeka, alisema, “Ndugu Monson, mimi sikumuacha yeye apitie kwenye shamba letu wakati huo au siku zote bali nilimhitaji yeye achukue njia ndefu kwa miguu kufikia shamba lake. Mimi nilikuwa na makosa, na mimi najuatia hayo. Ameshaenda sasa, lakini eh, mimi natamani ningesema kwake, ‘Nimekosa sana.’ Jinsi gani natamani ningepata nafasi ya pili ya kuwa mkarimu.”
Nilipokuwa ninamsikiliza, kulikuja katika akili yangu utambuzi wa kuhuzunisha wa John Greenleaf Whittier: “Kati ya maneno yote ya huzuni ya ulimi au kalamu, cha kuhuzunisha sana ni: Ingeweza kuwa!”’’’11 Ndugu na kina dada, tunapowatendea wengine kwa upendo na ukarimu wa kuzingatia, sisi tutaepuka majuto kama hayo.
Upendo unaonyeshwa kwa njia nyingi za kutambulika: tabasamu, kupunga mkono, neno la ukarimu, pongezi. Maonyesho mengine yanaweza kuwa si wazi sana, kama vile kuonyesha upendeleo wa shughuli za wengine, kufundisha kanuni kwa ukarimu na subira, kutembelea mtu ambaye ni mgonjwa au hajiwezi kutoka nyumbani. Maneno na vitendo hivi, na vingine vingi, vinaweza kuwasilisha upendo.
Dale Carnegie, mtunzi Mmarekani maafuru na mhadhiri, aliamini kwamba kila mtu anayo ndani yake “uwezo wa kuongeza jumla ya furaha ya ulimwengu … kwa kutoa maneno machache ya shukrani ya kweli kwa mtu ambaye ni mpweke au amevunjika moyo.” Alisema, “Labda utaweza kusahau kesho maneno ya ukarimu unayosema leo, lakini mpokeaji ataweza kuyafurahia katika maisha yake yote.”12
Na tuanze sasa, siku ya leo, kuonyesha upendo kwa watoto wote wa Mungu, iwe wao ni wanafamilia wetu, marafiki zetu, watu tunaofahamiana, au hata wageni tu. Tunapoamka kila asubuhi, acha sisi tuamue kujibu kwa upendo na ukarimu kwa kile chochote kinachoweza kuja njia yetu.
Zaidi ya ajili ya ufahamu, ndugu na kina dada, ni upendo wa Mungu kwetu sisi. Kwa sababu ya upendo huu. Yeye alimtuma Mwanawe, ambaye alitupenda sisi ya kutosha kutoa maisha Yake kwa ajili yetu, kwamba tuweze kupata uzima wa milele. Tulipokuja kuelewa kipawa hiki kisischokuwa na kifani, mioyo yetu itajawa na upendo kwa Baba yetu wa Milele, kwa Mwokozi wetu, na kwa wanadamu wote. Kwamba hiyo iwe hivyo ndiyo maombi yangu ya dhati katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina
© 2014 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Printed in USA. English approval: 6/13. Translation approval: 6/13. Tafsiri ya First Presidency Message, May 2014. Swahili. 10865 743