2017
Upatanisho wa Kristo Ni Ushahidi wa Upendo wa Mungu.
Februari 2017


Ujumbe wa Mwalimu Mtembeleaji, Februari 2017

Upatanisho wa Kristo Ni Ushahidi wa Upendo wa Mungu

Kwa maombi jifunze maneno haya na utafute msukumo wa kujua kitu cha kufundisha.

Picha
Nembo ya Muungano wa Usaidizi wa wakina Mama

Imani, Familia, Usaidizi

Kuelewa kwamba Baba yetu wa Mbinguni alimtoa Mwanawe wa Pekee ili tuweze kuwa na maisha ya milele na uwezekano wa uzima wa milele hutusaidia kuhisi upendo wa Mungu usio na kikomo na upendo usiotambulika vyema kwetu sisi. Mwokozi wetu pia anatupenda.

“Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? …

“Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo,

“Wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu” (Warumi 8:35, 38–39).

Kuhusu mateso ya Yesu Kristo, Mzee D. Todd Christofferson wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alisema: “Mateso ya Mwokozi kule Gethsemane na uchungu wake msalabani vinatukomboa kwa kutosheleza matakwa ya haki juu yetu. Anawaonyesha huruma na kuwasamehe wale wanaotubu: Upatanisho wa Yesu Kristo pia unatosheleza deni tunalodai haki kwa kuponya na kutoa fidia kwetu kwa mateso tunayopitia bila hatia. ‘Kwani tazama, anapokea maumivu ya wanadamu wote, ndio, maumivu ya kila kiumbe kinachoishi, waume kwa wake, na watoto, ambao ni wa familia ya Adamu’ (2 Nefi 9:21; tazama pia Alma 7:11–12).”1

Kristo “ametuchora [sisi] katika viganja vya mikono [Yake] ” (Isaya 49:16). Linda K. Burton, Rais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama, anasema, “Lile tendo kuu la upendo linapaswa kusababisha kila mmoja wetu kupiga magoti na kusali kwa unyenyekevu kumshukuru Baba yetu wa Mbinguni kwa kutupenda kiasi cha kumtuma Mwanawe wa Pekee na Mkamilifu kuteseka kwa ajili ya dhambi zetu, huzuni, na yote yanayoonekana siyo ya haki maishani mwetu.”2

Maandiko na Maelezo ya Ziada

Yohana 3:16; 2 Nefi 2:6–7, 9; reliefsociety.lds.org

Muhtasari

  1. D. Todd Christofferson, “Ukombozi,” Liahona, Mei 2013, 110.

  2. Linda K. Burton, “Je, Imani Katika Upatanisho wa Yesu Kristo Imeandikwa Mioyoni Mwetu?” Liahona, Nov. 2012, 114.

Zingatia Hili

Tunawezaje kutoa shukrani na upendo kwa Mungu na kwa Yesu Kristo kwa ajili ya zawadi ya Upatanisho wa Mwokozi?

Chapisha