2014
Jiandae kabla ya Kuomba
Oktoba 2014


Vijana

Jiandae kabla ya Kuomba

Rais Eyring anatukumbusha kwamba maombi “ni mawasiliano ya pande mbili kati ya Mungu na watoto Wake.” Kuchukua muda wa kujiandaa kwa ajili ya maombi yetu kunaweza kufanya mawasiliano hayo ya pande mbili kuwezekana. Unaweza kutumia jarida lako kwa kuchukua dakika chache kuandaa kuomba kila siku. Unaweza kutengeneza orodha ya baraka ambazo kwazo unataka kumshukuru Baba wa Mbinguni, watu ambao wanahitaji maombi yako, na maswali ambayo ungetaka yajibiwe. Kisha mkaribishe Roho kwa kuimba wimbo au kusoma mistari michache ya maandiko. Unapoomba, sikiliza kwa makini jinsi Roho Mtakatifu anavyoongoza kile unachopaswa kusema, na usikilize kwa makini hisia zako na mawazo yako. (ona M&M 8:2–3). Fikiria kurekodi yale unayoyapitia katika jarida lako na kupitia upya majibu unayopokea. Unaweza pia kutumia shughuli zilizoko kwenye kurasa 95–97 za Hubirini Injili Yangu: Mwongozo kwa Huduma ya Misionari ili kukusaidia kutathmini maombi yako na kujifunza kutambua Roho Mtakatifu.

Chapisha