2014
Utume Mtakatifu wa Yesu Kristo: Mkate wa Uzima
Oktoba 2014


Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Oktoba 2014

Utume Mtakatifu wa Yesu Kristo: Mkate wa Uzima

Kwa maombi soma mambo haya na utafute kujua kile cha kushiriki. Kuelewa maisha na ujumbe wa Mwokozi kutaongezaje imani yako Kwake na kubariki wale unaowaongoza kupitia ualimu tembelezi? Kwa taarifa zaidi, nenda kwenyereliefsociety.lds.org.

Imani, Familia, Usaidizi

Yesu alisema, “Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele.” (Yohana 6:51). “Yesu anatufundisha, wanafunzi Wake, kwamba tunapaswa kumtegemea Mungu kila siku kwa ajili ya mkate—msaada na riziki—tunayohitaji katika siku fulani,” alisema Mzee D. Todd Christofferson wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili. “Mwaliko wa Bwana unazungumzia juu ya Mungu wa upendo, anayefahamu hata mahitaji madogo ya kila siku ya watoto Wake na mwenye hamu ya kuwasaidia, mmoja kwa mmoja. Anasema kwamba tunaweza kuomba kwa imani kwa Kiumbe huyo, ambaye ‘huwapa wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.’ (Yakobo 1:5).”1 Tunapofahamu kwamba Yesu Kristo atatoa kwa ajili ya mahitaji yetu, tutamgeukia kwa riziki yetu ya kiroho.

Mzee Jeffrey R. Holland wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili anatualika “kujiunga katika matukio ya wanafunzi wa mwanzo wa Kristo, ambao pia walitamani mkate wa uzima—wale ambao hawakurudi lakini walimjia, walikaa pamoja Naye, na ambao walitambua kwamba kwa ajili ya usalama na wokovu hapakuwa na mwingine ambaye wangeweza kumwendea.”2

Maandiko ya Ziada

Yohana 6:32–35; Alma 5:34; 3 Nefi 20:3–8

Kutoka kwenye Maandiko

Yesu Kristo alikuwa akifundisha kundi kubwa la watu zaidi ya 4,000. Baada ya siku tatu, aliwaambia wanafunzi Wake: “Nauhurumia huu umati kwa sababu hawana kitu cha kula;

“Nami nikiwaaga waende zao nyumbani hali wanafunga, watazimia njiani. …

“Wanafunzi wake wakamjibu, Je! Ataweza wapi mtu kuwashibisha hawa mikate hapa nyikani?

“[Yesu] Akawauliza, Mnayo mikate mingapi? Wakasema, Saba.”

Kisha Kristo “akaitwaa ile mikate saba, akashukuru, akaimega, akawapa wanafunzi wake wawaandalie; 

“Walikuwa na visamaki vichache; akavibariki, akasema wawaandalie na hivyo pia.

“Hivyo wakala, wakashiba, wakakusanya mabaki ya vipande vya mikate makanda saba.” (Ona Marko 8:1–9.)

Muhtasari

  1. D. Todd Christofferson, “Recognizing God’s Hand in Our Daily Blessings,” Liahona, Jan. 2012, 25.

  2. Jeffrey R. Holland, “He Hath Filled the Hungry with Good Things,” Liahona, Jan. 1998, 76.

Zingatia Haya

Tunapokuja kwa Kristo, Yeye hutuboresha vipi?