2014
Wito Mtakatifu wa Yesu Kristo: Kuhudumu
June 2014


Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Juni 2014

Wito Mtakatifu wa Yesu Kristo: Kuhudumu

Ukiwa umeomba soma jarida hili na ujaribu kujua ni nini cha kushiriki. Ni jinsi gani kuelewa maisha na utumishi wa Mwokozi kunaweza kuongeza imani katika Yeye na kuwabariki wale unaowaangalia kwa kupitia utembelezi wa nyumabni? Kwa maelezo zaidi, nenda kwenye www.reliefsociety.lds.org.

Imani • Familia • Usaidizi

Tunapowahudumia wengine, tunakuwa wafuasi wa kweli wa Yesu Kristo, ambaye alituonyesha mfano. Rais Thomas S. Monson alisema: “Tumezungukwa na wale walio na mahitaji. Sisi ndiyo mikono ya Bwana hapa duniani, tukiwa na jukumu la kuwatumikia na kuwainua watoto Wake.”1

Linda K.. Burton, rais wa Urais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, alifundisha: “Kwa kufanya mazoezi, kila mmoja wetu anaweza kuwa kama Mwokozi pale tunapowatumikia watoto wa Mungu. Ili tuweze [kutumikiana] wenyewe kwa wenyewe, ningependa kupendekeza maneno manne ya kukumbuka: ‘Kwanza chunguza, kisha tumikia.’ Tunapofanya hivyo, tunatii maagano, na utumishi wetu, kama Rais Monson, utakuwa ushahidi wa ufuasi wetu.”2

Tunaweza kuomba kila asubuhi ili kutambua fursa za kuwatumikia wengine. “Baba wa Mbinguni atakuongoza, na malaika watakusaidia,” alisema David L. Beck, Rais Mkuu wa Vijana. “Utapewa nguvu za kubariki maisha na kuokoa nafsi.”3

Kutoka katika Maandiko

Mathayo 20:25–28; 1 Nefi 11:27–28; 3 Nefi 28:18

Kutoka kwenye Historia Yetu

Kwenye mkutano mkuu wa Oktoba 1856, Rais Brigham Young (1801 –77) alitangaza kwamba mikokoteni ya watangulizi ilikuwa bado inasafiri nyikani na kwamba kila mmoja alitakiwa kusaidia kuchangia mahitaji kwa ajili yao mara moja. Lucy Meserve Smith aliandika kwamba wanawake “walivua sketi zao [sketi kubwa], soksi, na kila kitu walichoweza kupeana, pale kwenye tabenakulo, na kuzijaza kwenye mkokoteni.

Wakati watangulizi waokoaji walipoanza kuwasili Mjini Salt Lake, Lucy aliandika, “Mimi kamwe sikuchukua zaidi furaha katika kazi yangu niliyowahi kuifanya maishani mwangu, uelewano wa hisia za aina hii ulishinda. Ilinibidi tu niende dukani na kuwajulisha mahitaji yangu; kama ilikuwa nguo, ilipimwa bila gharama.4

Raisi George Albert Smith (1870–1951) alisema kuhusu kuwatumikia wengine: “Furaha yetu ya milele itatoshana na jinsi sisi wenyewe tunavyojitolea kuwasaidia wengine.”5

Fikiria Hili

  1. Maombi yanawezaje kutuongoza kuwa nyenzo katika mikono ya Bwana?

  2. Kuhudumia wengine kunawezaje kutusaidia kuweka maangano yetu?

Muhtasari

  1. Thomas S. Monson, “What Have I Done for Someone Today?” Liahona,Nov. 2009, 86.

  2. Linda K. Burton, “Kwanza Chunguza, Kisha Tumikia,” Liahona, Nov. 2012, 78, 80.

  3. David L. Beck, “Your Sacred Duty to Minister,” Liahona, May 2013, 56.

  4. Lucy Meserve Smith, in Daughters in My Kingdom: The History and Work of Relief Society (2011), 36 –37.

  5. George Albert Smith, in Daughters in My Kingdom, 77.