Ujumbe wa Mwalimu MTEMBELEAJI, Juni 2016
Maagizo na Maagano ya Hekalu
Kwa maombi jifunze maneno haya na utafute kujua kitu cha kushiriki. Je, kuelewa “Tangazo kwa Ulimwengu” kutazidisha vipi imani yako kwa Mungu na kubariki wale unaowachunga kupitia ualimu wa kutembelea? Kwa maelezo zaidi, nenda kwenye reliefsociety.lds.org.
Ibada zote zinazohitajika kwa ajili ya wokovu na kuinuliwa zinaambatana na maagano ya Mungu. “Kuweka na kutii maagano ina maana kuchagua kujifunga wenyewe kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo,” alisema Linda K. Burton, rais mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa kina Mama.1
Mzee Neil L. Andersen wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alisema, “Bwana alisema, ‘Katika maagizo … uwezo wa uungu unadhihirishwa.’
“Kuna baraka maalum zitokazo kwa Mungu kwa ajili ya kila mtu anayestahili aliyebatizwa, anapokea Roho Mtakatifu, na kupokea sakramenti kila mara.”2
“Wakati wanaume na wanawake wanapokwenda hekaluni,” alisema Mzee M. Russell Ballard wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, “wote wanakuwa wameunganishwa kwa uwezo huo huo, ambao ni uwezo wa ukuhani …
“… Wanaume wote na wanawake wote wana kibali cha nguvu hii kwa ajili ya usaidizi katika maisha yao wenyewe. Wote ambao wamefanya maagano matakatifu na Bwana na wanaoheshimu maagano hayo wanastahili kupokea ufunuo wa kibinafsi, kubarikiwa na utumishi wa malaika, na kuzungumza na Mungu, kupokea utimilifu wa injili, na, hatimaye, kuwa warithi ubavuni mwa Yesu Kristo ya yote aliyonayo Baba.”3
Maandiko ya Ziada
Hadithi Hai
Mwaka 2007, siku nne baada ya tetemeko kubwa la ardhi huko Peru, Mzee Marcus B. Nash wa Sabini alikutana na rais wa tawi Wanceslao Conde na mke wake, Pamela. “Mzee Nash alimwuliza Dada Conde watoto wao wadogo walikuwa wapi. Akiwa na tabasamu, alijibu kwamba kwa neema ya Mungu wote walikuwa salama na wazima. Aliulizia juu ya nyumba ya familia ya Conde.
“‘Imebomoka, alisema kwa urahisi.
“… ’Na bado,’ Mzee Nash alisema, ‘unatabasamu wakati tukiongea.’
“‘Ndio,’ alisema, ’nimeomba na nipo katika amani. Tuna kila kitu tunachohitaji. Tupo pamoja, tunao watoto wetu, tumeunganishwa hekaluni, tunalo Kanisa hili zuri, na tunaye Bwana. Tunaweza kuijenga tena kwa usaidizi wa Bwana. …
“Ni nini juu ya kufanya na kutii maagano na Mungu ambako kunatupa sisi uwezo wa kutabasamu wakati wa shida, kuyageuza mateso kuwa ushujaa … ?”
“Chanzo ni Mungu. Njia yetu ya kufikia kwenye uwezo ule ni kwa njia ya maagano yetu na Yeye.”4
© 2016 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Imechapishwa Marekani. Kiingereza kiliidhinishwa: 6/15. Tafsiri iliidhinishwa: 6/15. Tafsiri ya Visiting Teaching Message, June 2016. Swahili. 12866 743