2017
Wa Moyo Mmoja
September 2017


Ujumbe wa Ualimu wa Kutembelea, Septemba 2017

Wa Moyo Mmoja

Kwa maombi jifunze nyenzo hii na utafute mwongozo ili kujua kitu cha kushiriki. Ni kwa namna gani kuelewa madhumuni ya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kunawatayarisha mabinti wa Mungu kwa ajili ya baraka za uzima wa milele?

Nembo ya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama

Imani Familia Usaidizi

“Bwana akawaita watu wake Sayuni, kwa sababu wao walikuwa wa moyo mmoja na wazo moja, na waliishi katika haki; na hapakuwa na maskini miongoni mwao” (Musa 7:18). Tunawezaje kuwa kitu kimoja?

Mzee M.Russell Ballard wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alisema: “Katikati mwa neno la Kingereza atonement ni neno moja. Ikiwa binadamu wote wangeelewa hili, hatungekuwa na mtu yeyote ambaye hatungemjali, bila ya kuzingatia rika, utaifa, jinsia, dini, au hali ya kimaisha na kiuchumi. Tungejitahidi kumuiga Mwokozi na hatungekuwa na uhasama, wenye kutojali, wenye kukosa heshima, au wasiojali hisia za wengine.”1

Rais Henry B. Eyring, Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza, alifundisha: “Mahali ambapo watu wako pamoja na Roho, [wao] wanaweza kutarajia amani. Roho wa Mungu kamwe huwa haleti ubishi (ona 3 Nefi 11:29). … Huelekeza kwa amani binafsi na hisia ya umoja na wengine.”2

Akizungumzia changamoto za familia, Carole M. Stephens, aliyehudumu kama Mshauri wa Kwanza katika Urais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, alisema: “Mimi kamwe sijapata kupitia talaka, machungu na utovu wa usalama ambao hujitokeza kutokana na kutelekezwa, au majukumu yanayohusiana na mama ambaye hajaolewa. Sijapatwa na kifo cha mtoto, utasa, au mvuto wajinsia moja. Sijapata kupatwa na udhalimu au ugonjwa sugu, au ulevi. Hazijakuwa fursa zangu za upanuzi wangu.

“… Lakini kupitia majaribu na majaribio yangu binafsi … Nimepata kumfahamu vyema Yule ambaye anaelewa. …Zaidi ya hayo, nimeshapatwa na mithani yote ya duniani ambayo nimetaja kupitia jicho la binti, mama, bibi, dada, shangazi, na rafiki.

“Nafasi yetu kama mabinti wa Mungu washika-maagano siyo kujifunza kutokana na changamoto zetu wenyewe; ni kuungana katika huruma na fadhili tunapowasaidia wana familia wengine wa familia ya Mungu katika shida zao.”3

Maandiko na Maelezo ya Ziada

Yohana 17:20–23; Waefeso 4:15; Mosia 18:21–22; 4 Nefi 1:15;

reliefsociety.lds.org

Muhtasari

  1. M. Russell Ballard, “The Atonement and the Value of One Soul,” Liahona, Mei 2004, 86.

  2. Henry B. Eyring, “That We May Be One,” Ensign, Mei 1998, 67.

  3. Carole M. Stephens, “Familia ni ya Mungu,” Liahona, Mei 2015, 11–12.