Ujumbe wa Mwalimu MTEMBELEAJI, Januari 2016
Familia: Tangazo kwa Ulimwengu
Kwa maombi jifunze maneno haya na utafute kujua kitu cha kushiriki. Kuelewa fundisho la familia kutawabariki vipi wale unaowachunga kwa njia ya ualimu wa kutembelea? Kwa taarifa zaidi, nenda kwenye reliefsociety.lds.org.
Katika mkutano mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama katika mwaka wa 1995, wakati Rais Gordon B. Hinckley (1910–2008) alisoma kwa mara ya kwanza Familia: Tangazo kwa Ulimwengu, Bonnie L. Oscarson, rais mkuu wa Wasichana, alisema: “Tulikuwa na shukrani kwa ajili ya na kuthamini uwazi, urahisi, na ukweli wa hati hii ya ufunuo. Tangazo kwa familia limekuwa kigezo chetu cha kupima falsafa za ulimwengu, na mimi nashuhudia kwamba kanuni zilizowekwa ni za kweli hata leo kama zilivyokuwa wakati zilifunuliwa kwetu na nabii wa Mungu karibu miaka 20 iliyopita.”1
Kutoka kwa tangazo kwa familia, ongeza Carole M. Stephens, mshauri wa kwanza katika urais mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, “tunajifunza, ‘katika eneo la kabla kuzaliwa, wana na mabinti wa kiroho walimjua na walimwabudu Mungu kama Baba yao wa Milele’2 …
“… Kila mmoja wetu yu katika familia na anahitajika katika familia ya Mungu.”3
Sisi tunaishi katika wakati ambapo ni lazima wazazi walinde nyumba zao na familia zao. Familia: Tangazo kwa Ulimwengu linaweza kutuongoza.
Maandiko ya Ziada
Hadithi Hai
“Lee Mei Chen Ho kutoka Kata ya Tatu ya Tao Yuan, Kigingi cha Tai Yuan Taiwan, alisema tangazo limemfundisha kwamba mahusiano ya familia yanasaidia kukuza silka za uungu kama vile imani, subira, na upendo. ‘Ninapojaribu kujiendeleza mwenyewe kulingana na tangazo hili, ninaweza kupata furaha ya kweli,’ yeye alisema.”4
Barbara Thompson, ambaye alikuwepo wakati tangazo liliposomwa kwa mara ya kwanza na baadaye akahudumia kama mshauri katika urais mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, alisema: “Niliwaza kwa muda mchache kwamba [tangazo kwa familia] kihalisi haikunihusu sana mimi kwa kuwa sikuwa nimeolewa na sikuwa na watoto wowote. Lakini ghafula nilivyokuwa nikifikiria, lakini linanihusu mimi. Mimi ni mwanafamilia. Mimi ni binti, dada, shangazi, binamu, mpwa, na mjukuu wa kike. … Hata kama ningekuwa mwanafamilia pekee aliye hai, mimi bado ni mwanafamilia wa familia ya Mungu.”5
© 2016 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Imechapishwa Marekani. Kiingereza kiliidhinishwa: 6/15. Tafsiri iliidhinishwa: 6/15. Tafsiri ya Visiting Teaching Message, January 2016. Swahili 12861 743.